WanaJF,
Pamoja na kwamba mzee Lowassa kwa sasa amesitisha harakati zake za utangazaji wa nia ya kuelekea magogoni kufuatia amri ya chama, ila kuna nguvu ya ziada kutoka kwa wapenzi wake inayoendelea kumshawishi kutangaza nia na kuendelea na safari yake ya matumaini.
Leo kwa mara ya kwanza nakiri kwenu wanaJF kuwa Lowassa hahusiki kwa namna yoyote kupanga ama kuratibu vikundi vya watu kufanya maigizo ya kumshawishi, bali ni umati wenyewe ndio wenye mapenzi kwa huyo mzee.
Baada ya makamu wa rais kumuomba Lowassa akamwakilishe katika harambee ya waislamu ya ujenzi wa msikiti, Mhe Lowassa alifika na zoezi lilianza mara moja la harambee. Zoezi lilikwenda kama ilivyopangwa isipokuwa lengo la kiwango walichokihitaji waislamu kilizidi takribani kwa mara mbili na kufikia takribani Milioni mia tatu.
Hali hiyo iliwafanya waislamu (kulikuwa na uwakilishi kutoka maeneo mbalimbali nchini), kwa msimamo wao mmoja kutoa tamko la kumuunga mkono Lowassa katika safari yake ya matumaini! Hali ambayo ilipokelewa kwa furaha na waumini wengi wa dini ya kiislamu waliohudhuria harambee hiyo.
Lowassa akiwasili kwenye eneo la tukio.
Hapa akiwa anasalimiana na mashekhe mbalimbali.
Lowassa akipatiwa shukrani baada ya kukamilisha zoezi la harambee.
Maelfu ya watu walijitokeza kwenye harambee hizo.
Note: Pesa hizo zitatumika kujengea msikiti ambao utaenda sambamba na uanzishwaji wa kituo cha kulelea watoto yatima na wanaoishi kwenye mazingira magumu.
My take,
Kweli mafuriko hayawezi kuzuiliwa kwa kiganja.