Wagonjwa watano wapandikizwa Figo Benjamin Mkapa

kiwenini

Member
Joined
Nov 25, 2018
Posts
73
Reaction score
43
1552820655404.png

Hospitali ya Benjamin Mkapa imefanikiwa kupandikiza Figo jumla ya Wagonjwa saba tangu ilipoanza kufanya huduma hiyo kwa kushirikiana na Madaktari kutoka shirika la afya la Tokushukai lilopo nchi ya Japan.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto wakati alipofanya ziara ya kukagua hali ya utoaji huduma za kibingwa za magonjwa ya Figo katika Hospitali ya Benjamin Mkapa Jijini Dodoma.

Dkt. Ndugulile amesema kuwa Idadi ya wagonjwa waliokwishapandikizwa figo hapa nchini ni 43, ambapo 38 wamepatiwa huduma hiyo kwenye hospitali ya Taifa Muhimbili na wagonjwa watano(5) hospitali ya Benjamin Mkapa

“Hivi navyoongea tayari mgonjwa mmoja amekwishapandikizwa figo na ameshatoka salama, yupo anaendelea kuangaliwa, lakini wana mpango wa kuwafanyia wengine wawili tutapokuwa tumekamilisha hili tutakuwa na wagonjwa saba ambao wamefanyiwa hospitali hii” alisema Dkt. Ndugulile.

Dkt. Ndugulile aliendelea kusema kuwa, Serikali imelenga kuhakikisha kwamba inawajengea uwezo Wataalamu wa ndani kufanya upasuaji wa kibingwa ili waweze kuwahudumia Watanzania bila msaada kutoka Wataalamu wa nje.

“lengo na kusudio ni kuhakikisha kwamba tunajenga uwezo wa ndani wa kuweza kufanya upasuaji huu” Alisema Dkt. Ndugulile

Dkt. Ndugulile amesema kuwa Serikali imeokoa zaidi ya kiasi cha shilingi bilioni 4.2 ambacho kingetumika katika matibabu ya wagonjwa 80 mpaka 100 ambao wangepelekwa nje ya nchi kwa ajili ya matibabu.

“Wagonjwa waliokwishapandikizwa figo hapa nchini ni 42, kama tungewapeleka wagonjwa nje ya nchi ingegharimu serikali kiasi cha shilingi bilioni 4.2 kwa idadi hiyo ya wagonjwa. 80 mpaka 100, wakati huduma hii hapa nchini inagharimu kiasi cha shilingi milioni 21 kwa kila mgonjwa.” alisema Dkt. Ndugulile

Aidha, Dkt. Ndugulile amewashukuru Wataalamu kutoka shirika la Tokushukai kutoka nchi ya Japan kwa kujitoa na kuja kuwajengea uwezo Wataalamu wa ndani hali iliyosaidia kupunguza kiasi kikubwa cha fedha ambacho hutumika kwa ajili ya matibabu kwa wagonjwa wanaoenda kutibiwa nje.

“Kwa niaba ya Serikali ya Tanzania nimepita kuwashukuru na kuwapongeza, kwa sababu badala ya kutusaidia sisi samaki, wenzetu wa Japan wameamua kutupatia sisi mishipi na kutufundisha jinsi ya kujua naamini ujuzi huu utatusaidia sana ” alisema Dkt. Ndugulile.
 
Ni hatua nzuri lakini bado sio lakujivunua sana wakati hospital, vituo vya afya zahanati hazina madawa, tena yale muhimu!! Kwani wenye matatizo hayo ya figo ni wachache kulinganisha na wenye matatizo madogo madogo!! Afya ya msingi kwanza ndio muhimu, mfano juzi nimeona kiongozi mmoja anasema kwa huduma hizo sasa Tz ni kama ulaya vile???!!! Kweli? Kule huduma za msingi walishaziboreha miaka mingi!! Mgonjwa anakwenda hospital panadol tu hakuna, utamwambia habari za kupandikiza figo akuelewe?
 
Ni vizuri sana kuwa na uwezo wa kufanya upasuaji na upandikizaji mgumu kama huu ndani ya nchi yetu..haitatulazimu tena kuwa na mapesa ya kwenda nje..
 
Jambo zuri na la kupongezwa ila ukifika vituo vya afya hospital za wilaya na mikoa hasa ya hapo DODOMA hospitali hazijiwezi kwa kila hali mpaka majengo...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Safi sana ugonjwa wa figo ni mbaya sana na dawa yake ni dialysis au kupandikiza, vyote ni gharama lakini zitashuka jinsi siku zinavyokwenda. Napongeza hatua hii!
 
View attachment 1047554

Hospitali ya Benjamin Mkapa imefanikiwa kupandikiza Figo jumla ya Wagonjwa saba tangu ilipoanza kufanya huduma hiyo kwa kushirikiana na Madaktari kutoka shirika la afya la Tokushukai lilopo nchi ya Japan.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto wakati alipofanya ziara ya kukagua hali ya utoaji huduma za kibingwa za magonjwa ya Figo katika Hospitali ya Benjamin Mkapa Jijini Dodoma.

Dkt. Ndugulile amesema kuwa Idadi ya wagonjwa waliokwishapandikizwa figo hapa nchini ni 43, ambapo 38 wamepatiwa huduma hiyo kwenye hospitali ya Taifa Muhimbili na wagonjwa watano(5) hospitali ya Benjamin Mkapa

“Hivi navyoongea tayari mgonjwa mmoja amekwishapandikizwa figo na ameshatoka salama, yupo anaendelea kuangaliwa, lakini wana mpango wa kuwafanyia wengine wawili tutapokuwa tumekamilisha hili tutakuwa na wagonjwa saba ambao wamefanyiwa hospitali hii” alisema Dkt. Ndugulile.

Dkt. Ndugulile aliendelea kusema kuwa, Serikali imelenga kuhakikisha kwamba inawajengea uwezo Wataalamu wa ndani kufanya upasuaji wa kibingwa ili waweze kuwahudumia Watanzania bila msaada kutoka Wataalamu wa nje.

“lengo na kusudio ni kuhakikisha kwamba tunajenga uwezo wa ndani wa kuweza kufanya upasuaji huu” Alisema Dkt. Ndugulile

Dkt. Ndugulile amesema kuwa Serikali imeokoa zaidi ya kiasi cha shilingi bilioni 4.2 ambacho kingetumika katika matibabu ya wagonjwa 80 mpaka 100 ambao wangepelekwa nje ya nchi kwa ajili ya matibabu.

“Wagonjwa waliokwishapandikizwa figo hapa nchini ni 42, kama tungewapeleka wagonjwa nje ya nchi ingegharimu serikali kiasi cha shilingi bilioni 4.2 kwa idadi hiyo ya wagonjwa. 80 mpaka 100, wakati huduma hii hapa nchini inagharimu kiasi cha shilingi milioni 21 kwa kila mgonjwa.” alisema Dkt. Ndugulile

Aidha, Dkt. Ndugulile amewashukuru Wataalamu kutoka shirika la Tokushukai kutoka nchi ya Japan kwa kujitoa na kuja kuwajengea uwezo Wataalamu wa ndani hali iliyosaidia kupunguza kiasi kikubwa cha fedha ambacho hutumika kwa ajili ya matibabu kwa wagonjwa wanaoenda kutibiwa nje.

“Kwa niaba ya Serikali ya Tanzania nimepita kuwashukuru na kuwapongeza, kwa sababu badala ya kutusaidia sisi samaki, wenzetu wa Japan wameamua kutupatia sisi mishipi na kutufundisha jinsi ya kujua naamini ujuzi huu utatusaidia sana ” alisema Dkt. Ndugulile.
Wazungu /wachina sijui???? wanafanya nini hapo?
 
Kwa nini kujikweza,kwani kuna ubaya gani wakiandika kuwa madaktari RAIA was Japan wamefanikiwa kupandikiza figo kwa kupitia hospitali ya Benjamin mkapa
 
Kwenyewe hospital za Wilaya na mikoa mgonjwa anauziwa file sh. 10,000/ alafu kumuona Dr. sh 5,000/ vipimo mfano kupima Choo sh, 3,000/+3,000/+mkojo +3,000/ jumla sh, 24,000/ uyu ni mtu wa kawaida na anamagonjwa ya kawaida akishamaliza anaambiwa hakuna dawa.

Ndo maana tunawaambia mmeingia mikataba ya kutupunguza (kutuua) kwa nja ya siasa .

Pesa mnatuibia huduma hakuna ivi mnataka nini zaidi ya uhai wetu?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom