ameline
JF-Expert Member
- Jan 8, 2013
- 2,292
- 1,152
[h=3]UPEKEE WA NDEGE NJIWA[/h]
1.Njiwa hutaga mayai mawili tu
2.Njiwa ndio viumbe pekee duniani wenye mpenzi mmoja,yaani huyo mmoja akipotea au kufa anaebakia hawezi kuwa na mpenzi mwingine.Hata yule anaebaki huendelea kuombolea kifo cha mpenzi wake.
3.Njiwa dume na jike wote huwa na jukumu la kuwalisha watoto kwa pamoja.
4.Hata ukimfuga njiwa akiruka umbali gani hasahau nyumbani lazima arudi.Ndio maana toka zama hizo njiwa walikuwa wakitumika kutuma na kurudisha ujumbe fulani.
5.Binadamu huwala njiwa kama mboga hivi,kumbanika,kumchoma n.k
6.Njiwa hutumika kama alama ya amani,upendo,matumaini na mshikamano.
7.Ni ndege wasiopenda fujo ukiwafuga kama ni nyumba iliyojaa ugomvi virugu wanahama wanaondoka.