JAMHURI
JF-Expert Member
- Dec 15, 2010
- 449
- 60
M Chumvi
Wahamiaji Walowezi 6000 Wilayani Kiteto Mkoani Manyara, wameanza kutambuliwa kwa kuingizwa katika mfumo wa Kompyuta.
Kimkoa uzinduzi huo ulifanyika Kata ya Sunya Wilayani Kiteto, ambapo mgeni rasmi alikuwa Kamanda wa Uhamiaji Manyara, Afande Juliana Sagamiko.
Akizungumza na wananchi wa Sunya Kamanda Sagamiko alisema, zoezi hilo linafanyika nchi nzima, na wameamua lifanyike kwa mfumo wa Kompyuta.
"Awali tulianza kuweka kumbukumbu zao kwenye madaftari, lakini sasa tunawaingiza kwenye mfumo wa kompyuta kama njia salama"
Alisema kwa Mkoa wa Manyara wameanzia na Kata y Sunya ambayo ina wahamiaji Walowezi wengi takribani 6000.
Alisema bado katika maeneo mengine kuna wahamiaji walowezo wengi ambao nao watalazimika kuingizwa katika mfumo huo.
Kamanda Sagamiko alisema watahamia Wilaya ya Simanjiro kisha Wilaya zingine za Mkoa wa Manyara.
Paulo Magimbi mmoja wa wanao ingizwa kwenye mfumo huo alipongeza akisema, litakuwa chanza cha kutambuliwa kambila lake la Kikamba ambalo halipo miongoni mwa makabila zaidi ya 120 hapa Nchini.
Katika makabila 120 ya Tanzania sisi Wakamba hatumo..sasa tunaiomba Serikali yetu sikivu ya Dr. John Pombe Magufuli itambue Wakamba.
Alisema historia ya Wakamba inaeleweka kuwa walitoka Kenya miaka mingi iliyopita wakiwa kama wawindaji, baada ya kufika Tanzania wakaendele kuishi na walipotaka kurudi ilishindikana.
Wakati huo Rais Kenyatta wa Kenya alimdai Rais wa Tanzania Julius Kambarage Nyerere watu wake ambao ni Wakamba akaambiwa walikufa..ndipo wakazaa babu zetu nao wakazaa baba kisha sisi.
Alisema wao ni Watanzania halisi ambao hawana shaka ila wanachotaka ni kutambiliwa kama moja ya makabila hapa nchini
Hata hivyo taarifa za uhakika zinaeleza kuwa zoezi hilo litakuwa mwanzo wa kushawishi Wabunge kupitisha sheria ya kutambua kabila hilo la Wakamba.
Kwa upande wake Kamanda wa Uhamiaji Kiteto Ikomba Eliud Mathew aliwataka watu hao kujitokeza kwa wingi ili waweze kurahisisha zoezi hilo.
Alisema nia ya Serikali ni njema hivyo hakuna sababu ya watu kuhofu na kuwataka waiamini Serikali yao kwa kile inachokifanya hivi sasa.
Mwisho