Wahehe na Tohara

Wahehe na Tohara

Mimi nilitahiriwa nikiwa na miaka 18 kwa hiari yangu sio utamaduni wetu kutahiri lakini sioni umuhimu wa kufanya hivyo glans sio sensitive kama niliyokuwa mwanzo ngozi yake imekuwa sawa na ya maeneo mengine kama mkono

Mhhh ulikuwa unawakwaza wenzako wewe, labda kama wa bara, lakini pwani demu akishagundua tu hujatoa hiyo kitu anatoka ndukiiiii....
 
Haya mambo ya kuiga iga siyo mazuri. Mi niko original hata jino sijawahi kutoa.
 
Mhhh ulikuwa unawakwaza wenzako wewe, labda kama wa bara, lakini pwani demu akishagundua tu hujatoa hiyo kitu anatoka ndukiiiii....

inawezekana ni kero sana.
 
Niliwai kushuhudia baba mmoja wa kiarusha akitandikwa fimbo na waarusha wenzake hadi kulazwa, kisa eti alimpeleka mwanawe hospital kufanyiwa tohara baadala ya jando,
Dah kuna baadhi ya makabila yana mila ngumu sana
 
kutahiri ni kutokana na familia ulio mbna mm nmekulia mufindi kwenye machai na nmetahiriwa nikiwa sijijui yaani nimepata akili najiona nko safi hivo so kutahiri ni familia na familia km family yako wameelimika mbna faster
 
Nataka kufahamu tu! Wahehe hawana Utamaduni wa kuwatahiri watoto wao wakiume?

Nimeona wanaume watu wazima wakihamasishwa kufanyiwa tohara.
Si jambo baya ila ni vyema kuwatahiri wakiwa watoto.

Nilidhani ni wasukuma tu, wasiokuwa na utamaduni huu...
Ni makabila gani mengine hapa nchini wasiokuwa na mila na desturi hii?

Inaonekana ndio un?anza kupata exposure sasa au ndio umeanza kuingia kwenye kundi la wakubwa au tu so mfuatiliaji. Ni muda mrefu kiasi hili suala la tohara limeanza kuhamasishwa hasa baada ya kuona ni Moja ya sababu zinazochangia kuongeza maambukizi ya virusi vya UKIMWI. Kwa hiyo sehemu zenye maambukizi yanayoonekana kuwa ni makubwa tafiti na hata ufikiriaji huonyesha kuna uwezekano pia tohara katika eneo hilo yaweza kuwa si ya kuridhisha na hivyo kuna haja ya kuh?masisha. Hivyo kuna uwezekano kuwa ni kweli wengi hawajatahiri ndio maana wanahamasisha ili kupambana na ugonjwa huo. Lakini kubwa kuna mtu mmoja amechambua vizuri juu ya mikoa ambayo haw?na utamaduni wa kutahiri tangu awali na Iringa ni mojawapo isipokuwa kwa Waislamu walio pale na wengine waliojua hili mapema, hasa kwa kuwa hakukuwa na tatizo lililo sababishwa na hali yakutokutahiriwa kwa jamii ya watu hao na wengine wanaohusika.Jamii zililenga zaidi kutatua tatizo lililowakabili. Muda mwingi ilifahamika kuwa kwenye kanda ya Waislamu kwa maana ya Pwani Tanga na mingine no lazima tu wawe wametahiri na ilisemekana ni kwa sababu ya maelekezo ya imani. Sijajua historia ya Wakurya ya wao kutahiri.
 
Umeandika vyema! lakini hapo kwenye mikoa umeenda kombo kidogo.
Kilimanjaro wanatahiri toka zamani.

Nikweli mkuu...ila kimikoa kaenda kombo kabisa.kama dodom singida wanatahiri toka dhamani....hata hivyo asilimia kubwa ya watazania wanatahiriwa nimikoa michache tu ambayo hawatahiri.haswa makabila flaniflan..
 
Nikweli mkuu...ila kimikoa kaenda kombo kabisa.kama dodom singida wanatahiri toka dhamani....hata hivyo asilimia kubwa ya watazania wanatahiriwa nimikoa michache tu ambayo hawatahiri.haswa makabila flaniflan..
Kama wasukuma hivi
 
Makabila yaliyokuwa yanatahiri wanaume nchi hii kabla ya ujio wa mkoloni hayazidi mawili nayo yalitahiri tu wale waliokuwa na matatuzo ya ku-slidisha mkono wa sweta; zaidi yalikeketa wanawake tu sasa unaposema wasukuma sijui wahehe ndo hawatahiri vijana wao ni mzungu au mwarabu wa oman?
Unasemaje wewe? Mi ni wa pwani nna historia ya ukoo wetu toka karne ya 11 mkoloni mzungu hata tongo hazijamtoka na tangu enzi hizo walikuwa wakiondoa govi. Basi tu siku hizi jiji limebadilika enzi hizo govi hakuwa na namna ya kuoa watu wa pwani kama hajatahiri. Kwa kifupi makabila ya pwani yamekuwa yakitahiri karne nyingi nyuma.
 
Unasemaje wewe? Mi ni wa pwani nna historia ya ukoo wetu toka karne ya 11 mkoloni mzungu hata tongo hazijamtoka na tangu enzi hizo walikuwa wakiondoa govi. Basi tu siku hizi jiji limebadilika enzi hizo govi hakuwa na namna ya kuoa watu wa pwani kama hajatahiri. Kwa kifupi makabila ya pwani yamekuwa yakitahiri karne nyingi nyuma.
Unajua waarabu wameanza kuingia mwambao wa pwani karne ya ngapi?
Ipo siku utadai makabila ya pwani yamekuwa wafuasi wa imani ya kiarabu/uislam hata kabla ya muingiliano na waajemi na waarabu.
 
Mkuu, wahehe hawatahiri, mikoa mingi sana tanznaia hawatahiri kabisa. mkoa wa iringa, njombe, mbeya, rukwa/sumbawanga, kigoma, mwanza,tabora,dodoma,ruvuma, kagera yote, Kilimanjaro, hawatahiri kabisa. ukiona mtu ametahiri ujue amekulia mjini au amejipeleka mwenyewe akiwa mtu mzima. au labda awe amezaliwa familia ya kiislam ndio wanatahiri, ila dini zingine hawathubutu kabisa.

mikoa wanayotahiri ni kama tanga, lindi, dsm, pwani,mtwara,arusha,mara/wakurya, manyara etc, hao wengine wanafanya kimila ila wengine ni kwasababu ya dini ya kiislam hasa ukanda wa pwani. in general, itis possible kwamba asilimia 50% ya watz wanatoka makabila yasiyotahiriwa na hawajatahiriwa kabisa hadi leo. nashukuru Mungu nimetahiriwa kwasababu kutotahiriwa ni aibu kubwa nafikiri, pamoja na kwamba natoka kabila lisilotahiri, isipokuwa, kama ningekuwa sijatahiri hadi leo, nisingetahiriwa kwasababu naamini mtu asiyetahiriwa pengine anapata ladha bora zaidi kuliko mimi niliyetahiri, ndio maana wazungu wameanza kampeni ya kukataza watoto kutahiri baada ya study kuonyesha mtu asiyetahiriwa anaona utamu kuliko aliyetahiriwa.
Ladha na aibu kipi bora?
 
Back
Top Bottom