Wagonjwa 268,224 wapata msamaha wa matibabu wenye thamani ya shilingi bilioni 34 .7

Wagonjwa 268,224 wapata msamaha wa matibabu wenye thamani ya shilingi bilioni 34 .7

Nipe Maji

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2025
Posts
335
Reaction score
190
Kati ya Kipindi cha Mwezi Julai 2024 hadi Machi 2025, Serikali imetoa misahama ya matibabu ya afya yenye thamani ya Shilingi 34,720,233,085.28 kwa wagonjwa 268,224 wasio na uwezo wa kumudu gharama za matibabu.

Hayo yamebainishwa na Waziri wa Afya Mhe. Jenista Mhagama alipokuwa akiwasilisha hotuba ya makadirio ya Bajeti ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Afya kwa mwaka wa fedha 2025/26.

“Misamaha imetolewa kwa wagonjwa waliopata huduma za uchujaji damu (Dialysis), huduma za mionzi kwa wagonjwa wa saratani, vipimo vya maabara, huduma za radioiojia, huduma za upasuaji, gharama za kumuona daktari, dawa na huduma za wagonjwa mahututi (ICU),” amebainisha Waziri Mhagama.

Waziri Mhagama amebainisha kuwa wagonjwa hao walipata huduma hizo katika Hospitali za Rufaa za Mikoa, Kanda, Maalum na Taifa.
 
Back
Top Bottom