Eh! Kumbe Waislam si Watanzania.Asalam Aleikum waungwana. Leo mimi kama mtanzania mwenye uchungu na watanzania wa dini zote naomba kuchukua nafasi hii kuwashauri ndugu zangu waislamu. ACHANENI NA CCM INAWALOSTISHA. SAbabu ni nyingi ila nawapa hizi chache hapa chini:
Hivi unafikiri Waislamu ni wajinga? yaani unataka kuwafundisha na kuwaonyesha wapi ndipo kunapowafaa? yaani wao hawajui wala hawaoni? sasa kama unawashauri Waislamu wajiondoe CCM NA SIDHANI kuwa waislamu wote wako CCM kwani wako wengi wasio na chama, wengine wako CUF, wengine wako CDM, na hata NCCR! una chama kingine mbadala ambacho kitawahakikishia Waislamu kupata mahakama ya kadhi, OIC, na haki zao zote?
Mimi nina suluhisho la Mahakama ya Kadhi na OIC! Mahakama za Kadhi zianzishwe na waislamu wenyewe na kugharamiwa nao! OIC wajiunge BAKWATA ambayo inawahusu Waislamu pekee! Haya mambo ya kujiunga na chama chenye mrengo wa kidini ili kupata upendeleo fulani itawahangaisha mpaka kaburini, madai yenu hayataisha milele hata mkipewa vyuo 20 vya TANESCO kuvigeuza kuwa vyuo vikuu vya kiislamu!
CUF kwa kuwa ni chama cha waislamu... Full stop
Zitto na Arfi si wajinga kama wewe Zubeda? Sijawahi kusoma sread yako ikani-impess hivi una elimu gani? Nina wasiwasi sana nawe Zubeda
Asalam Aleikum waungwana. Leo mimi kama mtanzania mwenye uchungu na watanzania wa dini zote naomba kuchukua nafasi hii kuwashauri ndugu zangu waislamu. ACHANENI NA CCM INAWALOSTISHA. SAbabu ni nyingi ila nawapa hizi chache hapa chini:
CCM imewadanganya kuwa itawapa mahakama ya kadhi na kuiingiza Tanzania kwenye jumuiya ya kiislamu (OIC). Cha kusikitisha ni kwamba hadi leo hii hakuna hata dalili ya debates juu ya swala hilo. Kama wangeona ni muhimu kufanya hayo wangeshafanya. Kama mnabisha angalia walivyolikubali kwa haraka swala la kuilipa DOWANS. Yani hilo swala lilikuwa muhimu mpaka uamuzi wake haukuitaji kikao cha baraza la mawaziri. KWA TAHARIFA TU, priority ya CCM kwa sasa ni kuimaliza CHADEMA. Hilo la mahakama ya kadhi na OIC ni changa la macho.
Pili, CCM inauzalilisha uislamu kwa kuwachaguliwa kionozi wao wa dini. Amini usiamini, ni dini ya kiislamu tu inachaguliwa kiongozi wake (mufti) na CCM kwa kupandikizwa na Usalama wa Taifa (TISS). YAni hata dini ndogondogo Tanzania zipo huru na mkono wa CCM lakini dini kubwa kama uislamu kuchaguliwa wa kuwaongoza ni dharahu zinazopaswa kupingwa waziwazi.
Tatu na mwisho kwa leo, wale walioko CCM wanaojiita waislamu na kuwashawishi si waislamu wa kweli. Niliwahi kuwaeleza kuhusu paper iliyokuwa presented hapa Cambridge University na authority wa dini ya kiislamu (jina kapuni). Yeye alisema hivi, kuna tofauti kubwa kati ya moslem (kama hawa waliopo CCM) na islamists (waislamu wa kweli). Moslem wapo kwa faida ya matumbo yao na wala si kumcha Mungu. Ndio maana Makamba ni moslem, Rostam ni moslem, Kikwete na DOWANS yake no moslems ndio maana hawaogopi Mungu wanaila Tanzania mchanamchana. Mpaka uwe islamist ndio unakuwa musilamu kwelikweli. Sasa nyie ndugu zangu kwanini mnakubali kuendeshwa na Moslems badala ya Islamists? IKATAENI CCM tuijenge nchi mpya kama EGYPT walivyoamua kuondokana na Moslem wao MUBARAK!!!
Kwanza naomba nikuulize umeishia darasa la ngapi mzee maana uandishi huu unatisha kama sio kusikitisha.
Pili maneno unayoyasema yana ukweli ndani yake (hasa katika kutofautisha baina ya muislam na waislam) lakini hayana mshiko. Kwanza kabisa elewa watanzania ni jamii inayotokana na mchanganyiko wa waislamu, wakristo, wapagani na wengineo. Sasa ukishalifahamu hilo kisha twende katika nini siasa. Siasa ni mitazamo yenye kusaidia kuendeleza taifa (au kwa jina jengine ni ideology). Sasa unapowashauri waislamu waikatae CCM je unamaana hao waislamu wote watakuwa na the same political ideology? Jibu hapana kwani kila mmoja ana mtazamo wake.
Tatu umezungumzia hoja ya OIC na Mahakama ya Kadhi nani kakuambia haifanyiwi kazi? Au ndio umetumwa uje kutuambia ili tuvunjike moyo ulizia humo ndani utafahamu kitu gani kinaendelea. Hivi vitu serikali ya Tanzania haina hoja ya msingi ya kuvikataa kwani vinaviolate the basic principles za the so called secular state. Wakizikataa tuaenda mahakamani kudai huko tutajua kama serikali hii ni ya nani kwani kuna vitu bila ya kivisimimamia kidete havitakaa vieleweke. Hivyo basi usifikiri hiyo Hoja imekufa au haishughulikiwi kaa usubiri uone ndio useme.
Mwisho umesema kama haitatekelezwa tukihame Chama Cha Mapinduzi swali je waislamu waende wapi wakihama chama cha mapinduzi? Ndio utakuta hii nchi inakoelekea ni kuparaganyika kama sio kupotea katika ramani. Unajua cheza na watu na makabila yao ila usicheze na watu na imani zao. Mahakama ya kadhi ni sehemu ya maisha ya mtanzania anayeabudu dini ya kiislamu hivyo basi kumnyima mahakama ya kadhi ni kumnyima nafasi ya kufanya ibada yake. Vilevile kumnyima mahakama ya kadhi ni kumnyima haki ya kisheria ambalo ni jukumu ya mahakama ya nchi kutoa huduma hiyo. Hivyo kama waislamu wanavyowavumilia sheria zenu za kianglikana na kikatoliki katika mahakama za sasa na sie tuvumilieni na mahakama ya kadhi tutaenda vizuri vyenginevyo mnatafuta ushari.
Mohamed Shossi said:Kwanini CUF wapeni sababu
Haaaa unachekesha kaka mlisha onyesha tangu mwanzo kuwa chadema ni chama cha kanisa ndio maana mlimsimamisha mchungaji agombee.mmekosa ndio mnarudi kutafuta wanachama wa kiislam,tutajiunga baada ya slaa kuoa maa takrab zinaaaaaaaaa