Wahitimu wa Mzumbe University kulikoni?

Wahitimu wa Mzumbe University kulikoni?

Bambo

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2009
Posts
238
Reaction score
50
Zamani ikiitwa Institute of Development Management, na sasa ni Mzumbe university.Naomba tujadili wahitimu wa taasisi hiyo kwani wengi wao (about 80%) wakija huku ughaibuni kufanya masters kwenye proper universities wanakwama na nina ushahidi na hilo wanaambulia postgraduate diploma. Nimefanya utafiti wa miaka kama mitatu iliyopita kutoka universities za hapa UK kama Manchester,Aston university na birmingham's city university,Southampton, Leeds n.k hawa jamaa wana struggle sana kucope.Kinyume na wale wanaotoka Mlimani ambao wengi wao wanafanikiwa kupata hizo masters bila matatizo!!!
Sasa sijui tatizo ni nini?
Wahitimu wa mzumbe mlio humu mtanisamehe
 
Waingereza wana msemo GABBAGE IN GABBAGE OUT; sasa hawa jamaa wa mzumbe walikuwa wanafundishwa na waalimu waliokuwa na PH.D feki [ WAkina Warioba, Kamala etc] kwahiyo wao nao wakawa feki na ndio maana wanapokwenda kufanya post graduate programmes wanapata shida sana.
 
naomba utaje majina ya angalau wawili walioshindwa kupata masters huko UK na wakaambulia PGD ambao walipata bachelor mzumbe.

JF itakulinda kwani "It's where we dare to talk openly" ili kuondoa majungu, hata kama ni mimi magezi wewe taja tu.
 
Swala la kufeli masters za Uk haliwapati magraduate wa Mzumbe tu hata waliotoka Mlimani( at least namjua moja) wanafeli vile vile. Kumbuka kuna graduate wenye 1st class, second class(upper or lower) na Pass. Ukijiunga vyuo vya UK ukiwa na Pass uwezekano wa wewe kufeli ni mkubwa sana bila kujali ume graduate Mzumbe, Mlimani, SUA, UDOM n.k. Usemi wa samaki moja akioza wameoza wote umepitwa sana na wakati.
 
Back
Top Bottom