Waiba Tsh Bilioni 27.9 katika zaidi ya ATM 1,400 ndani ya masaa 3!

RASHEEDMTOI

Member
Apr 13, 2015
85
68
Majambazi wa kiteknolojia nchini Japani waiba zaidi ya Yuan bilioni 1.4 sawa sawa na Tsh Bilioni 27.9 (Ksh Bilioni 1.29) kupitia ATM 1,400 katika miji kadhaa nchini humo ndani ya masaa 3.

Wizi huo ulifanyika kwenye ATM kwa kutumia kadi za kibenki na imetambulika kadi hizo za ATM zilihusisha akaunti za benki ya nchini Afrika Kusini.

Hakuna wizi uliohusisha akaunti ya benki ya nchini Japan, waliiba taarifa za kibenki za wateja wa nchini Afrika kusini – wa benki ya Afrika Kusini.

ATM zilizotumika kutoa pesa zilikuwa za miji ya Tokyo, Kanagawa, Aichi, Osaka, Fukuoka, Nagasaki, Hyogo,Chiba, Nigata na mingine zaidi.

Inasemekana wizi huu ulihusisha kundi kubwa la watu na hivyo kuonesha kulikuwa na mipango mikubwa kuanzia kuiba taarifa za data za kibenki kupitia mtandao na kisha kutumia data hizo kutengenezea kadi zilizotumika kwa wizi huo.

Kwa sasa polisi wa nchini Japani wamesema wanajitahidi kupitia video kutoka kwenye kamera za kwenye ATM za miji hiyo ili kuweza kubaini watu waliohusika ila kwa kuwa inaonekana ilihusisha ATM nyingi na watu wengi basi itachukua muda sana.

Pia wanashirikiana tayari na polisi wa nchini Afrika kusini kwa karibu kupitia shirika la Interpol ili kuweza kufahamu ni kwa jinsi gani taarifa za kibenki za wateja ziliweza kuchotwa kutoka kutoka nchini humo.

Kwa sasa tayari mabenki kadhaa yashaathirika na masuala ya udukuzi wa data – hii ni pamoja na Qatar National Bank, Bangladesh Central Bank na ata shirika la Fedha la nchini Marekani, US Federal Reserve. Katika sehemu hizi nyingine umoja wa udukuzi wa kimtandao kupitia kundi la Anonymous limehusika zaidi.

Source TEKNOKONA
 
Hao anonymous wanajiamini sana, huwa wajua sana sheria za nchi husika na kupata ushahidi wa kuwafunga ni ngumu sana. Wanaweza kutega button ya kuswitch off computer kwenye kitasa cha mlango.
 
Yuan na Japan wapi na wapi???????

ila kuweka limit ya perday ni jambo zuri sana, manake mtu hawezi kukuibia 10M bila kushtuka
 
Back
Top Bottom