Wagombea Ubunge Morogoro kwa CHADEMA warejesha form; Waahidi makubwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wagombea Ubunge Morogoro kwa CHADEMA warejesha form; Waahidi makubwa

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Ramos, Aug 19, 2010.

 1. R

  Ramos JF-Expert Member

  #1
  Aug 19, 2010
  Joined: May 13, 2010
  Messages: 498
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Wagombea ubunge kwa Majimbo ya Morogoro Mjini na Morogoro Kusini mashariki kupitia CHADEMA wamerejesha form zao leo na kuahidi kufanya makubwa endapo wakichaguliwa.

  Mwanasheria Amani Mwaipaja ambaye anagombea kwa chama hicho Morogoro mjini amewaambia waandishi wa habari kuwa endapo atachaguliwa atatumia jitihada na uwezo wake wote kuhakikisha kuwa mji huo unapata hadhi na heshima yake kama zamani. Ameyataja maeneo atakayoweka nguvu kubwa kuwa ni maji, barabara, maeneo ya wafanyabiashara wadogo na vikundi vya kujiendeleza kiuchumi hasa kwa wanawake.

  Naye Bw. Aquiline Magalambula ambaye anagombea katika jimbo la Morogoro kusini mashariki ameahidi kuweka nguvu kubwa katika kuboresha upatikanaji wa maji safi na salama, umeme vijijini, barabara na kilimo.

  (nimeshindwa ku-upload picha; naomba wadau mnielekeze)
  [FONT=&quot][/FONT]
   
 2. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #2
  Aug 19, 2010
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,632
  Trophy Points: 280

  Heshima kwako Ramos,

  Mkuu ingekuwa jambo la maana kama ungeweka profile za wagombea ubunge na ikiwezekana weka profile za wagombea wa vyama vyote vinavyoshiriki kugombea ubunge huko Morogoro ili wanajamvi tuyasome na kuwachambua.Ukianza kuleta wagombea wa chama chako tu utakuwa huwatedei haki wanajamvi na watanzania kwa ujumla.

  Wanajamvi wa majimbo mengine tafadhali tuleteeni yanayojiri kwenye majimbo yenu.
   
 3. R

  Ramos JF-Expert Member

  #3
  Aug 19, 2010
  Joined: May 13, 2010
  Messages: 498
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Nitazitafuta mkuu. Ilitokea tu kuwa wakati wanarejesha hawa wa CHADEMA nilikuwa around, nikalinasa tukio...
   
Loading...