Nasema maandamano yangefanyika yangekuwa yanaidhalilisha sana dini ya kiislam,viongozi wake,waumini wake,kitabu chake[Quran] na Mtume wake Muhamad SAW kwasababu zifuatazo.
[1] Waislamu wanataka kuandamana kwasababu serekali ya CCM imeshindwa kuanzisha mahakama ya Kadhi.Ukweli ni kwamba Serekali ya CCM imewaruhusu waislam waanzishe na kuiendesha mahakama ya kadhi wenyewe kwasababu ni sehemu ya ibada yao [waislamu].Ni ajabu kubwa kuona wanazuoni tena waliobobea kuendelea kudai mahakama ya kadhi ilihali serekali imesharidhia kuanzishwa kwake.
[2] Waislamu wa Tanzania wanajua wazi CCM imekuwa ikiwadanganya wananchi kwa muda mrefu katika mambo mabali mbali,inashangaza sana kusikia viongozi wa waislam hawakuona haja ya kuandamana wakati mabilioni ya EPA,Meremeta,ununuzi wa radar,ndege ya rais,mikataba ya madini na ufujaji wa fedha kwenye maidara ya serekali ukifanyika.Akili yangu inakataa kuamini kwamba viongozi wa waislamu leo hii wanagundua CCM ni waongo kwasababu tu wameshindwa kuvunja katiba ya JMT kwa kuingiza mahakama ya kadhi.Viongozi wa aiana hii kamwe hawataweza kuwakomboa waislam kwasababu wanashindwa kuwaeleza ukweli waumini wao kwamba mahakama ya kadhi inaweza kuanzishwa na waislamu wenyewe bila kutegemea fadhila za serekali.
then mukawa victorious kwa kitu gani? hivi ninyi nani aliwapandikiza ujinga kiasi hiki? we maandamano ya Yesu si Mungu mlipewa haki na nani ili kuonekana kuwa mmefanikiwa, sikujua kuwa wewe MS akili yako ni shake well kiasi kikubwa namna hiyombona unajidanganya. Mbona yale ya yesu sio mungu talifanikiwa
You are totally wrong! Hakuna uhuru usiokuwa na mipaka ndugu, hata kama utaubandika jina la demokrasia, uhuru wako unapoishia ndipo na wa mwenzako unapoanzia! Hawa watu wameambiwa waanzishe Mahakama yao wenyewe, bado wamekaa vijiweni kunywa kahawa wakisubiri Serikali iwaanzishie IBADA yao ya KIISLAMU! Upstairs kwa hawa wandugu kunafanya kazi kweli?
Mkuu Buch nilichokuwa namaanisha mimi sio uhalali wa kuanzisha mahakama yao ya kadhi bali ni uhuru wa kuandamana.
Wangeachwa waandamani ili mradi wasivunje sheria.
kuwazuia kuandamana ni kama kuwahofia hasa ukizingatia wanaandamana kwa sababu ya kuhamasisha wananchi wasiichague tena CCM.
Maandamano ya wanafunzi wa chuo kikuu huwa ni productive. Maana huko haki huwa haipatikani bila maandamano.So far katika nchi hii hakuna maandamano ambayo yamekuwa na productivity!...Wastage of time at the peak tune!
Sasa hapo sio kuingia tena kwenye siasa ndugu? Na msingi wa maandamano hayo ni upi hasa ukizingatia kwamba Mahakama za Kadhi zimeruhusiwa kuanzishwa na waislamu na kuendeshwa na waislamu wenyewe kwa gharama zao?
hahahaha, mzee chadema wakipewa nchi. Nadhani sijui dini nyengine wakae wapi?
Nitake radhi Mkuu,
hahahaha, mzee chadema wakipewa nchi. Nadhani sijui dini nyengine wakae wapi?
Unajua kuna makubaliano ambayo CCM ilikubaliana (kipindi kile cha harakati za Jk kuingia madarakani) na waislamu juu ya kuanzishwa kwa hii mahakama.
Ninavyoona mimi kuandamana kwa amani kahuna tatizo ni haki ya wananchi.
Serikali inaogopa nini? au inahofu wananchi watahamasika na kutoichagua CCM?
Swala sio udini, ni demokrasia.
Hebu tuangalie kwa ufupi Sheria ya Mahakama ya Kadhi Zanzibar (The Kadhi's Court Act, 1985, No. 3 of 1985) inasemaje. Kumbuka kuwa suala la Mahakama (isipokuwa Mahakama ya Rufani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania), si la Muungano, kwa hivyo isidhaniwe kwamba Katiba ya JMT inalihusu!
Section 4 (1). "There shall be a Chief Kadhi who shall be appointed by the President. (2) The Chief Kadhi shall not enter upon the duties of his office until he has taken and subscribed the oath of allegiance...as may be prescribed by the House of Representatives. (3) A person shall be qualified to be appointed to hold or to act in the Office of Chief Kadhi if, and shall not be so qualified unless- (a) he professes and follows the Muslim religion; (b) he possess such knowledge of the Muslim law which in the opinion of the President is qualified to be appointed as such."
Kama Mahakama za Kadhi ndio zinatakiwa Rais awe anamteua CHIEF KADHI na pia maoni yake kuhitajika KWENYE MAMBO YA KIDINI, sasa hiyo nchi sio ya Kiislamu? Anyway, kwa Zanzibar, Waislamu ni wengi, lakini Wakristo nako wapo, Je, akishika madaraka Mkrito atamteua Kadhi? Very confusing indeed!
Hivi Mahakama hiyo ikianzishwa na kuendeshwa na waislamu wenyewe bila kuingiliwa na Serikali inakuwa SIO MAHAKAMA YA KADHI? Mbona imeng'ang'aniwa kwamba Serikali iliahidi, Serikali iliahidi, Serikali iliahidi..........Serikali iliahidi! Ni kweli iliahidi kulitafutia UFUMBUZI suala la uanzishwaji wa Mahakama ya Kadhi! Serikali HAIKUTOA ahadi kwamba "Itaanzisha na kugharamia Mahakama za Kadhi!" Mbona mambo rahisi yanataka kufanywa kuwa magumu kama chuma cha pua