Wahariri wa Mwanahalisi na Mawio wafungiwe, ni wachochezi

MTV MBONGO

JF-Expert Member
Feb 18, 2016
1,275
1,237
Kanuni na taratibu za uandishi zinataka mwandishi awe mtenda haki asipendelee upande wowote: ayaanike mazuri na mabaya na asiwe MCHOCHEZI! Nashangaa magazeti mawili Mwanahalisi na Mawio kujikita ktk kuvunja kanuni na maadili ya fani ya uandishi wa habari kwa kuendekeza UZUSHI NA UCHOCHEZI.

Mtakumbuka gazeti la Mwanahalisi liliwahi kufungiwa na sasa limeachiwa na cha ajabu hawajajirekebisha ktk kosa hili. nao Mawio wako kifungoni kwa kosa hilohilo. ni magazeti yanayojitahidi kuandika makala zilizoshiba vzr ila tu ni wachochezi na wanataka kutuvuruga sisi Watanzania.

Nadhani serikali inakosea kuyafungia magazeti badala ya wahariri, kwani wanaweza kuhama chombo kimoja cha habari na kwenda kingine au kuanzisha kipya. wahariri wachocjezi wanajulikana na hivyo wafungiwe kujihusisha na uandishi wa makala na habari ili tukae kwa amani.

Nayapongeza magazeti ya Tanzania Daima na Uhuru kwani licha ya kuwa ni magazeti ya vyama vofauti vya siasa hayachochei sana machafuko au chuki za kisiasa japo yanaonyesha wazi kuvipendelea vyama vyao.

Pongezi za dhati kwa magazeti ya Mwananchi, Jamhuri na Dira kwa kuikosoa serikali inapokosea na kuipongeza inapofanya vema. Haya ndiyo magazeti ya kuigwa na wahariri wake wanastahili pongezi kubwa kwani hayana upendeleo wowote.
 
Tatizo serikali yetu ina kansa, kwa nini wasiyapeleke Mahakamani wakatoe ushahidi wa kile wanachokireport kama wanaleta uchochezi?
 
Hawa ndio wahariri makini coz wanagusa wengi wasipo gusa mianaona mara mia hawa kuliko wale wa magazeti chama Uhuru na mzalend
 
Wewe utakuwa umetoka kuzimu sio bure, Mawio halipo, waambie hapo Lumumba siku hizi Alhamisi tuna gazeti la MSETO. Kanyaga twende....
 
Back
Top Bottom