Wahanga wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera hawajapata huduma wanayoistahili.

Alex Xavery

JF-Expert Member
Apr 19, 2015
230
196
Asante sana kwa kila binadamu aliyejaribu kwa namna yoyote ile kuwajali wahanga wa tetemeko la ardhi kwa msaada wa hali na mali.

Juhudi za serikali zote, kuu na za mitaa ni nzuri, japo ushirikiano kati ya serikali hizi mbili sio mzuri hata kidogo.

Asante kwa serikali za mitaa kwa juhudi kubwa za dharula za kuwajari wahanga, asante kwa juhudi za serikali kuu kwa mipango ya muda mrefu japo dharula hamuijui na namna ya utekelezaji wake.

Naomba kufikisha taarifa hii kwa ulimwengu kwamba japo zipo familia baadhi zimeathirika kwa kiwango cha kutokuwa hata na chakula lakini kwetu sisi hili sio JANGA LA NJAA, mkoa Kagera madhara makubwa ya tetemeko la ardhi ni kuharibika kwa makazi ya watu.

Hivyo watu wanahitaji msaada wa haraka wa makazi ya muda mfupi na vifaa vya muhimu kama magodolo na vyombo vya ndani na vya kupikia ili kupisha ukarabati na ujenzi wa makazi yao yaliyoathirika.

Hivyo taasisi husika na watoaji wa misaada tusijikite sana katika kuwagombanisha wananchi kwa hivyo vyakula vibaba, badala yake waweza nunua turubai moja ama kwa uwezo wako na kwenda kuzitupia walau kaya mbili waweze kujikinga kwa baridi lkn pia kwa mnvua zijazo wakati ujenzi na ukarabati wa nyumba zao haujakamilika.

Hali ya makazi ni mbaya sana na sio hali ya vyakula na mavazi.

Asanteni sana na karibuni tuwasaidie wahanga wa janga hili.
 
yule wa wanyonge yuko wapi ?
naona jukumu kalipeleka kwa wafadhili..
yeye yuko bussy na ndege mpya..
 
Nashauri tu kile kitengo cha maafaa kilicho ofisi ya mkubwa kiondolewe tu wapewe wananchi maana naona wananchi wapo mstari wa mbele kusaidia maafa kuliko hicho kitengo
 
Back
Top Bottom