Elias Msuya
Senior Member
- Dec 23, 2011
- 173
- 671
Wanaharakati wanaojitambulisha Raia ni Sisi, Kumbusho Kagine na Bubelwa Kaiza wamefungua kesi namba 12670/2025 kupitia mtandao dhidi ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) na Mwanasheria Mkuu wa Serikali wakiiomba Mahakama itoe amri ya kurekebisha upungufu uliomo kwenye Kanuzi za Maadili ya Uchaguzi.
Taarifa kutoka kwa Raia ni Sisi wanaowakilishwa na mawakili wasomi Mpoki Bukuku na Jebra Kambole imesema kesi imetajwa leo Jumatano, Juni 25, 2025 mbele ya Jaji Kagomba, Mahakama Kuu Dodoma.
Taarifa Zaidi zinadai kuwa Serikali imeweka pingamizi dhidi ya umahiri wa kiapo.
“Jaji Kagomba amepanga kusikiliza na kutolea uamuzi pingamizi la wajibu maombi siku ya Alhamisi Julai 3, kisha, iwapo ataona pingamizi halina mashiko, kuendelea kusikiliza shauri hilo. Shauri litasikilizwa Mahakama ya Wazi, [Mahakama Kuu] Jijini Dodoma,” imesema taarifa ya Raia ni Sisi.