KERO Wahandisi wa Halmashauri tunaonewa

KERO Wahandisi wa Halmashauri tunaonewa

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Wahandisi Ujenzi (Civil Engineers) waliopo Halmashauri zetu wanapitia wakati Mgumu sana.

Unakuta anasimamia miradi maelekezo anayopokea kutoka kwa Mkurugenzi (DED) na Mkuu wa Wilaya yanakuwa kinyume na utaalamu, unaweza ukaambiwa upige plaster leo na upake rangi leoleo, ukishindwa kufanya hivyo unaweza ukatafutiwa kosa na ukachukuliwa hatua, kimsingi ukitaka kufuata taaluma yako unaonekana hufai.

Pia, usafiri wa kupeleka Wahandisi site unakuwa changamoto sana mradi unaweza kuanza hadi unafika hatua ya kupaua Mhandisi hajawahi kwenda site kwa sababu DED hatoi usafiri na mafuta.

Ni wakati sasa Wizara ya TAMISEMI kufanya mabadiliko Mambo ya Kihandisi yaendeshwe kihandasi maana siasa zinakuwa nyingi sana kwenye kazi zinazohitaji utalaamu.

DEDs mipango na manunuzi ndio chanzo cha miradi kukwama na kuwa chini ya kiwango na kutokamilika lakini mdudu yakifanyika analaumiwa Mhandisi.

Wahandisi wa Halmashauri wanalipwa mishahara midogo sana, watu mmesoma wote miaka minne mnazidiana! Wizara husika ipo, Engineers Registration Board wapo, wanakula hela bure badala ya kutetea masilahi ya Wahandisi.

Wahandisi wa Halmashauri tuwe na umoja wetu.
 
AISEE UMEANDIKA UKWELI MTUPU

Hili linatokea kwenye halmashauri nyingi na inakatisha tamaa

Tatizo SIASA inaingilia Utaalamu au Proffession za watu
 
Usemayo ni kweli. Kimsingi kufanya kazi LGA ni laana. Kuna changamoto nyingi sana kwenye miradi ya ujenzi.

kuna hili la kurudisha fedha za miradi TAMISEMI.

Kwamba mnaletewa Tsh 200,000,000/= ya mradi alafu katika hiyo 50,000,000/= inarudishwa au inachukuliwa na hao jamaa wa TAMISEMI wakati BOQ ya mradi ji Tsh 200M. Mradi ukishindwa kuisha sisi tunalaumiwa na kusimamishwa kazi.

Kuna maagizo ya mdomo toka kwa MaRC, MaDC na MaDED wa chupi. Hawa ni wale waliohonga chupi zao na kuwa viongozi. Wanatoa maelekezo ya mdomo ukikataa unainua vita.

Kuna rushwa na 10% za viongozi kwa wakandarasi wa miradi ya ujenzi. Ujenzi lazima uwe substandard kwani pesa imeshaliwa na viongozi.

Ziara za kulishwa maneno na jazba za viongozi wetu kwenye miradi. Kwamba DED/DC/RC au hata WAZIRI analishwa maneno huko na hawa wenzetu wa TAKUKURU au ogisi ya DSO then anakuja kufanya ziara akiwa na jazba lakini akitaka pia apate chochote hapo.

Inasikitisha sana.
 
Hii nchi imeharibiwa na siasa uchwara za wanasiasa wapuuzi.

Kufanya kazi LGA imekua mzigo mzito kwa wataalamu kwanza pesa hakuna maagizo kila kona tena yasiyo na tija.

Nashauri taaluma ziheshimiwe japo kuna wataalam wengine wananzingua wajirekebishe.
 
Naomba niongezee
1/Msiahahara midogo,Tarura Eng anaanza na 2.2M wakati sisi tunaanza na 1.1M
2/Ukisema ufuate miongozo ya kiuhandisi unafokewa na mkurugenzi kama mtoto,yeye anataka kazi iishe haraka ili aonekane anafanya sana kazi na maboss zake
3/Usafiri wa kwenda site imekuwa changamoto,halafu mwisho wa siku they expect kazi ziende vizuri
4/OC tunapata wengine max 80k kwa mwezi,ukiomba usafiri unaambiwa hela ya OC ndiyo usafiri,IS THIS FAIR?
KAZI IKIWA NZURI WAKURUGENZI WANASIFIWA,IKIWA MBAYA MA ENG TUNASEMWA,WHYYYY??
ERB MKO WAPI KUTETEA HAKI ZETU?
TAMISEMI MKO WAPI SISI TUNATESEKA?
 
Huko halmashauri Sitaki hata kukusikia.

You cannot hold your proffesaionalism, Kwasababu unaongizwa na kusimamiwa na fools kama Baba levo.

Poleni sana Wasomi mnao fanya kazi LGA, Ndo maana wakati mwingine hua sishangai watu wakiiba pesa za mradi maana stress haziendani na mshahara
 
Kada zote ni hivyo.
Mkuu wa wilaya ni :
✓Mwalimu.
✓Daktari.
✓Mwanasheria.
✓Muhandisi.
Kifupi siasa imeuwa kila kada.
 
UPO SAHIHI..VIONGOZI WA HALMASHAURI WAMEJAA UMWAMBA, POROJO NYINGI..WEWE KAMA ENG FUATA TAALUMA YAKO INAVOKUELEKEZA NA MIONGOZO YA KAZI NDO MAANA UMEAMINIWA UKAWEKWA HAPO...NANYIE MA ENG WA HALMASHAURI MUACHE KUCHELEWESHA MADODOSO YA VIFAA KWAKUJIFANYA MNAJUA KILA KITU INAVIKIA MUDA MNATAKA KUM BY PASS HATA MTU WA MANUNUZI KWA KUMUINGILIA KWENYE TAALUMA YAKE...KWAKWELI LOCAL GOVERMENT NI PASUA KICHWA.
 
Siku hizi maanjinia ni walimu na manesi sijui nani alipendekeza utaratibu huu
 
UPO SAHIHI..VIONGOZI WA HALMASHAURI WAMEJAA UMWAMBA, POROJO NYINGI..WEWE KAMA ENG FUATA TAALUMA YAKO INAVOKUELEKEZA NA MIONGOZO YA KAZI NDO MAANA UMEAMINIWA UKAWEKWA HAPO...NANYIE MA ENG WA HALMASHAURI MUACHE KUCHELEWESHA MADODOSO YA VIFAA KWAKUJIFANYA MNAJUA KILA KITU INAVIKIA MUDA MNATAKA KUM BY PASS HATA MTU WA MANUNUZI KWA KUMUINGILIA KWENYE TAALUMA YAKE...KWAKWELI LOCAL GOVERMENT NI PASUA KICHWA.
Mainjinia tulionao wengi wao vimeo wamekalili nadharia ukisema shika mwiko uoneshe mfano anageuka mbogo anasema unamdharau
 
Kuna maagizo ya mdomo toka kwa MaRC, MaDC na MaDED wa chupi. Hawa ni wale waliohonga chupi zao na kuwa viongozi. Wanatoa maelekezo ya mdomo ukikataa unainua vita.
Duh!...noma sana
 
LGA Siasa imezidi utaalamu na hili linasababishwa na Njaa maana LGA kuna Njaa sana MaDC na MaDED wengi hawana weledi zaidi ya uchawa ili wasitenguliwe.
ERB,AQRB fanyeni kazi yenu huki LGA panawaumiza wataalam kisa Siasa
 
Wahandisi Ujenzi (Civil Engineers) waliopo Halmashauri zetu wanapitia wakati Mgumu sana.

Unakuta anasimamia miradi maelekezo anayopokea kutoka kwa Mkurugenzi (DED) na Mkuu wa Wilaya yanakuwa kinyume na utaalamu, unaweza ukaambiwa upige plaster leo na upake rangi leoleo, ukishindwa kufanya hivyo unaweza ukatafutiwa kosa na ukachukuliwa hatua, kimsingi ukitaka kufuata taaluma yako unaonekana hufai.

Pia, usafiri wa kupeleka Wahandisi site unakuwa changamoto sana mradi unaweza kuanza hadi unafika hatua ya kupaua Mhandisi hajawahi kwenda site kwa sababu DED hatoi usafiri na mafuta.

Ni wakati sasa Wizara ya TAMISEMI kufanya mabadiliko Mambo ya Kihandisi yaendeshwe kihandasi maana siasa zinakuwa nyingi sana kwenye kazi zinazohitaji utalaamu.

DEDs mipango na manunuzi ndio chanzo cha miradi kukwama na kuwa chini ya kiwango na kutokamilika lakini mdudu yakifanyika analaumiwa Mhandisi.

Wahandisi wa Halmashauri wanalipwa mishahara midogo sana, watu mmesoma wote miaka minne mnazidiana! Wizara husika ipo, Engineers Registration Board wapo, wanakula hela bure badala ya kutetea masilahi ya Wahandisi.

Wahandisi wa Halmashauri tuwe na umoja wetu.

Wewe siyo Mhandisi bhana, sisi wahandisi tuna chombo chetu kinaitwa Engineers Registration Board (ERB) ukiona Kuna jambo lisilokuwa na tija au afya Njema kwa taaluma Yako unaripoti huko, ili likitokea jambo lolote Baya, ERB hawatakufungia usajili wako, maana utakayeathirika ni wewe kwa kufungiwa usajili.

Usikubali hilo mkuu
 
Back
Top Bottom