Wagombea CCM wamwaga fedha kama njugu

Wagombea CCM wamwaga fedha kama njugu

OgwaluMapesa

JF-Expert Member
Joined
May 24, 2008
Posts
10,942
Reaction score
437
Ni kufuru iliyopitiliza inayoonyeshwa na baadhi ya wagombea watia nia ya kuutaka urais ambapo wanatumia fedha kupita kiasi katika zoezi la kusaka wadhamini huko mikoani.

Kwa wale wagombea ambao ni viongozi wa kiserikali wamekuwa wakitumia rasilimali za kiserikali kama vile magari, ndege, basi pamoja na madereva wa serikali katika mbio za urais.

BERNARD MEMBE

Membe amekuwa akitoa elfu arobaini (40,000/-) kwa kila mtu anayekuja kumdhamini katika urais. Pia anatembea na kundi la wasanii na watu maarufu ambao huwalipa kiasi cha Tsh. laki tatu (300,000/-) kwa kila mtu, kwa kila siku.

Wale wasaidizi wake ama wapambe wake wa karibu huwalipa kiasi cha Tsh. laki tano (500,000/-) kwa kila mtu, kila mtu.

Hapo achilia mbali gharama za kukodisha magari, gharama ya mafuta kwa wanaotumia magari binafsi na posho za madereva na walinzi.

Tusisahau ni Membe huyu huyu anayejipambanua kupiga vita rushwa na ufisadi wakati matendo anayoyafanya mikoani yanadhihirisha kubariki rushwa nchini.

Pia Membe anasaidiwa na tajiri mkubwa Afrika ambaye amekuja kuwekeza kusini mwa Tanzania

MAKONGORO NYERERE

Huyu ni mtoto wa Baba wa Taifa Mwl J.K Nyerere ambaye anajinasibu mara zote kuwa ni mtu safi asiye na doa, mpiga vita ufisadi nchini na mtu maskini.

Kwa mujibu wa taarifa za kina zinaonyesha Makongoro naye anatumia pesa kama kawaida katika zoezi hili la kusaka wadhamini.

Makongoro hutoa kiasi cha Tsh. elfu kumi (10,000/-) hadi elfu ishirini (20,000/-) kwa kila mtu anayedondoka wino wa kumdhamini kwa kila mkoa anaopita kusaka wadhamini.

Kama haitoshi Makongoro huambatana na kundi la wapambe na waandishi wa habari ambao huwalipa kiasi cha Tsh. elfu hamsini (50,000/-) kwa kila mtu kila siku.

Sote tujiulize mtu maskini yupo hivi? Pesa zote hizi za kuwalipa watu amezitoa wapi? Kama huyu si fisadi basi tumwiteje?

MWIGULU NCHEMBA

Huyu ni Naibu waziri wa fedha ambaye amejitosa katika kinyang'anyiro cha urais akiwa mmoja wapo wa watia nia kijana kabisa.

Mwigulu yeye hutoa kiasi cha Tsh. Elfu ishirini na tano (25,000/-) kwa kila mtu anayejitokeza kumdhamini.

Pia Mwigulu anatembea na wapambe wake maarufu kama "masalia wa chadema" pamoja ambao huwapa posho ya Tsh. laki moja kila siku pamoja na kugharamikia mafuta ya magari yao.

Pia Mwigulu huambatana na mpiga picha wake aitwaye Festo Sanga pamoja na aliyekuwa msaidizi wake wa Unaibu katibu wa CCM (Myeka) aitwaye Rubein ambaye huwalipa posho ya Tsh. laki mbili kwa kila siku. Pia hutoa hela ya mafuta ya gari lao.

Mwigulu huzunguka na gari la serikali na kutoa posho kwa madereva wote wa msafara.

SOSPETER MUHONGO

Muhongo amekuwa akitoa kiasi cha Tsh. elfu thelathini (30,000/-) kwa kila mtu anayejitokeza kumdhamini.

Pia Muhongo huzunguka na wapambe wake wapatao 50 ambao huwalipa kiasi cha Tsh. Elfu hamsini kwa kila mtu kila siku ambapo amewakodishia coaster wanalozunguka naye.

LAZARO NYALANDU

Nyalandu yeye huzunguka kwa kutumia ndege ya TANAPA na kutumia magari ya serikali kila mkoa anapokuwa.

Nyalandu hutoa kiasi cha Tsh. elfu ishirini (20,000/-) kwa kila mtu anayejitokeza kumdhamini.

Wapambe wake huwapa kiasi cha Tsh. laki moja kila siku ambapo hutembea na wapambe wasiopungua 30 kwenye kila mkoa.

SAMWEL SITTA

Sitta yeye anatumia basi maalum la wizara ya uchukuzi ambalo lina mpaka sebule ndani yake. Basi hilo hupanda yeye pamoja na wapambe wake. Katika msafara wake gari lake la serikali linakuwepo pia kwenye msafara.

Wasaidizi wake huwalipa Tsh. laki moja kwa kila siku kwa kila mtu. Pia hugharamikia mafuta ya basi pamoja na kutoa posho kwa madereva wake.

Sitta hutoa kiasi cha Tsh. elfu kumi na tano kwa kila mtu anayejitokeza kumdhamini.

Sitta ni maarufu sana kwa kupiga vita mafisadi lakini matendo yake yanaonyesha ana punje za ufisadi mdomoni.

STEVEN WASIRA

Wassira ni mmoja wapo wa wagombea ambaye anakumbukwa kwa kipindi cha nyuma kutuhumia na mahakama kwa kutoa rushwa wakati wa uchaguzi na hivyo kuvuliwa ubunge wake na mahakama.

Wassira amekuwa akizunguka na gari la serikali na kutoa kiasi cha Tsh. elfu ishirini tu kwa kila mtu anayejitokeza kumdhamini.

JANUARI MAKAMBA

Makamba amejitokeza katika mbio za kuisaka ikulu ambaye amekuwa akinunua kadi za watu kumdhamini kwa Tsh. elfu ishirini kwa kila mtu.

Januari hutumia gari la serikali katika kampeni zake.

JOHN POMBE MAGUFULI

Magufuli anazunguka mikoani kwa kutumia gari la serikali lenye plate number inayosomeka W UJ na hutoa kiasi cha elfu ishirini kwa kila mtu anayejitokeza kumdhamini.

DR. TITUS KAMANI

Kamani naye amejitosa kugombea na hutoa kiasi cha Tsh. elfu ishirini na tano (25,000/-) kwa kila mtu anayejitokeza kumdhamini. Amefanya hivyo katika mkoa wa Mwanza.

EDWARD LOWASSA

Edward Lowassa ambaye ni Waziri mkuu wa zamani anazunguka mikoani kwa kutumia gari binafsi na magari mawili ya wasaidizi na walinzi wake wapatao 10.

Lowassa huwalipa wasaidizi na walinzi wake kiasi cha Tsh. elfu kumi kwa kila siku.

Magari yake huwekwa mafuta na tajiri mmoja toka Arusha aliyejitolea kutoa huduma hiyo.

Kwa wale wanao mdhamini urais hupata fursa ya kusalimiana na kupiga picha nao na na kisha mpambe wake hutoa kiasi cha Tsh. elfu tano kwa baadhi ya wanaomdhamini Lowassa

..... Itaendelea .....
 
Mtoa mada ni TEAM LOWASSA.Anajaribu kutuonyesha kwamba fisadi Lowassa anatoa rushwa ndogo kuliko mafisadi wenzake na kwamba hatumii fedha nyingi kama wenzake. Kwa nini hakutaja private jet anayotumia na pesa wanazolipwa maelfu ya watu wa kumshangilia?
 
Mleta Maada nikibaraka wa lowasa! Yaani huyu jamaa anavyogawa hela hivyo alafu unakuja na takwimu za elfu kumi per day!!!kwa taarifa yako Edo anatoa laki na nusu kwakila MTU anaye mshika mkono tu kumsalimia,alafu wewe unasema mini bana! Mako umemsingizia Mimi Niko kwenye msafara wake,hara maji ya kunywa tu shida! Jamaa hana kitu kabisa yaani maisha aliyoishi mzee wake ndo anayaaksi!
 
hahaaaa huyu.ni timu lowasa hamna jipya, anamuweka Lowasa nyuma kwa Rushwa mmmmmmh sio rahisi kwa ukweli
 
  • Thanks
Reactions: DSN
Hapo kwa LOWASA umempendelea sana. Yule ndiye kinana wa kumwaga mapesa na anatumia usafiri wa ndege.

Habari yako ina sura za upendeleo
 
  • Thanks
Reactions: DSN
Hoja haina mashiko hususani kwa upande wa kundi linalofuatana na hao watia nia. Wasipowezeshwa watalala wapi na watakula nini?

Mfano Sumaye nasikia ametuma wawakilishi kanda ya ziwa, unategemea wasafiri kwa nauli zao na wakalale hotelini kwa pesa zao bila kuwezeshwa na Sumayi?
 
suzan lemahapo kwa LOWASA nina mashaka napo.............. shilingi elfu tano?
na ndege private anayotumia je?
 
Last edited by a moderator:
  • Thanks
Reactions: DSN
Hiyo ni BEI ELEKEZI YA CCM? Hiki chama ni majanga jamani! Uwiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii
 
Suzan "Bashe" Lema akiwa kazini, asipoandika hivi atakula wapi? babu alipe 10000 kwa siku?
 
Ni kufuru iliyopitiliza inayoonyeshwa na baadhi ya wagombea watia nia ya kuutaka urais ambapo wanatumia fedha kupita kiasi katika zoezi la kusaka wadhamini huko mikoani.

Kwa wale wagombea ambao ni viongozi wa kiserikali wamekuwa wakitumia rasilimali za kiserikali kama vile magari, ndege, basi pamoja na madereva wa serikali katika mbio za urais.
.............................................................. Itaendelea .....

Jambo baya ktk haya uliyoyaeleza ni kutumia mali za kiofisi ktk kuhangaikia mambo binafsi ya kisiasa. Kuhusu hizo pesa mimi nawaomba waendelee tu. Wananchi wambieni wachukuwe bila kinyongo maana tulishajua Escrow ndo ilikuwa maana yake hiyo! Ni vigumu kuwazuia wananchi kuchukuwa pesa wakati tunajua hata anayezitoa kaiba.


Tuwaelimishe wananchi pesa wachukuwe lakini kupiga kura waamue wao wenyewe, kwa siri yao wenyewe! Ukishaona refa hakemei wanaovunja sheria za mchezo, nawe kanyaga tu!
 
KABISA ni team Lowasa. MTU ANAYETUMIA HELA ZA KUFURU NI LOWASA. Halafu hao matajiri wake anaopenda kuwataja kwamba wanamsaidia yeye atawalipa nini? HATUKUBALI KUUZA NCHI YETU TUKIONA. NEVER HAPPEN!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
  • Thanks
Reactions: DSN
Wakuu naona mnaendeleza siasa za kizushi mimi niko Lumumba sijakwenda Unguja wala Pemba na hao mnaowaita masalia ya chadema hakuna anaelipwa na Mwigulu posho wala mshahara acheni uzushi na siasa za maji taka.
 
Mtoa mada ni TEAM LOWASSA.Anajaribu kutuonyesha kwamba fisadi Lowassa anatoa rushwa ndogo kuliko mafisadi wenzake na kwamba hatumii fedha nyingi kama wenzake. Kwa nini hakutaja private jet anayotumia na pesa wanazolipwa maelfu ya watu wa kumshangilia?

Kwa mfano Dada Juliana Shonza yuko nyumbani kwao Mbozi Mlowo na harakati zake za kuutaka Ubunge wa viti maalum mkoa wa Mbeya.Acheni siasa nyepesi.
 
KABISA ni team Lowasa. MTU ANAYETUMIA HELA ZA KUFURU NI LOWASA. Halafu hao matajiri wake anaopenda kuwataja kwamba wanamsaidia yeye atawalipa nini? HATUKUBALI KUUZA NCHI YETU TUKIONA. NEVER HAPPEN!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Naona Team Lowasa wanajitekenya kisha wanacheka Wenyewe.
 
  • Thanks
Reactions: DSN
Back
Top Bottom