Wahusika wakuu wa Bayport

Wahusika wakuu wa Bayport

Nas Mapesa

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2014
Posts
5,286
Reaction score
5,423
Salaam,

Nachukua nafasi hii kutoa malalamiko juu ya shughuli za Bayport wilaya ya Kahama.

Kuna utaratibu unatumika wa kuendelea na makato kwa mtu aliyemaliza/ kulipiwa mkopo kutoka taasisi nyingine, nimeamua kutoa la moyoni kwa viongozi ambao najua wamo humu baadhi akiwemo mama etu a...,ki ukweli roho imeniuma sana baada ya kuona naendelea kukatwa na Bayport ikiwa nimemaliza mkopo wao.

Inawezekana pengine ni michezo ya baadhi ya watendaji ndani ya taasisi naomba uongozi haraka sana ufuatilie hii tabia hapa Kahama.

Ikiwa kweli taasisi hii ilianzishwa kwa lengo la kusaidia watu iendelee hivyohivyo bila kuleta figisufigisu.

Mwisho napenda kutoa pongezi kwenu angalau sasa riba imepungua tofauti na yale maumivu ya mwanzo.

ZINGATIENI: Tendeni haki kwa wateja wenu kupunguza malalamiko kama yangu, madai yangu muhimu pia.
 
Nina sita kusema hao ni Majizi.. Kamwe sitakuja kurudia kukopa Bayport. Labda atakuwa mjukuu. Wale jamaa siyo niko huku Swax walinipandishia makato,kama haitoshi nikataka nirudishe mkopo wao eti nilipe za kwenye salary slip.Nilienda mpaka Headquarter nilikuta madudu matupu. Wabuluze mahakamani kama kwnye salary slip deni halisomi. Wezi wale sitakuja kopa tena kwao na wewe kama haujakopa usiende wapigaji wale.
 
Swala lako linatatulika nenda kwenye ofisi zao waangalie kwenye system.. watakurefund kama wamezidisha ni system error.. BAYPORT SASA MAKATO YAKO CHINI NA HAKUNA LONGO LONGO.. kwa maelezo zaidi mtu akitaka ani PM
 
mkuu pole sana kwa madhira kutoka byport sijui wanamatatizo gani,kuna vitu nimejibiwa hapa kahama mkuu nikiandika utacheka sana.
 
Bayport ni ile kampuni ya mikopo ya mama Ane Mkapa?
 
Hawa jamaa wezi nilikopa mil 1 na laki5 salary slip imekuja na deni la milioni 38 na laki saba.
 
Pole sana but nenda kachukue barua kwenye kampuni husika ya kuonesha kwamba umemaliza deni na huna deni lolote kwao then hiyo barua peleka ofisi ya HR halmashauri kwako watasitisha mara moja hayo makato kwenye Lawson then sasa dai hela yako iliyoenda Bayport wakati huna Deni tatizo kubwa la Walimu hamfuati procedure mnabaki kulalamika tu issue zingine kusolve ni simple mno eg hyo issue yako ni dk 1 tu inakuwa imeshaisha vilevile kabla hujakopa sehemu yoyote nakushauri uwe unaomba ushauri ofisi ya Utumishi kwani wao wanajua Taasisi zote za fedha zone nazokopesha zenye riba kubwa na zenye nafuu zenye matatizo na zisizokuwa na matatizo kwani hudeal hudeal moja kwa moja kuingiza makato ya watumishi kwenye Lawson.
 
Wezi sana hao waogopeni, waliokopa wanajuta kukopa bayport sasa hivi wanawashikisha ambao hawaifahamu
 
Riba ni haram! ndio maana watu wanaunda taasisi kwa ajili ya kufanya dhuluma
 
Swala lako linatatulika nenda kwenye ofisi zao waangalie kwenye system.. watakurefund kama wamezidisha ni system error.. BAYPORT SASA MAKATO YAKO CHINI NA HAKUNA LONGO LONGO.. kwa maelezo zaidi mtu akitaka ani PM

Sidhani kama ni kweli Bayport ni mwaka zaidi ya sita huu wanamkata mzee wangu pesa na anasema aliomba kurejesha yote afutiwe Mkopo wakakataa.
Pia kipindi wamesainiana ile mikataba jamaa wa Bayport walichukua na hawakurudisha kwa wahusika hivyo muhisika anashindwa kujitetea kiasi cha pesa alichokopa na marejesho yanayotakiwa!
 
Pole sana but nenda kachukue barua kwenye kampuni husika ya kuonesha kwamba umemaliza deni na huna deni lolote kwao then hiyo barua peleka ofisi ya HR halmashauri kwako watasitisha mara moja hayo makato kwenye Lawson then sasa dai hela yako iliyoenda Bayport wakati huna Deni tatizo kubwa la Walimu hamfuati procedure mnabaki kulalamika tu issue zingine kusolve ni simple mno eg hyo issue yako ni dk 1 tu inakuwa imeshaisha vilevile kabla hujakopa sehemu yoyote nakushauri uwe unaomba ushauri ofisi ya Utumishi kwani wao wanajua Taasisi zote za fedha zone nazokopesha zenye riba kubwa na zenye nafuu zenye matatizo na zisizokuwa na matatizo kwani hudeal hudeal moja kwa moja kuingiza makato ya watumishi kwenye Lawson.

mkuu mi wife anakatwa pesa na bayport wakati hajawahi kukopa huko ..hii inakuaje?
 
mkuu mi wife anakatwa pesa na bayport wakati hajawahi kukopa huko ..hii inakuaje?

Nenda ofisi zao kacheki kweli kama hakuchukua huo mkopo inaweza kuwa amechukua anakuficha we kacheki ofini kaa kuna mkataba wake kaa hakuna chukua barua peleka HR ofisi watasitisha.
 
Hawa jamaa wezi nilikopa mil 1 na laki5 salary slip imekuja na deni la milioni 38 na laki saba.

Inashangaza kuona Wizi huu Mkubwa wanaofanyiwa watumishi na serikali Ipo, hii kampuni inalalamikiwa sana na ni ya kinyonyaji, mfano katika wilaya Tandahimba watu wameingiziwa fedha kinyemela bila kuomba na kutakiwa kulipa mara 5 yake...Kama Hitla Aliangushwa Nao Wasijiamini saana.
 
Bay port ni wauajiiii tena sitaki hata kuwasikia na hapa nakomenti basi tu, sipendi hata kuwataja. mimi nilikopa 520,000. tena kwa kulaghaiwa na shemeji yangu ambae alikuwa anafanya kazi bayport. kwa kuwa nilikuwa na shida nikakubali wanipe then baada ya mshahara kutoka wamenikata hiyo pesa yao ambapo jamaaa kasema ni miaka mitano sasa baada ya muda kuzidisha zile makato na na miaka mitano yani ni zaidi ya maratatu ya nilichopewa nakuhusu kupungua kw riba inakuwaje ss wa zaman haipungui? mpka sasa wanakataa
 
Inashangaza kuona Wizi huu Mkubwa wanaofanyiwa watumishi na serikali Ipo, hii kampuni inalalamikiwa sana na ni ya kinyonyaji, mfano katika wilaya Tandahimba watu wameingiziwa fedha kinyemela bila kuomba na kutakiwa kulipa mara 5 yake...Kama Hitla Aliangushwa Nao Wasijiamini saana.
Nilienda kuwaona ili warekebishe hadi sasa salary slip bado inasoma hiyohiyo milioni 38
 
Rai kwa wananchi na mnaonisoma sasa, hili ni jambo la kweli kabisa na limetokea kwangu na si mtu mwingine sina chuki na taasisi ya bayport wal taasisi nyingine ya mikopo. niwashauri tu kama hujawahi kukopa BAYPORT, USIKOPEEEEEE HI NI ZAIDI YA KIAMA.
 
Hii taasisi ni WEZIII Kabisa miaka mitano imepita ila bado wanakata tu. F...ck Baypoti
 
Back
Top Bottom