PAYE
JF-Expert Member
- Jun 19, 2025
- 354
- 395
Waislamu kutoka maeneo mbalimbali ya Dar es Salaam asubuhi ya leo Oktoba 25, wamefika katika Msikiti wa Nurul-Hikma ulioko Mtaa wa Yombo, karibu na Mwembe Yanga, Temeke kwa ajili ya Kongamano la Amani na Dua Maalumu ya Kuliombea Taifa.
Mkurugenzi wa Al-Hikma Foundation, waandaaji wa dua na kongamano hilo, Sheikh Nurdeen Kishki, amesema miongoni mwa mambo makubwa yatakayofanyika ni kusoma Qur’an Tukufu nzima mara tano, ambapo kila hatua inapomalizika mashekhe wanahitimisha kwa dua.
Soma: Maombi na dua maalum yafanyika kuliombea taifa kuelekea uchaguzi mkuu wa Oktoba 29, 2025
Sheikh Kishki amesema lengo ni kumwomba Mwenyezi Mungu, kupitia maneno matukufu yaliyo katika Kitabu chake aendelee kuijalia Tanzania amani na utulivu ili uchaguzi upite salama, kwani bila amani hata ibada haziwezi kufanyika.
Mgeni rasmi katika kongamano hilo, linaloshirikisha mashekhe na viongozi mbalimbali wa dini ya Kiislamu, anatarajiwa kuwa Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zubeiry bin Ally Mbwana.
Jana Ijumaa (Oktoba 24, 2025) Rais wa Al-Hikma Foundation, Sheikh Sharif Abdulqadir Al-Ahdal, alisema miaka ya nyuma kila unapofika wakati wa uchaguzi, taasisi hiyo ilikuwa ikisoma dua kivyake, lakini safari hii wameona umuhimu wa kushirikisha Waislamu wengi wa Dar es Salaam.