Usemayo ni kweli. Kimsingi kufanya kazi LGA ni laana. Kuna changamoto nyingi sana kwenye miradi ya ujenzi.
kuna hili la kurudisha fedha za miradi TAMISEMI.
Kwamba mnaletewa Tsh 200,000,000/= ya mradi alafu katika hiyo 50,000,000/= inarudishwa au inachukuliwa na hao jamaa wa TAMISEMI wakati BOQ ya mradi ji Tsh 200M. Mradi ukishindwa kuisha sisi tunalaumiwa na kusimamishwa kazi.
Kuna maagizo ya mdomo toka kwa MaRC, MaDC na MaDED wa chupi. Hawa ni wale waliohonga chupi zao na kuwa viongozi. Wanatoa maelekezo ya mdomo ukikataa unainua vita.
Kuna rushwa na 10% za viongozi kwa wakandarasi wa miradi ya ujenzi. Ujenzi lazima uwe substandard kwani pesa imeshaliwa na viongozi.
Ziara za kulishwa maneno na jazba za viongozi wetu kwenye miradi. Kwamba DED/DC/RC au hata WAZIRI analishwa maneno huko na hawa wenzetu wa TAKUKURU au ogisi ya DSO then anakuja kufanya ziara akiwa na jazba lakini akitaka pia apate chochote hapo.
Inasikitisha sana.