Wagombea wa Republican washindania Nevada

thesym

JF-Expert Member
Aug 15, 2012
3,842
4,794
Wagombea urais wa chama cha Republican nchini Marekani wanakabiliana kwenye uchaguzi wa mchujo katika jimbo la Nevada katika kinyang’anyiro cha nne cha kuamua mgombea wa chama hicho.

Mfanyabiashara Donald Trump, ambaye amekuwa akiongoza kwenye kura za maoni kitaifa, anaongoza pia kwenye kura za maoni jimbo hilo, na anatarajia kupata ushindi wa tatu mtawalia baada ya kushinda New Hampshire na South Carolina.

Nevada, ambalo ni jimbo lisilo na mbabe na lenye watu wengi wa asili ya Amerika Kusini, ni muhimu sana katika uchaguzi.

Upigaji kura kwa sasa unaendelea na kuna foleni ndefu vituoni.

Kura ya maoni ya karibuni CNN/ORC imeonesha Trump ana uungwaji mkono 45% akifuatwa na Seneta Marco Rubio 19% naye Seneta Ted Cruz akiwa na 17%.

Ingawa Nevada ina wajumbe wachache, inatarajiwa kuwa mtihani kwa Trump kutokana na matamshi yake dhidi ya wahamiaji ikizingatiwa kwamba ina watu wengi wa asili ya Amerika Kusini.

Hillary Clinton alishinda kwenye jimbo hilo katika chama cha Democratic Jumamosi.

Alimshinda mpinzani wake Bernie Sanders kwa kumpita kwa asilimia tano na wagombea hao wawili sasa wanaangazia jimbo la South Carolina lenye watu wengi weusi.

Uchaguzi wa mchujo wa chama cha Republican katika jimbo la South Carolina utafanyika Jumamosi.

Uchaguzi wa mchujo hutumiwa kuchagua wagombea wa vyama viwili vikuu kwenye uchaguzi mkuu wa urais ambao utafanyika mwezi Novemba

source: bbc swahili

update
mchakato umemalizika na trump ameshinda
BhxgziGxSMDRd038.jpg


He thanks his sons, who are on stage with him, for their help.

This was very exciting tonight, but I’ll tell you, it looks like we won by a lot evangelicals, we love evangelicals. Thank you.

He thanks Jerry Fallwell, Jr, who has been running radio ads on Trump’s behalf, for being “with us from the beginning.”

“I love the poorly-educated,” he says.

He boasts about “46 percent with the Hispanics - number one! I’m really happy about that.”

Nevada Republican caucuses live: Donald Trump wins in record turnout
 
Na mtakia kila la trump ili aje aichangamshe dunia ikae katika mstali.
 
Hili lijamaa litachukua Ikulu (White House) kimzahamzaha. Misimamo yake inafurahisha japo michungu kwa baadhi ya makundi ya kijamii.
 
Hili lijamaa litachukua Ikulu (White House) kimzahamzaha. Misimamo yake inafurahisha japo michungu kwa baadhi ya makundi ya kijamii.
Mkuu, nimefuatilia kampeni za Trump na yote yanayosemwa juu yake nikagundua ni uongo na propaganda za kupikwa na "the establishment" au elite . Huyu jamaa ni mwanamageuzi halisi, hafungamani na matajiri waliokuwa wanaiongoza Marekani. Hata aina ya siasa zake imekiuka misingi ya Republicans. Hii imemfanya adui wa Democrats na Republicans. Pia ameonyesha anajua siri nyingi sana kuhusu conspiracies kama 9/11 na ameonyesha nia ya kuwashughulikia wahusika wote. Kuna baadhi ya wamarekani wanaamini Trump atauawa ili kumzuia asiitwae white house. Trump ni kama Magufuli, hafungwi na mipaka ya chama, kwake kweli itabaki kweli daima.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom