nngu007
JF-Expert Member
- Aug 2, 2010
- 15,860
- 5,803
[h=2][/h]Alhamisi, Januari 10, 2013 07:40 Na Sarah Mossi

KATIKA ukurasa wa mbele wa gazeti hili kuna habari ya kukatisha tamaa inayohusiana na hali ilivyo sasa katika Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar, baada ya baadhi ya watu wanaojiita Wahafidhina kudaiwa kutotaka kufanya kazi na wenzao wa CUF.
Kwa wale tunaokumbuka Zanzibar ilivyokuwa mara baada ya kumalizika uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi 1995, ukafuatiwa na ule wa mwaka 2000 na matokeo ya mauaji, ukafuatiwa tena na matokeo ya uchaguzi wa 2005, atakubaliana nami nikisema imetosha.
Katika chaguzi zote hizi tulishuhudia Zanzibar ikiingia katika kipindi kigumu na cha hali ya hatari, huku maisha ya Wazanzibar yakizidi kuw amagumu na uchumi kudidimia.
Matokeo haya ndiyo yaliyozaa wakimbizi wengi wakiwamo vijana na wazee wa kike na kiume kukimbilia nchi za Uingereza, Marekani na nchini Kenya kuomba hifadhi za kisiasa, ili kunusuru maisha yao.
Hakika hali hiyo haikufurahisha watu, lakini wapo watu walionufaika na hali ya vurugu iliyokuwapo Zanzibar ndio hao leo hii wanaojiita wahafidhina.
Licha ya kubuniwa miafaka lukuki yenye lengo la kuinusuru Zanzibar na kuratibiwa na watu wa ndani na nje ya Zanzibar, lakini haikufua dafu, bado hali ikaendelea kuwa tete.
Waswahili wanasema hakuna marefu yasiyo na ncha na wala Hakuna jambo lisilokuwa la mwisho, Hatimaye 2010 wananchi wa Zanzibar wakapiga kura ya maoni kutaka Serikali ya Umoja wa Kitaifa ili kuvinusuru visiwa vyao na watoto wao.
Mwaka 2010 Zanzibar ikaingia kwenye uchaguzi mkuu kwa salama na amani na matokeo yalipotangazwa ingawa mgombea wa CUF alishindwa na CCM kuibuka kidedea, lakini hakuwapo mshindi na Serikali ya Umoja ikaundwa.
Ikiwa ni miaka miwili tu tangu kuundwa kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa, hali imeanza kuwa siyo ya kufurahisha miongoni mwa watendaji wa ngazi za juu katika serikali hiyo.
Tunaelezwa watendaji wananuniana, kila mmoja na lake, ukiuliza eti ni wahafidhina hawataki umoja wa kitaifa, kana kwamba Zanzibar ni mali yao na watoto wao.
Tuseme ukweli bila kuficha, hawa watu wanaojiita Wahafidhina, ndio wanaiharibu Zanzibar ambayo sifa yake kuu ni Zanzibar njema atakaye na aje.
Hawa wahafidhina ndiyo waliyoifikisha hapa Zanzibar ilipo. Siyo ile Zanzibar tuliyoachiwa na mabibi na babu zetu. Hivi sasa mwananchi wa Zanzibar anashindwa kumudu kula hata mlo wake mmoja tu. Zanzibar ninayoijua mimi ilikuwa ni kula mara tatu. Leo hii kila kona ya Visiwa hivyo watu wanalia. Hakuna wa kumnyamazisha mwenzake.
Wahafidhina hawa ndio wamesababisha kuwapo na makundi ya kidini, kama vile uamsho. Tusiume maneno wanachama wa chama fulani ndio wanatokana na kundi hilo. La hasha! Nakataa hapa ndio walipotaka Wahafidhina kutufikisha.
Nitatoa sababu moja tu kuihalalisha kauli yangu kwamba Wahafidhina ndio Uamsho. Kwamba historia ya ubaguzi wa kidini Zanzibar haukuwapo. Waislamu na Wakristo wa visiwani walishirikiana kila Nyanja.
Wakati wa Sikukuu za Kiislamu, Wakristo walialikwa kujumuika pamoja na wenzao kusherehekea sikukuu hizo na wakati wa sikukuu za Wakristo , Waislamu nao walialikwa. Hii ndio Zanzibar waliyoiacha bibi zetu akina Mother Jessie Amour.
Nimelazimika kulitaja jina la Bimkubwa huyu kwani wale wanaomjua watakuwa mashahidi kuwa aliishi vipi ingawa alikuwa ni mkristo lakini, nyumbani kwake ukifika, utawakuta watu wa dini tofauti wakiwamo Waislamu na Wakristo wamefika wakifanya mazungumzo ya hapa na pale.Huyu Bi Mkubwa alikuwa ndio nembo halisi ya namna ya Wazanzibar walivyoishi wa dini tofauti.
Lakini katika miaka ya karibuni kukajitokeza kundi la watu ambao hawajulikani walitokea upande gani wa Zanzibar wanaojiita wenye uchungu na Zanzibar kwa maneno mengine Wahafidhina.
Wakaanza na mtindo wa kuunda vikundi vya kuhubiri dini na badala ya kuhubiri dini, wakaaza kutukana imani za wenzao. Wahafidhina hawa, wakaona kwenye dini wanaelekea kushindwa, wakaelekea kwenye siasa.
Cha ajabu kwenye siasa nako wameona wameshindwa baada ya kuwapo serikali ya maridhiano sasa wanarudi tena kwenye dini. Nia yao ni kutaka kuifanya Zanzibar isikalike ili wao wafaidike.
Hii ndio maana ya kauli yangu kwamba hawa Wahafidhina ndio Uamsho. Wanakuja na staili tofauti tofauti za madai, lakini lengo lao kubwa ni kutaka Wazanzibar wasielewane wenyewe kwa wenyewe.
Ushauri wangu ni kwamba wakati umefika wenye akili tumetambua nini Wahafidhina wanataka Zanzibar. Hawa wanajulikana kwa majina. Hakuna sababu ya kuwaonea aibu na wakati umefika tuwaambie Watuachie Zanzibar yetu.