Wahusika wakuu wa Bayport

Wahusika wakuu wa Bayport

Daaah pole sana Mkuu, dawa kawashitaki panapohusika maana huu ni uwizi wa hali juu

Kwa hiyo mkuu hapo mpaka umalize hizo m38 si jui mwaka gani asee, fanya hima peleka mahakamani wezi hao. na kila ninapo lisikia hili lijina la beypot na patwa na hasira natamani kama ninauwezo nilifungiage kabisa huko na kuwafilisi walipe wateja wanaodaiwa iwe fundisho. NIMEKOMAAAAAAAAA
 
Walichonifanyia bayport sitakaa nisahau. Namshauri yeyote mwenye shida ya mkopo atafute pengine pa kukopa hapo hapafai jamani kimbia hao wezi kama ukoma.
Nilikopa laki7 nikalipa zaidi ya mil2 na laki 7 nilikatwa hadi nikakata tamaa ya kazi. Nilienda ofsn kwao kulalamika wala haikusaidia
 
CRDB na NMB punguzeni urasimu kukokpesha watumishi, hizi kampuni zingine sijui hata kama zina leseni
 
Hawa jamaa wezi nilikopa mil 1 na laki5 salary slip imekuja na deni la milioni 38 na laki saba.

Bayport hata siku moja hawawezi kurekebisha makato yako utaendelea kupigwa danadana tu mpaka uchoke anayeweza kukurekebishia makato yako ni mwajiri wako tu kupitia ofisi ya HR we cha kufanya pale bayport wambie wakupatie tu barua ya kuonesha ya kwamba unachokatwa sio sahihi then peleka kwa HR wako wakurekebishie Bayport kamwe wao hata siku moja hawawezi kwenda kupeleka marekebisho hayo kwa mwajiri kwani unakula kwao nenda wewe mwenyewe.
 
Kwa hiyo mkuu hapo mpaka umalize hizo m38 si jui mwaka gani asee, fanya hima peleka mahakamani wezi hao. na kila ninapo lisikia hili lijina la beypot na patwa na hasira natamani kama ninauwezo nilifungiage kabisa huko na kuwafilisi walipe wateja wanaodaiwa iwe fundisho. NIMEKOMAAAAAAAAA

Nashukuru kwa ushauri wakuu itabidi nifanye hivyo maana itakula kwangu.
 
Ni washezi sana hata mie najuta nawashauri ndungu zangu msijaribu umeona wapi m2 unalipa m7.5
 
HR wangu alisema mpaka wanipe barua wao na wamegoma jamani msiende hao ni matapeli
 
Jamani si Bay port tu peke yake,kuna mijizi mingi aisee,FAIDIKA,PLATINUM.Kuna jamaa zangu yamewatokea puani,eg.alikopa platinum kiasi cha milioni 2,akaambiwa atarejesha kwa miezi 48 @ Tsh.134,000 ambayo ni sawa na 6milions na laki kadhaa wakati NMB kwa hiyo 2mil,utarejesha 2.75mil kwa 36 months @ 75,000.

Tatizo mojawapo lipo na wateja wenyewe,na njaanjaa zao wanasaini mkataba bila kuusoma vzr na bila mwanasheria na hata nakala tu hawabakiwi nao.
 
Sitaki hata kuwasikia hao, anayejua kuhusu mkopo wa kuanzia maisha wa Lapf anijuze tafadhali.
 
Mmliki wa bayport ni RIZ ONE Jk.aliinunua 2010.na akaajili wazungu na huduma zikawa bora kuliko ile ya anna mkapa.
 
Swala lako linatatulika nenda kwenye ofisi zao waangalie kwenye system.. watakurefund kama wamezidisha ni system error.. BAYPORT SASA MAKATO YAKO CHINI NA HAKUNA LONGO LONGO.. kwa maelezo zaidi mtu akitaka ani PM

Bayport sio kwa kukopa
 
inauma sana sikudhani kama limewatokea watu wengi namna hii,poleni ndugu zangu tushikane kwa nguvu zote kwa sauti ya pamoja yatakwisha
 
Pole sana but nenda kachukue barua kwenye kampuni husika ya kuonesha kwamba umemaliza deni na huna deni lolote kwao then hiyo barua peleka ofisi ya HR halmashauri kwako watasitisha mara moja hayo makato kwenye Lawson then sasa dai hela yako iliyoenda Bayport wakati huna Deni tatizo kubwa la Walimu hamfuati procedure mnabaki kulalamika tu issue zingine kusolve ni simple mno eg hyo issue yako ni dk 1 tu inakuwa imeshaisha vilevile kabla hujakopa sehemu yoyote nakushauri uwe unaomba ushauri ofisi ya Utumishi kwani wao wanajua Taasisi zote za fedha zone nazokopesha zenye riba kubwa na zenye nafuu zenye matatizo na zisizokuwa na matatizo kwani hudeal hudeal moja kwa moja kuingiza makato ya watumishi kwenye Lawson.

mkuu sidhani kama umepitia comment za watu humu ndani,na kwa ufupi tu ni kwamba hakuna mtumishi mpumbavu wa kukubali kukatwa bila kufuatilia ukiona mtu mzima analia ujue kuna jambo hawa watu nikikueleza namna wanavyocheza michezo ya kitoto hutaamini
 
serikali kupitia wizara ya fedha tunawaomba mskie kilio chetu kwanini baypot?????
 
nikipita karibu na jengo la blue roho ina sisimka nilikopa milioni moja na nusu deni milioni 6 inaniuma sana lakini!we ngoja.
 
Back
Top Bottom