Wahouthi warusha tena makombora kuelekea Israel

The Zanzibar Echo

JF-Expert Member
Joined
Apr 21, 2025
Posts
490
Reaction score
836
Jeshi la Israel linasema limefanikiwa kulidunguwa kombora lililorushwa kutoka nchini Yemen mapema leo.

Taarifa hiyo imekuja baada ya milio ya ving'ora vya hadhari kusikika kwenye maeneo kadhaa ya Israel, kutokana na kombora hilo.

Jeshi hilo halikusema ikiwa kombora hilo lilidunguliwa kwenye eneo gani wala madhara yaliyotokana nalo.

Wanamgambo wa Kihouthi, wanaodhibiti sehemu kubwa yaYemen, ukiwemo mji mkuu Sana'a, ni sehemu ya muungano wa kijeshi dhidi ya Israel wenye mafungamano na Iran, ambao unajumuisha makundi mengine kama vile Hizbullah nchini Lebanon na Hamas katika Ukanda wa Gaza.

Tangu vilipoanza vita vya Gaza mnamo Oktoba 2023, Wahouthi wamekuwa wakirusha makombora mara kwa mara kuelekea Israel, ingawa jeshi la Israel limekuwa likidai kuwa mengi ya makombora hayo huwa yanadunguliwa bila kusababisha madhara yoyote.

Wahouthi wamekuwa pia wakiziandama meli zenye mafungamano na Israel zinazopita kwenye Bahari ya Sham, wakidai kuwaunga mkono Wapalestina.

Israel, kwa upande wake, imefanya mashambulizi kadhaa dhidi ya kile inachosema ni miundombinu ya kijeshi ya Wahouthi, ikiwemo bandari ya Hodeida na uwanja wa ndege wa Sana'a.
 
haya mashambulizi ya wahouth huwa yanafaida gani mbona yanaishia kupanguliwa

Sent from my Infinix X663 using JamiiForums mobile app
 
Naweza sema kwenye vita ukiwahi kuvimiliki vyombo vya habari basi wewe ni mfalme wa ulimwengu
 
Hawa wapiganaji ni wajinga Sana huwezi kushinda vita na Israel Kwa kurusha makombora..... UJINGA ni mzigo sana
 
Wakiskia king'ora tu wameingia chakani,sasa hata hizo kodi zao si zinaenda bure,bora warudishe mijengo wakae humo humo kwenye makalavati.
 
Hapo magaidi wa kihouthi wametoa kibali cha kushambuliwa. Hapo Israel inaenda kuwatandika bila ya kulaumiwa na yeyote.
 
Nahisi kuna kadhaa huwa yanafika vzr tu Israel , sema habari zinafichwa.
Wasingeendelea kurusha tu makombora wakijua yatapanguliwa yote kila mara.
 
Back
Top Bottom