Waingereza wafuatilia utendaji wa JK | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waingereza wafuatilia utendaji wa JK

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Rutashubanyuma, Mar 28, 2011.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Mar 28, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,208
  Likes Received: 414,316
  Trophy Points: 280
  Waingereza wafuatilia utendaji wa JK Send to a friend Sunday, 27 March 2011 05:46

  Claud Mshana
  RAIS Jakaya Kikwete atalazimika kupunguza safari zake nje ya nchi na kutumia muda mwingi kushughulikia masuala ya ndani ya nchi ikiwa anataka kumaliza vizuri katika kipindi chake cha mwisho cha utawala wake Taasisi ya Utafiti wa masuala ya uchumi ya Uingereza, Economic Intelligence Unit(EIU), imeeleza.

  Taarifa ya EIU imesema kuwa Rais Jakaya Kikwete yupo njia panda kutoa kipaumbele cha kufanya mageuzi ndani ya chama anachokiongoza (CCM), au kutumia muda wake kutekeleza ilani ya chama hicho, huku akikabiliwa na changamoto iliyoitaja kuwa kubwa ni kuimarisha CCM na kutekeleza ahadi zake kwa wananchi.

  Kwa mujibu wa taarifa hiyo EIU iliyochapishwa Februari mwaka huu, Rais Kikwete anapaswa kutumia muda wake mwingi kushughulikia masuala mbalimbali yanayoendelea ndani ya nchi ikiwa pamoja na mpasuko ndani ya CCM, utekelezaji wa ahadi alizotoa na kusimamia mageuzi ya kiuchumi nchini.

  “Katika kipindi cha kwanza cha utawala wa Kikwete, kulikuwa na ukosoaji mkubwa dhidi ya safari zake nje ya nchi. Watu waliamini kuwa hatumii muda mwingi kushughulikia matatizo yaliyopo nchini kwake. Sasa tunatarajia kuwa atapunguza safari za nje katika awamu yake ya mwisho ya uongozi,” inasema taarifa hiyo.

  Taarifa hiyo kuwa EIU inaeleza kuwa Tanzania imekuwa ikikabiliwa na matatizo mbalimbali ikiwamo kupanda kwa bei za vyakula, bidhaa na huduma mbalimbali, ukosefu wa ajira, madai ya mishahara, mgawo wa umeme, mikopo ya vyuo vya elimu ya juu na vitendo vya ufisadi vilivyoligharimu taifa mabilioni ya fedha za walipa kodi na kwamba yote hayo yamedumu kwa muda mrefu.

  EIU imetoa taarifa yake ndani ya miezi minne ya kwanza ya awamu ya pili ya utawala wake aliouanza mwishoni mwa mwaka 2010 baada ya kuchaguliwa Oktoba 31 katika Uchaguzi Mkuu, Rais Kikwete.

  Katika kipindi cha kwanza cha utawala wake, Kikwete pia alikuwa na safari nyingi nje ya nchi, nazo zilizolalamikiwa kuwa hazina tija kwa maendeleo ya nchi.

  Kwa mujibu wa vyombo mbalimbali vya habari nchini, Rais Kikwete alianza safari za nje Desemba 14 mwaka jana, mmoja tu baada ya kutangazwa kuwa mshindi wa kiti cha urais kufuatia Uchaguzu Mkuu uliofanyika Oktoba 31, 2010, ambapo alikwenda Zambia kwenye mkutano wa nchi wanachama wa maziwa makuu.

  Rais Kikwete alisafiri tena Januari 26, kwenda Uswis na Ethiopia na mwezi mmoja baadae alisafiri kwenda kuhudhuria mikutano ya kimataifa ambapo kati ya Februari 20 hadi 24 alikuwa nchini Mauritania.

  Machi Mosi alikwenda nchini Ufaransa kutoa mada kwenye mkutano wa kimataifa na alikwenda nchini, Mauritania kuhudhuria mkutano wa kutafuta suluhisho la migogoro ya kisiasa iliyoikumba nchi ya Ivory Coast.

  “Malengo makubwa kwake (Rais Kikwete) katika kipindi chake cha mwisho madarakani ni kujitoa ndani ya uzio wa kufurahisha watu ili kuendelea kuungwa mkono, au anaweza kuongeza juhudi zake katika kufanya mageuzi ndani ya chama. Hata hivyo, anapaswa kufanya maamuzi juu ya muda na nguvu anazotaka kutumia katika kushughulikia migogoro ndani ya chama na muda kiasi gani atahitaji katika masuala ya kitaifa.” Inasema sehemu ya taarifa hiyo.

  Hivi karibuni, Rais Kikwete alitangaza kufanya mabadiliko makubwa ndani ya CCM, mabadiliko ambayo kwa kiasi kikubwa yametokana na ushindi mdogo ilioupata wakati wa Uchaguzi Mkuu uliopita.

  Lakini, EIU inasema kuongezeka umaarufu wa Chadema ni changamoto kubwa kwa Serikali ya CCM na wakati huo Chadema itakuwa na changamoto ya kujipanga vizuri na kuunda umoja ili kufanikisha malengo yake ili kukabiliana na CCM ambacho bado ni kizuri kina nguvu na ushawishi wa kisiasa nchini.

  “Jambo lingine la muhimu katika siasa za ndani, ni jinsi Chadema itakavyoweza kuendana na mazingira ya kuwa chama kikuu cha upinzani na inapaswa kukubaliana na ukweli kuwa CCM ni wazuri wa kutumia baadhi ya mawazo ya upinzani na kuyafanya yao,” inasema taarifa hiyo ya EIU na kuongeza:

  “Hili limeweza kuthibitishwa baada ya Uchaguzi Mkuu ambapo Chadema ilianza kudai katiba mpya, wazo ambalo Rais Kikwete amelichukua na hivi sasa yuko mbioni kuunda Kamati ya Kupitia Mabadiliko ya Katiba.”

  Kuhusu kesi inayowakabili viongozi wa Chadema baada ya kutokea vurugu za Arusha, zilizosababisha vifo vya watu wanakadiriwa kufkia watano, EIU inasema kuwa upo uwezekano kwa kesi hiyo kutupiliwa mbali kwa kile kinachoonekana kuwa kuendelea kwake kunaweza kuzuia machafuko zaidi nchini.

  “Kama kesi hiyo itaendelea, kuna uwezekano wa kuibua machafuko mapya, hivyo kuna uwezekano mkubwa wa kesi hiyo kutupiliwa mbali kimya kimya kukwepa hatari hiyo,” inadai taarifa EIU.

  Ushirikiano wa Afrika Mashariki

  Ripoti hiyo imedai kuwa Tanzania inakwenda mwendo mdogo katika kufikia malengo ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), ikihofia ardhi yake kumilikiwa na wahamiaji kutoka nchi nyingine wanachama wa Jumuiya hiyo hasa Kenya na Uganda.

  Hata hivyo, EIU ilisema kuwa nchi wanachama wa EAC hazina dhamira ya dhati kuingia katika matumizi ya sarafu moja, licha ya makubaliano yaliyofikiwa baina ya nchi hizo na Benki Kuu ya Jumuiya ya Ulaya (ECB).

  “Tunaona kuwa hakuna matumaini yeyote ya kuanza kutumia sarafu moja katika muda uliopangwa wa 2012. Tunaona hiki ni ni kikwazo kwa nchi wanachama kuendelea na ratiba iliyopangwa, wakati nchi zote hazina dhamira ya kweli ya kufanya hivyo,” inadai taarifa hiyo.

  Taarifa hiyo ya EIU inasema, licha ya kutokuwepo usawa wa kiuchumi miongoni mwa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, kuanza matumizi ya sarafu moja hakuna dhamira halisi ya kisiasa kama inavyodhaniwa na wengi.

  Mwananchi Jumapili lilipowasiliana na Waziri wa Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samweli Sitta, jana aliomba atafutwe kesho kwa sababu alikuwa kwennye mkutano muhimu.


  Comments

  12  0 #18 Mahamed 2011-03-28 10:38 Waafrika kuburuzwa kunakaribia hatmaYake sababu hata kifopu anapokaribia shimo atakaidi kuingia mpaka asukumiwe kwa nguvu. Bahati nzuri Waafrika werevu wameshaamka, hivyo hakuna atakae kutuumiza bila yeye pia kudhurika.
  Na vibaraka wao pia watashughilikiw a na w-a-t-a-k-o-s-a maisha hata yale ya mbwa zao sababu ulaya pia wanaangamia kiuchumi.
  Maadui wetu hawataki kuona mikakati ya kimaendeleo, na wanaogopa sana watu wanao safiri sababu kuna elimu ya dhati katika kusafiri-kama tu msafiri anajua anachokifanya. Kuzimiazimia kwa Rais Kikwete kunatufundisha kua anaumia kwa ajili ya taifa letu. Sababu safari za starehe hazimuumizi mtu kwa uchovu. HANDS OFF OUR COUNTRY PLEASE.
  Quote
  Quote

  0 #17 Mahamed 2011-03-28 10:36 Waafrika kuburuzwa kunakaribia hatmaYake sababu hata kifopu anapokaribia shimo atakaidi kuingia mpaka asukumiwe kwa nguvu. Bahati nzuri Waafrika werevu wameshaamka, hivyo hakuna atakae kutuumiza bila yeye pia kudhurika.
  Na vibaraka wao pia watashughilikiw a na wa[NENO BAYA]sa maisha hata yale ya mbwa zao sababu ulaya pia wanaangamia kiuchumi.
  Maadui wetu hawataki kuona mikakati ya kimaendeleo, na wanaogopa sana watu wanao safiri sababu kuna elimu ya dhati katika kusafiri-kama tu msafiri anajua anachokifanya. Kuzimiazimia kwa Rais Kikwete kunatufundisha kua anaumia kwa ajili ya taifa letu. Sababu safari za starehe hazimuumizi mtu kwa uchovu. HANDS OFF OUR COUNTRY PLEASE.
  Quote
  Quote

  0 #16 Mahamed 2011-03-28 10:35 wahusika wa habari tunadai uhuru wa press. Hakuna neno baya nililo andika, kwanini nabambikwa. Article ilioandikwa katika makala hii inaashiria negative propaganda dhidi ya taifa letu.
  Quote

  0 #15 Mahamed 2011-03-28 10:30 wa[NENO BAYA]sa
  Quote

  0 #14 Mahamed 2011-03-28 10:29 (wa[NENO BAYA]sa)
  Quote

  0 #13 Mahamed 2011-03-28 10:28 Na vibaraka wao pia watashughilikiw a na (wa[NENO BAYA]sa) maisha hata yale ya mbwa zao sababu ulaya pia wanaangamia kiuchumi.
  Quote

  0 #12 Mahamed 2011-03-28 10:23 Waafrika kuburuzwa kunakaribia hatmaYake sababu hata kifopu anapokaribia shimo atakaidi kuingia mpaka asukumiwe kwa nguvu. Bahati nzuri Waafrika werevu wameshaamka, hivyo hakuna atakae kutuumiza bila yeye pia kudhurika.
  Na vibaraka wao pia watashughilikiw a na wa[NENO BAYA]sa maisha hata yale ya mbwa zao sababu ulaya pia wanaangamia kiuchumi.
  Maadui wetu hawataki kuona mikakati ya kimaendeleo, na wanaogopa sana watu wanao safiri sababu kuna elimu ya dhati katika kusafiri-kama tu msafiri anajua anachokifanya. Kuzimiazimia kwa Rais Kikwete kunatufundisha kua anaumia kwa ajili ya taifa letu. Sababu safari za starehe hazimuumizi mtu kwa uchovu. HANDS OFF OUR COUNTRY PLEASE.
  Quote

  0 #11 Source 2011-03-28 09:32 Kweli watanzania bado tuko gizani. Mchana kweupee watu wanahitaji tochi? Hata jirani anapotumulikia bado tunaona giza na kumlaumu? Mh!? Kweli mbuzi yake kamba. Tunawezaje kuthubutu kumtetea kwa nguvu zote m2 anayetunyonya na kumlaumu anayefichua unyonyaji huo?
  Quote

  0 #10 Macknon 2011-03-28 08:41 SANGA,MBILIGI nendeni darasani. Huyo MASAWE nina wasiwasi kuwa siyo mchaga maana hakuna mchaga M[NENO BAYA] namna hiyo. kimsingi hakuna hoja ya kuwajibu maana mmechanganyikiw a na ku[NENO BAYA]ka.
  Quote

  0 #9 Massawe 2011-03-28 00:33 Hivi nyinyi Mwananchi mmepatwa na wazimu nini? Kikwete aliwafanya nini mpaka mnamuingilia kiasi hicho. Uchafu mnauchapisha utatusaidia nini watanzania? Hao waingereza hawaitakii mema nchi yetu. Wanatafuta sehemu ya kuuza silaha zao. Machafuko yakitokea nchi zetu hawa watengeneza silaha nchi tajiri wananufaika. Inaelekea wanaosema chadema inafadhiliwa na waingereza ni kweli, kwa sababu hizi ndizo topic za chadema chama kinachotaka kujenga umaarufu kwa kuvuruga nchi.
  Quote

  +1 #8 robin 2011-03-27 23:45 Watu wote mnao comment kuilaani taarifa hiyo mnafikiri serikali inaendeshwaje? Muulizeni Mkulo awaambie ukweli kuhusu serikali kuendeshwa kwa pesa za wahisani, ambazo ni za walipa kodi wao huko, sasa wakihoji ama kushauri ni kosa? Ukimpa mwanao ada ya shule akaendea disco utashangilia?
  Quote

  +3 #7 Mhifadhi 2011-03-27 18:57 La ukweli wamelisema sasa mtanzania akikerwa amesemewa mambo yake ni yule ambaye anufurahia umasikini na anapenda vizazi vijavyo viwe masikini. Ukweli tukiacha ushabiki ni kuwa serikali hii inatuangusha kila kukicha. Hapa wamepewa ushauri na ni vyema wakaufanyia kazi wakapembua chuya na mchele
  Quote

  -3 #6 elibariki yerald 2011-03-27 16:57 Quoting SANGA:
  Napata wasiwasi kama habari zinazoandikwa zinapi[NENO BAYA] kwa kina na wahariri kabla ya ku-publish maana hii sasa ni aibu. Habari ya ki[NENO BAYA] kama hii ndi mambo ambayo mtanzania wa leo anahitaji kusikia au kusoma? Nahisi "mwananchi" sasa mnasukumwa na mawazo hasi kwa serikali na ushabiki wa CHADEMA kupita kiasi ndio maana mnakosa hata muda wa kupitia na kuhariri kwa umakini habari zenu kabla ya kuzichapisha.
  Maoni ya EIU yanatuhusu nini watanzania,rais Kikwete hajachaguliwa na EIU,kachaguliwa na wananchi,labda wazungumzie Chadema inayofadhiliwa na chama kimoja huko Uingereza,na hela walizokopeshwa watazirudishaje ,wasituletee [NENO BAYA][NENO BAYA] zao kwenye nchi yetu.Eti wanazungumzia safari za Kikwete nje ya nchi,wazungumzi e na kampeni chafu,ubaguzi na za uchochezi na kuleta machafuko ya kivita zinazofanywa na Chadema.​


  mbombo pojili nkhojo jhowishwa nu kikwete jibuba vhoni.jhovishwa nu kiwete jhako.lekhake uvuniasi ..kiwete ibuda vatanzania ..
  Quote

  +1 #5 nkyandwale 2011-03-27 13:50 kama unataka kumtawala mtu kiuchumi, mtambue uwezo wake wa kufikiri, mambo yako yatakuwa barabra! Utakuwa umeshika injini na sio usukani kama wanavyodhani.
  Quote

  +2 #4 franco 2011-03-27 12:23 [NENO BAYA] ndio wali wao,hawa wenzetu wanatupa misaada ya bajeti,tujue kwamba hawa wenzetu wanajua siri za nchi yetu kuliko wewe wananchi mlala hoi,ndio maana unaona wanampiga gadafi mpaka chumbani kwake.SAFARI ZA RAIS WETU NI UFUJAJI WA PESA ZA WANANCHI SIO ZA RAIS AU ZA CCM NI ZA WANANCHI LEO HII MUULIZE RAIS WAKO SAFARI MOJA AU ZIARA YA UFARANSA RAIS NA VIONGOZI WENGINE WALITUMIA SHLINGI NGAPI WEWE UNAWEZA KULIA LABDA NI BAJETI YA WIKI KATIKA HOSPITALI YA MUHIMBILI,SASA WANATOA MSAADA WANAJUA KULIKO WEWE MLALA HOI
  Quote  12
  Refresh comments list
   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Mar 28, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,208
  Likes Received: 414,316
  Trophy Points: 280
  PHP:
  Taarifa hiyo kuwa EIU inaeleza kuwa  Tanzania imekuwa ikikabiliwa na  matatizo mbalimbali ikiwamo kupanda kwa  bei za vyakulabidhaa na  huduma mbalimbaliukosefu wa ajiramadai ya  mishaharamgawo wa  umememikopo ya vyuo vya elimu ya juu na vitendo  vya ufisadi  vilivyoligharimu taifa mabilioni ya fedha za walipa kodi na  kwamba yote  hayo yamedumu kwa muda mrefu.
  Hizi kero na nyinginezo JK alizikuta na ataziacha tu.......................kaa wale waliomtangulia....ila mafao yake binafsi hayo atayafanikisha tu.........................................ila siyo ya kitaifa.......................
   
 3. P

  PauliMasao JF-Expert Member

  #3
  Mar 28, 2011
  Joined: Nov 26, 2007
  Messages: 286
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Hakuna jipya hapa
   
Loading...