Waijua siri ya njiwa???

Waijua siri ya njiwa???

hakuna ndege ambao ni wachache kama njiwa, na ni kweli kwa wale tuliowahi kuwa na wadogo zetu wanaofuga njiwa kama ukileta njiwa dume 1 na majike 2 basi ujue huyo jike mwingine hatataga kamwe., maana njiwa hushikana wawili tu, hata huyo jike uliyemuweka na dume na akataga ukasema labda umuhamishie yule jike mwingine usisubiri kuwa atataga, ataambulia kudonolewa tu,.

mmmmh ! Dada ! wenzio utoto wote tumefuga njiwa, ukweli ni kuwa ukichukua jike moja madume mawili, yule dume mdogo atanyang'anywa, na yule njiwa mkubwa ndiye atakae chukuwa jike.
Ila maajabu yao, wakitaga tu mayai mawili, yai moja wanaliviza, na moja linatoa jike jingine, hivyo pea inatimia.
 
Duh hili la mpenzi mmoja nina mashaka nalo.., ingekuwa kweli basi hawa njiwa wangekuwa wachache sana.., Na wanachagua huyo mpenzi wakati gani / umri gani na ni vipi anakubalika kwamba huyu ni wangu ?

kuhusu idadi mkuu, njiwa ni mojawapo ya ndege wachache sana duniani na kuhusu kuchagua mpenzi hayo mambo tumuachie muumbaji ndo anajua siri hiyo kwani vitu vingine hutokea automatic hata wanasayansi hawana jibu. je nikikuambia pia kuwa ndege hupanga uzazi na wana njia mbalimbali za kupanga uzazi kama binadamu wafanyavyo utaamini?
 
Research yako umefanyia wapi, njiwa hana mpenzi mmoja tu kama unavyo dai.

si research tu bali ni uhalisia, we nenda kwa wafuga njiwa waulize, basi kama umefanya research ya kuthibitisha mpenzi zaidi ya mmoja wa njiwa tuletee, au kama ulishaona njiwa wakiwa 3 naomba walao picha
 
kuhusu idadi mkuu, njiwa ni mojawapo ya ndege wachache sana duniani na kuhusu kuchagua mpenzi hayo mambo tumuachie muumbaji ndo anajua siri hiyo kwani vitu vingine hutokea automatic hata wanasayansi hawana jibu. je nikikuambia pia kuwa ndege hupanga uzazi na wana njia mbalimbali za kupanga uzazi kama binadamu wafanyavyo utaamini?

mambo mengine watu wanaongezea chumvi ila hawa ndege husikia na wana hisia !
 
si research tu bali ni uhalisia, we nenda kwa wafuga njiwa waulize, basi kama umefanya research ya kuthibitisha mpenzi zaidi ya mmoja wa njiwa tuletee, au kama ulishaona njiwa wakiwa 3 naomba walao picha

wanakuwa watatu bana, ila kama ni dume mdogo atapigwa na kunyang'anywa. Ndege ambao sijawaona kuwa watatu ni wale kasuku wa Dodoma wenye kijani na njano na midomo mwekundu !
 
hapana bana si njiwa labda mwewe hao., maana hata wale njiwa pori tu hata kiota chao hawajengi kwenye mti ambao tayari wengine wamejenga, yaani huwa pekee 2 tu.
 
mambo mengine watu wanaongezea chumvi ila hawa ndege husikia na wana hisia !

hapana chumvi wala sukari ukiyashangaa ya musa..... na ukijaribu kutafakari au kufuatilia mambo meengi hasa viumbe vya huku duniani utashangaa... unaweza kugoogle pia for more info
 
mmmmh ! Dada ! wenzio utoto wote tumefuga njiwa, ukweli ni kuwa ukichukua jike moja madume mawili, yule dume mdogo atanyang'anywa, na yule njiwa mkubwa ndiye atakae chukuwa jike.
Ila maajabu yao, wakitaga tu mayai mawili, yai moja wanaliviza, na moja linatoa jike jingine, hivyo pea inatimia.

haya baba hongera kwa kufuga njiwa
 
ukisemaaa kwa ukaliiiii, mambo utayaharibuuuu

hali yangu mahamumuuu ooooh maradhi yamenisibuuuu,
usiku kucha nakeshaaa oooh na yeye ndio sababuuu
pendo langu halijeshaaa, oooh ndilo ninalihabibuuuu......lol
 
si research tu bali ni uhalisia, we nenda kwa wafuga njiwa waulize, basi kama umefanya research ya kuthibitisha mpenzi zaidi ya mmoja wa njiwa tuletee, au kama ulishaona njiwa wakiwa 3 naomba walao picha
FYI mimi nilikuwa na fuga njiwa, na mara nyingi sana nilikuwa nikinunua njiwa mmoja mmoja pale na umri wa miaka saba mpaa 10, lakini nikileta njiwa wa kike naona madume wa njiwa wanamuania njiwa wakike, wengine mpaa walikuwa wakigombana sa unataka kunifundisha nini hapo.

We kama unataka kuamini nacho sema chukua njiwa wakike mpeleke kwa wale wanao funga njiwa, uone kama hapandwi na yale madume na atamasahau yule dume aliye kuwa akimpanda kule atokako, na mambo yanakuwa kama kawaida.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom