Analogia Malenga
JF-Expert Member
- Feb 24, 2012
- 5,011
- 9,879
Watu 49 wanaodaiwa kuingia Tanzania bila utaratibu wakitokea Ethiopia wamekamatwa jana jioni Jumanne Novemba 3, 2020 na jeshi la uhifadhi na Misitu kikosi cha Tanapa katika hifadhi ya Taifa Saadani.
Wamekamatwa katika kijiji cha Saadani, kando ya Bahari ya Hindi, Bagamoyo mkoani Pwani.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Jumatano Novemba 4, 2020 na Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhifadhi, Paschal Shalutete inaeleza kuwa uongozi wa hifadhi ya Saadani umewakabidhi washukiwa hao kwa jeshi la Polisi na Idara ya Uhamiaji kwa hatua zaidi za kisheria.
“Tanapa inaendelea kusisitiza na kutoa onyo kwa wale wote wenye dhamira ya kutumia hifadhi za Taifa kwa vitendo ambavyo ni kinyume na sheria za nchi kuacha mara moja.”
“Jeshi la uhifadhi na misitu limejipanga vema kuhakikisha kuwa maeneo ya hifadhi yanaendelea kuwa salama kwa shughuli za uhifadhi na utalii na si vinginevyo,” imeeleza taarifa hiyo.