Wagonjwa wagomea zawadi ya vyakula, wataka dawa

Rais2020

JF-Expert Member
Jul 14, 2016
3,248
5,537
Katika hali isiyotarajiwa, baadhi ya wagonjwa waliolazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Bukombe mkoani Geita juzi walikataa kupokea msaada wa vyakula na sabuni kama zawadi ya sikukuu ya Pasaka, badala yake wakaomba wapelekewe dawa na vifaa tiba.

Tukio hilo lililoacha gumzo lilitokea wakati kikundi cha Huruma kinachoundwa na wanawake wajasiriamali Wilaya ya Bukombe kilipotembelea hospitali hiyo kugawa zawadi kwa wagonjwa.

Mmoja wa wagonjwa waliogoma kupokea zawadi hiyo, Lucia Mbalala alisema muda umefika kwa wanaoguswa kusaidia wagonjwa kwa kutumia fedha kidogo walizonazo kununulia vitu muhimu vitakavyosaidia matibabu ikiwamo dawa na vifaa tiba badala ya chakula.

“Inamfaa nini kumpa zawadi ya chakula na sabuni mgonjwa aliyelazwa hospitalini siku tatu bila kupata hata ya panadol? Lazima Watanzania tubadilike kimtazamo kwa kukataa zawadi zisizo na tija katika maisha na jamii yetu,” alisema Mbalala.

Alisema badala ya kusaidia, wengi wanaotembelea wagonjwa na watu wengine wenye uhitaji maalumu hulenga kujipatia sifa kisiasa au kwa malengo mengine yanayojificha nyuma ya zawadi hizo.

Mgonjwa mwingine, Annastazia Deus alivitaka vikundi na watu binafsi wanaofikiria kuwasaidia wagonjwa kufikiria hata kuwanunulia nguo watoto wachanga ambao baadhi hawana nguo kutokana na hali duni ya wazazi wao, badala ya kila mmoja kukariri kuwa zawadi kwa wagonjwa ni chakula na sabuni pekee.

Akizungumza wakati wa hafla fupi ya kupokea zawadi hizo, Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya Bukombe, Dk Nyamhanga Range alisema hospitali hiyo yenye uwezo wa kupokea na kuhudmia wagonjwa 116 inakabiliwa na upungufu wa vifaa tiba.

Aliomba vikundi na watu binafsi wenye mapenzi mema kujitokeza kusaidia upatikanaji wa vifaa tiba kwa ajili ya makundi maalumu wakiwamo wazee, wajawazito na watoto.

“Tunahitaji mashine maalumu ya joto kwa ajili ya watoto wanaozaliwa kabla ya wakati, nepi na nguo kwa ajili ya watoto wachanga,” alisema Dk Range.

Mwenyekiti wa kikundi cha Huruma, Rebeka Juma alisema wanachama wa kikundi hicho walijitolea kujichangisha Sh316, 000 kwa ajili ya kununulia chakula na vifaa vya usafi kama sabuni kwa ajili ya wagonjwa kama mkono wa sikukuu ya Pasaka.

Alisema watafanyia kazi maombi ya wagonjwa na uongozi wa hospitali kuhusu vifaa tiba akiahidi kuwasiliana makundi na watu wengine kuangalia namna ya kusadiana kutafutia ufumbuzi suala hilo.
Chanzo:Mwananchi
 
Acha waisome namba....majukumu ya serikali hayo unatakaje watu binafsi wafanye.,.....dawa ni kazi ya serikali wanaacha kuwaambia wabunge wao waobane serikali ipeleke madawa wanaishia kulaumu watu binafsi.....wabunge wao kazi ni kuunga mkono hoja za serikali+bajeti uchwara...Acha tuisome namba
 
Naona watu wameanza kujielewa sasa!

Unapeleka Dawa ya Meno na Sabuni wamekwambia hawaogi au wananuka?

Na hii inanikumbusha Shilika moja lilivyopeleka misaada ya Penseli na Vifutio shule moja kule makete ilihali wale watoto hata sare za shule hawana.

Tupeleke misaada ambayo kweli italeta haueni kwa wahusika na sio tu borailimradi muonekane mmepeleka misaada.
 
Mkuu kumbuka hosptali dawa wananunua!

Wangefanya mahesabu ya kuwapatia angalau hata Pesa ya dozi moja ya dawa walizoandikiwa.
 
Naona watu wameanza kujielewa sasa!

Unapeleka Dawa ya Meno na Sabuni wamekwambia hawaogi au wananuka?

Na hii inanikumbusha Shilika moja lilivyopeleka misaada ya Penseli na Vifutio shule moja kule makete ilihali wale watoto hata sare za shule hawana.

Tupeleke misaada ambayo kweli italeta haueni kwa wahusika na sio tu borailimradi muonekane mmepeleka misaada.

[/QUmasikini hana usemi au msaada hauna masharti Nyerere alisemaga it's expensive to be poor
 
Hhuyo mgonjwa ni great thinker,
Lakini vijana wa LUMUMBA wakipita hapa
Watasema ooooooh hao ni wapiga diliii wametumwaaa,

Nisipigwe lakini.
 
Acha waisome namba....majukumu ya serikali hayo unatakaje watu binafsi wafanye.,.....dawa ni kazi ya serikali wanaacha kuwaambia wabunge wao waobane serikali ipeleke madawa wanaishia kulaumu watu binafsi.....wabunge wao kazi ni kuunga mkono hoja za serikali+bajeti uchwara...Acha tuisome namba
Teh teh teh teh
 
imebaki kutandaza michuma ardhin eti SRG na kujenga airport chato aina hata faida. Na kunakidaraja lingine slender had coco beach liko njiani 600 billions dollars imagine.

Inasikitisha
 
imebaki kutandaza michuma ardhin eti SRG na kujenga airport chato aina hata faida. Na kunakidaraja lingine slender had coco beach liko njiani 600 billions dollars imagine.

Inasikitisha
Tumepata Rais wa ajabu kweli kweli haijawahi kutokea(In Tundu lissu 's Voice)
 
Hongera zao wamejitambua kwa hili tangu lini mgonjwa anapelekewa zawadi kana kwamba kuugua ni vizuri. Wote wanaotafuta kiki mbele ya kamera kwa kuwapelekea wagonjwa zawadi na ibada zisizo rasmi wapigwe marufuku
 
Back
Top Bottom