Wahitimu wa Vyuo tuache kulalamika

Graduate wa kizazi hiki tunatia aibu, kila siku kulalamika, nimehitimu na wenzangu ninachoongea nakiona, unakuta mtu ana degree hata kutafuta na kutuma nafasi za ajira hawezi ,nina jamaa zangu kila kukicha ni kulaumu serikali, lkn hawana muda wa kujifunza kuandika CV,COVER LETTER na APPLICATION LETTER zenye USHAWISHI.....

Kila siku wao nikulalamikia serikali tu, nilikuja kushangaa mwenzangu tuliyehitimu naye haijui hata PSRS UTUMISHI, MABUMBE,JOB NET,AJIRA LEO,E-KAZZI,BRIGHT MONDAY N.K YEYE NI KULALAMIKA TU.... cha ajabu hata kuandika CV, barua za maombi hawezi, huyu ni sample, lkn nilifaya utafiti ni wengi sana ya wahitimu wapo hivi, binafsi niliamini ktk MAOMBI, JUHUDI kisha bahati hufata mkondo.....

nilipohitimu tu chuo ilinichukua miezi mitatu tu kuajiriwa na KAMPUNI YA MZUNGU...Hapa hapa TZ kwa mshahara wenye figure 6,

Sikutaka kuamini maneno ya wenzangu tukikutana vijiweni eti OHOO UTUMISHI HAWAFAI, UTUMISHI WANAWEKA NDUGU ZAO, UTUMISH MITIHANI MIGUMU BORA USIENDE, AJIRA NGUMU SANA(Sikatai ni kweli lkn je unatuma maombi ? ajira kila siku zinatangazwa kama hujui hasa za makampuni binafsi, mimi )

Nilikuwa nikitoka kijiweni, nawasha laptop yangu nitakesha nitatuma maombi kila sehemu ,kupitia Platform mbalimbali.... Siku moja nikaona tangazo la kada yangu Mzungu ANATAKA mtu, nikicheki nina sifa kasoro moja sina experience ya miaka anayotaka, NIKATUMA HIVO HIVO...

Baada ya siku 2 akanicheki tukajadili akasema atanipa another position ktk kampuni yake, nipo mpaka sasa , hata vyeti hajawahi kuniomba....

Wakati huo NIMESHAOMBA kazi utumishi ili nijaribu maneno ya watu je kupita ni ngumu...for the first time NIKAPITA WRITTEN.... nikaenda ORAL.... sikubahatika kutoboa.... LKN NILIJIFUNZA VITU Kwanza watu wanakatisha tamaa, maana wengi hawakuja ,pia maneno kuwa mitihani inavuja yanakatisha tamaa,

Nakumbuka baada ya mtihani kuna jamaa yangu mlalamishi sana kwa serikali...aliupiga picha...jion akaupost whatsapp groups, cha ajabu nikaanza kuona tuhuma ule mtihani ulivuja,.....huku na yeye akiaminisha watu hivo...maana kwenye Written hakupita...

juzi nimesikia mtihani wa TAX kama sijakosea ulivuja... siwezi kulisemea lkn.... hizi habari zinakatisha tamaa , lkn mjiulize kama ulivuja why haukuletwa humu kabla, umeletwa baada ya kufanyika.....

Graduate tuache lawama, tuhangaike, tufanye juhudi, tuombe MUNGU,tuwe wabunifu... Mungu hamtupi mja wake ,omba nafasi za kazi, usikatishwe tamaa....

binafsi nimekuwa nikiitwa interview kila siku hadi nimezikinai...na nipo kazini .....

NIMEKUJA KUHITIMISHA KUWA VIJANA TUNALALAMIKA SANA LAKINI HATUJISHUGHULISHI....
😂😂😂😂Uyu nae bana kuitwa umesikia watu hawaitwi kwa interview??? Ishu ni kupata kazi ..... Serikali enyewe inasema hamna ajira za kututosha wote afu we kima unasema ajira zipo
 
Mtu akisema hivi ,basi mimi huwa naona anavusha wenzie maana hatatokea kwenye interview...akiamini tyr ile nafasi ina mtu.... mimi hata nafasi iwe 1 naitaigombania tu.. nikashindwe mbele ya safari
Sa we si mjinga..... Unaposema ivyo lazima uangalie na logistics zimekaaje uko Dar nafasi imetangazwa moja Kigoma usahili unafanyika Kigoma nawe unaenda hoping for the best but actually it's the worst .... I never take uncalculated risk
 
Ni kweli CV zinaweza kua tatizo lakini ajira pia ni tatizo kubwa zaidi. Huyu mwamba yeye kachukua sample size ya washkaji zake aliomaliza nao, je huko alikoenda kwenye hizo interview alikua peke yake??

Tuache kuona wasio nacho wazembe, huu uzi ungeleta kipindi huna ajira kama hao wenzio wala haya maneno ya kua unasema ivo kisa we umepata sijui kupata ni bahati na maneno ya hivyo yasingelikuepo.

Na kuna mwamba apo juu nae anakazia zaidi kua ishu ni CV, eti kazi zinatangazwa kila siku na Ngo's, tuache kudanganyana jaman, na kama izo kazi kweli zinatangazwa nyie wenye access na huko mnashindwa nini kushare hapa jf badala yale mnakuja kutambia kua kazi zipo ila watu hawajui izo plafform zinazotangaza hizo kazi.

Baadhi ya wasomi wetu mkiongozwa na mleta mada ni wachoyo wa maarifa, huyu mleta mada pamoja na kuzijua hizo bado hawafumbui macho rafiki zake bali anaenda kuapply peke ake huku akiwacheka wenzie kua ni wajinga na wavivu 😂😂, ila bongo nyoso aisee.

Nae huyu mtetezi wake hapo juu hasemi pia ni wapi huko zinakotangazwa izo kazi. Naye kashikilia tu najua najua najua!!! Fungua macho watu acheni huo ubinafsi sio lazma muombwe, mbna ujinga wa wenzenu mnautangaza ila mlipopita ninyi mkatoa ujinga hamsemi.

Ulijua kwa kuambiwa nawe waambie wenzio wejue.
 
1. Hatuwezi kuandika barua.
2. Hatuwezi kuandika CV.
3. Tunalalamika sana.
4. Hatuombi kazi tupo vijiweni.
5.Tunakata tamaa.
6. Tumekuwa wakuda (tinavujish mitihani)

Dah ndugu yangu umetunanga sana ila yote ya yote Mshukulu Mungu kwa hiyo nafasi uliyoipata na wala usiite kukinai hizo simu za interview unazopigiwa Mungu anakusudi na wewe kukufungulia neema zake. Na wala usiwaze ktk kuamini rafiki yako ni sample yakina sisi tunaokosa bahati uliyokuwanayo wewe.
Kila kitu kina mtihani wake ktk ulimwengu huu hata mafanikio uliyokuwanayo ni mtihani mbele ya Muumba wako usikengeuke muombe Mungu neema uliyoipata na wengine waipate.
 
Acha tu ndgu ni vema jamaa angekuja na elimu zaidi kua namna gani mtu anaweza andika CV yenye ushawishi, mahali anakoweza kuona hizo post ila mwamba kawananga kinoma noma 😂😂.
Kuna bro angu alimazaga chuo tena kipind cha jakaya alisota kitaa mwaka mzima na CV yake ilikua imeshiba na kutuma maomb huku na kule.
Sometimes kuna bahati pia wakuu hili tulikubali pia ,japo juhudi ni muhimu zaidi tusitegemee bahati.
 
Acha tu ndgu ni vema jamaa angekuja na elimu zaidi kua namna gani mtu anaweza andika CV yenye ushawishi, mahali anakoweza kuona hizo post ila mwamba kawananga kinoma noma .
Kuna bro angu alimazaga chuo tena kipind cha jakaya alisota kitaa mwaka mzima na CV yake ilikua imeshiba na kutuma maomb huku na kule.
Sometimes kuna bahati pia wakuu hili tulikubali pia ,japo juhudi ni muhimu zaidi tusitegemee bahati.
kazi tunayo tutanangwa mwaka huu.
 
Tumekuelewa mkuu, tunapaswa kubadilika kila mmoja kwa nafasi yake.

Tuache ile kusema nafasi yenyewe moja tayari ashawekwa mjukuu wa mkurugenzi.
Ndio ukweli wenyewe hata ukiacha kusema ndio .......kabudi......lubuva..... flani ndio kapewa nafasi we utafanyaje? Ukapoteze hela dom wakati watu wana majibu tayari😂
 
Anachoongea mdau ni kweli kabisa, Mimi ni Muhanga, baada ya kuacha kazi (Nilikuwa sijui kichapo cha mtaani) ili nigharimu almost mwaka na nusu mtaani natafuta kazi,hapo nina mke na mtoto alafu hata hela ya sukaar huna,
,
Baada ya kichapo cha kutosha hapo nimesha piga mizinga paka aibu, baadae nikakaa chini kutafakari nilipokosea, Baada ya kufanya critical analysis nikagundua nina mapungufu maeneo makuu mawili, la kwanza NIPO MBALI SANA NA MUNGU, la pili CV YANGU HAIJIUZI.

Baada ya kugundua hayo ikabidi nichukue hatua, kwanza nikaanza kumtafuta MUNGU, Pili nikaomba washkaji zangu wawili wantumie CV zao ili niangalie iliwezekana ni edit nitengeneze yangu, ebwana eeh hapo ndo nilipochoka, zile CV za jamaa yani hata ile yangu ilikuwa na afadhali,

Basi nikaamua kutengeneza CV yangu mimi kama mimi bila kuiga mahali, nikaiita New Era. Asikwambie mtu,haukupita mwezi nikaanza kuitwa kwenye interview, Nilipo gonga ya kwanza tu hapo hapo wakanipa kazi tena na mshahara mkubwa tu na ahadi kedekede, Sjakaa vizur nikapigiwa tena na taasisi ya serikali nikagonge interview, nikapiga baada ya siku tatu wakanipigia kuwa nimepita kwaiyo nikaripot kazin, wakati huo nlikuwa nimeshaanza kule kwa mwanzo,

Basi nikapiga pale mwez nikaacha nikaenda kule serikalin ila roho iliuma sana kuacha kaz ya mshahara mzur vile.Basi nikiwa serikalin nako nikapigiwa tena na kampun kubwa tu ya kimataifa ya mafuta niende kwenye interview, Hiyo sikuweza kwenda sababu nilikuwa tayar kazini alaf mkoani.

Kwaiyo nlichojifunza ni kuwa ukiona upo kitaa muda mrefu hupati kazi, Basi angalia vizur haya maeneo matatu huenda moja linashida. MAHUSIANO YAKO NA MUNGU, CV YAKO, UWEZO WAKO KUJIELEZEA KWENYE INTERVIEW.

Sent from my Nokia C1 using JamiiForums mobile app
Dah umeongea point sana
 
Ofisin nimewahi kuwa naenda ofisi ya HR wetu na Ni rafiki yangu.

Huwa ananionesha email siku wakitangaza kazi.

Kuna siku walitangaza kazi ya dereva wa Gari la ofisi akanionesha emails za maombi zilikuwa 400+. Alichofanya alichagua majina ya watu watano Kama shortlist. Wala huwa Hakuna hata kusoma email za kila mtu ni uongo.

Nimeona kazi nyingi Sana hawasomi email wala cv. Unamtajia email ya mshikaji wako anamuweka kwenye shortlist.

So vijana wenzangu jueni Hilo watu watakuja kuongea mengi humu ila bila network Hakuna kutusua. Najua watu watakuja humu kusema oooh mbona Mimi niliandika CV nikaitwa bila kujuana na mtu Hiyo ni Bahati sana. Asilimia zaidi ya 90 ya kazi ni network. 10 iliyobakia ndio Fortunate.

Mimi Mambo ya kuajiriwa ni nimeshaachana nayo nakomaa zangu na mishe zangu kitaa.

Sent from my CPH1803 using JamiiForums mobile app
 
Neno la hekima:
Mungu akikubariki ukafanikiwa muombe akuondolee kiburi cha kuona wasiofanikiwa ni wazembe"

Na wote tuseme Ameen
 
Anachoongea mdau ni kweli kabisa, Mimi ni Muhanga, baada ya kuacha kazi (Nilikuwa sijui kichapo cha mtaani) ili nigharimu almost mwaka na nusu mtaani natafuta kazi,hapo nina mke na mtoto alafu hata hela ya sukaar huna,
,
Baada ya kichapo cha kutosha hapo nimesha piga mizinga paka aibu, baadae nikakaa chini kutafakari nilipokosea, Baada ya kufanya critical analysis nikagundua nina mapungufu maeneo makuu mawili, la kwanza NIPO MBALI SANA NA MUNGU, la pili CV YANGU HAIJIUZI.

Baada ya kugundua hayo ikabidi nichukue hatua, kwanza nikaanza kumtafuta MUNGU, Pili nikaomba washkaji zangu wawili wantumie CV zao ili niangalie iliwezekana ni edit nitengeneze yangu, ebwana eeh hapo ndo nilipochoka, zile CV za jamaa yani hata ile yangu ilikuwa na afadhali,

Basi nikaamua kutengeneza CV yangu mimi kama mimi bila kuiga mahali, nikaiita New Era. Asikwambie mtu,haukupita mwezi nikaanza kuitwa kwenye interview, Nilipo gonga ya kwanza tu hapo hapo wakanipa kazi tena na mshahara mkubwa tu na ahadi kedekede, Sjakaa vizur nikapigiwa tena na taasisi ya serikali nikagonge interview, nikapiga baada ya siku tatu wakanipigia kuwa nimepita kwaiyo nikaripot kazin, wakati huo nlikuwa nimeshaanza kule kwa mwanzo,

Basi nikapiga pale mwez nikaacha nikaenda kule serikalin ila roho iliuma sana kuacha kaz ya mshahara mzur vile.Basi nikiwa serikalin nako nikapigiwa tena na kampun kubwa tu ya kimataifa ya mafuta niende kwenye interview, Hiyo sikuweza kwenda sababu nilikuwa tayar kazini alaf mkoani.

Kwaiyo nlichojifunza ni kuwa ukiona upo kitaa muda mrefu hupati kazi, Basi angalia vizur haya maeneo matatu huenda moja linashida. MAHUSIANO YAKO NA MUNGU, CV YAKO, UWEZO WAKO KUJIELEZEA KWENYE INTERVIEW.

Sent from my Nokia C1 using JamiiForums mobile app
mtupe maarifa basi na sisi ya kuandika CV nzuri ikiwezekena ata mkatuwekea na sample
 
Back
Top Bottom