Wahenga walisema "utu busara ujinga hasara"

Mwanamageuko

JF-Expert Member
Oct 31, 2010
8,604
5,581
Ninajaribu kujikumbusha na kuwakumbusha kauli za wahenga ili tuone mustakabali wa Taifa letu pendwa Tanzania kwani wanasema wahenga ukupigao ndio ukufunzao. Tuendelee na nukuu za wahenga katika mustakabali wa siasa za nchi yetu:-

Mzee Mwinyi yupo kimya, Mkapa kimya, Warioba kimya, Cleopa Msuya kimya, Amani Karume kimya,” amesema Kingunge na kuongeza;

“Ukimya huu unatokana na nini? Hawa wote waliwahi kula viapo vya utii kwa Katiba. Mimi nahoji, wazee wenzangu vipi mnakuwa kimya? Nawaambia kuwa mnachofanya si sawa.

“Naomba wazee wote tujitokeze kuhesabiwa katika hili la uvunjifu wa Katiba na sheria.

“Kwa hakika, tatizo kubwa la sasa la nchi yetu ni ombwe la kiuongozi, kwasababu kama ni watawala tunao kweli kweli, lakini tunachokosa ni watawala wenye maarifa ya kiuongozi.

Inashangaza kuona wazee wastaafu kukaa kimya wakati nchi inakabiliwa na tatizo linaloweza kutuangamiza.

“Upande mmoja unanoa mapanga, unaandaa bunduki kwa ajili ya kuchinja na kuua na upande wa pili wapo raia tu, tena wasio na silaha zozote.”

Mzee Kingunge Ngombale Mwilu.

Hayo ni baadhi ya maneno ambayo yana tafakuri nzito sana kwa wenye kufikiri nawaomba tuendelee kuweka busara za wahenga.
 
Hapo ben ndo remote yenyew ya yote yanayoonekana ko asilaumiwe yule hata ukiuliza waliosoma nae wanakuambia hajawah kuwa na akili hata kidgo cjui tulifanya nn jaman wallah crudii tena kosa nililofanya
.
.
.
Kyenekyaka mkighanile une
 
Hapo ben ndo remote yenyew ya yote yanayoonekana ko asilaumiwe yule hata ukiuliza waliosoma nae wanakuambia hajawah kuwa na akili hata kidgo cjui tulifanya nn jaman wallah crudii tena kosa nililofanya
.
.
.
Kyenekyaka mkighanile une
:D:D Watanzania tulipoitwa WAPUMBAVU na yule mzee wetu sikudhani kama alimaanisha kiasi hiki ila tukiangalia nukuu nyingine tutaendelea kupata picha:-

"Kuogopwa ni sifa na ada ya madikteta, viongozi halisi hawapendi kuishiriki sifa hii. Kujenga mazoea ya kutii viongozi hata katika mambo haramu ni dalili ya woga, ni kukaribisha udikteta." Mwalimu Nyerere
 
Walichonga Kinyago Wakakiweka Sebuleni, Sasa Kimeanza Kuwatisha Wenyewe!!
 
Walichonga Kinyago Wakakiweka Sebuleni, Sasa Kimeanza Kuwatisha Wenyewe!!
:D:D:D Namba zinasomwa kila mtindo awamu hii ila tuendelee kujikumbusha

"Katiba hii imenipa Madaraka makubwa sana, siku atakuja mtu ataitumia atakavyo na kuwa kama Mungu". Mwalimu Nyerere

Sishangai kauli kama vile "mkiona nimesimama hapa mjue kasimama Mungu!!" :(:eek::eek:
 
Back
Top Bottom