Wageni ‘vihiyo’ watumika hotelini Dar | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wageni ‘vihiyo’ watumika hotelini Dar

Discussion in 'Nafasi za Kazi na Tenda' started by ndiyomkuusana, Sep 24, 2012.

 1. ndiyomkuusana

  ndiyomkuusana JF-Expert Member

  #1
  Sep 24, 2012
  Joined: Aug 2, 2012
  Messages: 627
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 45
  [TABLE]
  [TR]
  [TD="bgcolor: #ffffff"][TABLE]
  [TR]
  [TD]na Edson Kamukara


  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [TD="width: 140, bgcolor: #ffffff"][​IMG] [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD][TABLE]
  [TR]
  [TD]BAADHI ya wafanyakazi wa kigeni kutoka mataifa mbalimbali hususan barani Asia, wameendelea kuajiriwa katika nyadhifa tofauti za juu kwenye hoteli kubwa za kitalii jijini Dar es Salaam wakati hawana ujuzi wa taaluma ya kazi husika.
  Uchunguzi wa Tanzania Daima umebaini kuwa wafanyakazi hao huletwa na ndugu zao wenye madaraka makubwa katika hoteli hizo bila kujali taaluma zao, na wakati mwingine hufanya kazi za kawaida ambazo kisheria zinatakiwa kufanywa na wafanyakazi wazawa.
  Gazeti hili limenasa orodha ya wafanyakazi wa moja ya hoteli kubwa maarufu zilizopo eneo la Kunduchi, yenye wafanyakazi wa kigeni 29 ambao takriban wote ni raia wa India ukiacha watendaji wachache wa juu kabisa.
  Taarifa kutoka ndani ya hoteli hiyo ni kwamba wafanyakazi hao wengi wao hawana ujuzi kabisa na kazi walizoajiriwa kufanya, hivyo baada ya kuingia hufundishwa na wale wachache wazawa ambao hata hivyo hawathaminiwi.
  Ili kukwepa mkono wa sheria za nchi kuhusu wageni kufanya kazi zinazoweza kufanywa na Watanzania wazalendo, baadhi ya wafanyakazi hao wasio na ujuzi (vihiyo), wamekuwa wakitumia majina tofauti hotelini hapo badala ya yale yaliyoko kwenye pasi zao za kusafiria au nyaraka za Idara ya Uhamiaji.
  Baadhi ya wafanyakazi wazalendo wa hotelini hapo, walilidokeza gazeti hili kuwa mchezo huo umekuwa ukifanywa kwa ushirikiano wa watendaji wasio waaminifu ndani ya Idara ya Uhamiaji na wamiliki wa hoteli hiyo.
  “Tumelalamika sana juu ya mchezo huu unaotunyima ajira, maana kazi wanazofanya hawana ujuzi nazo, tunawafundisha sisi, lakini wanaajiriwa wao na kulipana mishahara mikubwa; watu wa Uhamiaji tukiwaambia wanakuja wanazungumza na wamiliki mambo yanaishia hapo na kama haitoshi wanatutaja majina kwa wamiliki tunafukuzwa kazi kwa kutoa siri za ofisi,” alisema mmoja wa wafanyakazi hao wazalendo.
  Katika orodha ya wafanyakazi wa kigeni 29 wa hoteli hiyo ambayo gazeti hili lina nakala yake, kazi zilizoainishwa nyingi ni za kawaida kama ufundi, udaktari, umeneja stoo, uhasibu na nyinginezo ambazo kimsingi wako Watanzania wengi wenye ujuzi wa kuzifanya.
  “Yaani hapa ukiingia humu ndani utashangaa kuona watu wanavyoweza kwenda kwao kuleta ndugu, wake, waume na jamaa zao na kuwajaza kazini kwenye vitengo nyeti wakati hawafanyi lolote. Tunaye Store Controller, lakini ukisoma kibali chake cha kazi anatambulishwa kama Operation Manager,” kilisema chanzo chetu.
  Vile vile katika orodha hiyo yuko mfanyakazi mmoja anatajwa kama injinia, lakini wafanyakazi wenzake wanasema hajui lolote, hatua inayowafanya kuiomba serikali kuingilia kati kuzikagua hoteli hizo ili kubaini kama wahusika wanafanya kazi kwa mujibu wa sheria za nchi na vibali vyao.
  Nafasi za juu ambazo zinashikiliwa na wafanyakazi wazalendo hotelini hapo ni mbili, moja ikiwa ya Meneja Rasilimali Watu, ambaye hata hivyo anatajwa kutokuwa na kauli kwani wafanyakazi wazalendo wanapomlalamikia hawapi majibu ya kujitosheleza akidai kuwa yeye analetewa wafanyakazi na wakubwa zake. Mwingine mwenye wadhifa mkubwa ni Meneja Ulinzi.
  Juhudi za kuwatafuta wasemaji wa hoteli hiyo, waziri mwenye dhamana na kazi pamoja na Idara ya Uhamiaji zinaendelea kutokana na jana kuwa siku ya wikiendi na hivyo watendaji hao kuwa mapumzikoni.


  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. salosalo

  salosalo JF-Expert Member

  #2
  Sep 25, 2012
  Joined: Jun 7, 2012
  Messages: 579
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 45
  Bado nafasi ya raisi, akishindwa Obama malekani atakuja kuwa rais wa TZ. Kwanza sitaki kuamini kuwa mpaka leo kunanafasi za uongozi katika kampuni yoyote ambayo haiwezi kusimamiwa na mzawa. Hayo mambo ya kutokuwa na uwezo wa kuongoza ua kufanya kazi kama hizo ilikuwa zamani. Tusipoangalia tutakuwa tunafanya kazi ya kutatua matatizo ya ukosefu wa ajira kwa nchi za wenzetu kama India huku tukikuza upande wetu. Serikali simamieni sheria za nchi sawasawa. Hiki kitu mnachokiandaa (ukosefu wa ajira) madhara yake ni makubwa kwa watanzania wote mkiwemo viongozi. Ohoo!!!
   
 3. m

  magesa77 Senior Member

  #3
  Sep 25, 2012
  Joined: May 22, 2011
  Messages: 118
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Kikubwa zaidi kinachosikitisha ni kuona Meneja Rasilimali Watu anashindwa kuwatetea watanzania wenzake, anachoangalia ni yeye mshahara wake pamoja na kuwakumbatia wahindi wasio hata na vibali vya kuishi na kufanya kazi nchini. Kunduchi beach hoteli ni sehemu iliyojaa unyanyasaji wa hali ya juu kwa wafanyakazi wazawa. Pale Wet n wild water park ambayo ni sehemu ya hoteli, wafanyakaxzi wanalipwa mshahara wa elfu 80 kwa mwezi, hakuna overtime wala nini. Mhindi anaweza kumtusi na kumpiga mzawa asichukuliwe hatua yeyote. HOUR solution wanaotumiwa ktk mashauri ya kinidhamu wanafanya kuwanyanyasa wazawa bila kujali sheria za ajira za nchi hii, wanachoangalia ni pesa yao wanayolipwa kama consultants tu na si sheria zinasemaje, wamegeuka vibaraka wa kuwafurahisha wahindi na si kuangalia taaluma yao. Ama kwa hakika mtu msomi anayejua sheria za ajira na asiye na njaa sana, hawezi kufanya kazi ktk mazingira yale. Natoa angalizo kwa wanaotafuta ajira kuwa Kunduchi Beach hoteli si sehemu ya kufanya kazi. Jamani uhamiaji amkeni na fuatilia hao wahindi na Wakenya wasio na vibali hapo Kunduchi, pia wizara ya kazi na ajira ipamulike.
   
Loading...