Wahamiaji wapata afueni Italy

Wahamiaji wapata afueni Italy

Herbalist Dr MziziMkavu

Platinum Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
43,073
Reaction score
34,844
120318121333_malta.jpg

Maelfu ya wahamiaji haramu kuingia nchini Malta

Meli iliyokuwa imewabeba wahamiaji 102 waliookolewa inaelekea

nchini Italy baada ya Rome kukubali kuwaruhusu wahamiaji hao kuingia

nchini humo na hivyo kumaliza hali ya suitofahamu iliyokuwepo kati ya

wamiliki wa meli hiyo na maafisa wa Malta

Waziri mkuu wa Malta Joseph Muscat aliishukuru serikali ya Italia kwa kusema kuwa uamuzi huo utaimarisha uhusiano kati ya nchi hizo.

Malta ilikataa shinikizo za Muungano wa Ulaya kuwaruhusu wahamiaji hao kuingia nchini humo ikisisitiza kuwa meli iliyokuwa imewabeba iwarejeshe Libya.

Ilisisitiza kuwa kuwaruhusu waingine nchini humo ingeweza kutoa taswira mbaya kwa wahamiaji haramu.
Kisiwa hicho kidogo hupokea maelfu ya wahamiaji haramu wanaoelekea Ulaya kila mwaka .
Meli ya mafuta iliyokuwa imewabeba wahamiaji hao kutoka Libya ikielekea Malta ilikuwa inaelekea katika bandari ya Syracuse Jumatano asubuhi kulingana na maafisa wa trafiki baharini.

Kulingana na jarida la Times nchini Malta, kikundi kipya cha wahamiaji 86 kiliwasili nchini humo Jumatano asubuhi,baada ya kuokolewa ufuoni.

Tume ya Ulaya iliambia Malta siku ya Jumanne kuwa ina jukumu la kuwakubali wahamiaji hao ambao miongoni mwao kulikuwa mwanamke aliyekuwa amejeruhiwa , wanawake wanne wajawazito, na mtoto mwenye miezi mitano kwa msingi ya ubinadamu.
Wahamiaji wapata afueni Italy - BBC Swahili - Habari
 
Afrika.Afrika.Afrika.
Pamoja na raslimali nyingi ulizonazo ila wanao ni maskini wakutupwa na kuokotwa Malta na kisha kuhurumiwa na Italia.
Hadi lini?Viongozi walafi wanaojali matumbo yao na familia zao.Hadi lini?
 
Napata taswira ya wanyarwanda lakini mpango wa wahamiaji wa Kagame ni strategic na wakuogopwa kama ukoma

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
120318121333_malta.jpg

Maelfu ya wahamiaji haramu kuingia nchini Malta

Meli iliyokuwa imewabeba wahamiaji 102 waliookolewa inaelekea

nchini Italy baada ya Rome kukubali kuwaruhusu wahamiaji hao kuingia

nchini humo na hivyo kumaliza hali ya suitofahamu iliyokuwepo kati ya

wamiliki wa meli hiyo na maafisa wa Malta

Waziri mkuu wa Malta Joseph Muscat aliishukuru serikali ya Italia kwa kusema kuwa uamuzi huo utaimarisha uhusiano kati ya nchi hizo.

Malta ilikataa shinikizo za Muungano wa Ulaya kuwaruhusu wahamiaji hao kuingia nchini humo ikisisitiza kuwa meli iliyokuwa imewabeba iwarejeshe Libya.

Ilisisitiza kuwa kuwaruhusu waingine nchini humo ingeweza kutoa taswira mbaya kwa wahamiaji haramu.
Kisiwa hicho kidogo hupokea maelfu ya wahamiaji haramu wanaoelekea Ulaya kila mwaka .
Meli ya mafuta iliyokuwa imewabeba wahamiaji hao kutoka Libya ikielekea Malta ilikuwa inaelekea katika bandari ya Syracuse Jumatano asubuhi kulingana na maafisa wa trafiki baharini.

Kulingana na jarida la Times nchini Malta, kikundi kipya cha wahamiaji 86 kiliwasili nchini humo Jumatano asubuhi,baada ya kuokolewa ufuoni.

Tume ya Ulaya iliambia Malta siku ya Jumanne kuwa ina jukumu la kuwakubali wahamiaji hao ambao miongoni mwao kulikuwa mwanamke aliyekuwa amejeruhiwa , wanawake wanne wajawazito, na mtoto mwenye miezi mitano kwa msingi ya ubinadamu.
Wahamiaji wapata afueni Italy - BBC Swahili - Habari

Fuatilia campaign za uchaguzi ujao Sept barani Australia mkuu hili ni janga, wahindi na waarabu wanaingia kila day kwa kisingizio cha asulym seekers. So wagombe Rudd na Abbort ndio wanakomalia hii ishu ya uhamiaji ifutwe(sometimes wanazamishwa baharin makisudi)
 
Back
Top Bottom