Wageni tutaruhusiwa kununua nyumba NHC Bongo

Wageni tutaruhusiwa kununua nyumba NHC Bongo

MK254

JF-Expert Member
Joined
May 11, 2013
Posts
33,570
Reaction score
53,584
Hivi karibuni Tanzania itaruhusu wageni kununua hizo nyumba, wageni wengi kutokea nchi zingine za Afrika huwa tunajionea jinsi Wahindi wameruhusiwa kuzinunua kwa wingi wakati tunawekwa pembeni. Binafsi mkiruhusu hii lazima nitakua na nyumba huko, ni muhimu sana kuwa na nyumba kadhaa kwenye nchi tofauti tofauti.

JK: Foreigners to own property

A review of laws on fixed assets ownership in the country could soon see foreigners enabled to buy apartments in structures constructed by the National Housing Corporation, President Jakaya Kikwete revealed on Wednesday.

He said the government was considering reviewing the existing laws, particularly those that bar foreigners from making such purchases.The move could see the market for the NHC houses expand.

President Kikwete said many other countries including South Africa and the US allow foreigners to buy houses, a practice he said has greatly contributed to the growth of their economies."Restricting foreigners from buying NHC apartments is a matter we need to reconsider. We should not delay our progress," he said. The President was speaking at a function to lay the foundation stone for NHC's Morocco Square project in the city.

He also laid the foundation stone for another NHC Mindu Housing project in Upanga.The Morocco Square project worth Sh150 billion, that started mid-last year and is expected to end in December 2017, will consist of four towers built on one foundation.

Two of the towers will house office units, one hotel and the other will be for residential and commercial purposes.The project is mainly financed by a CRDB Bank loan to the tune of about Sh100 billion.

The residential tower will consist of 22 storeys with 100 apartments; the 20 and 17 storey towers will be for offices and shops and the 13 storey structure will house a hotel.

Welcoming the President, NHC Board of Directors' chairperson Zakhia Meghji, cited the law that restricts NHC to sell its houses to foreigners as one of the major obstacles.

She said the NHC is currently building many houses that are supposed to be sold but the internal market was limited.

"In order to expand the reach, we request that the law be reviewed to allow even Tanzanians in the Diaspora and foreigners to buy the houses," she appealed.

Souce: The Citizen
 
Samahani.... Hivi Watanzania wanaruhusiwa kununua nyumba huko Kenya?!
 
Samahani.. Hivi Watanzania wanaruhusiwa kununua nyumba huko Kenya?!

Watakujibu humu maana wapo Watanzania wengi wenye majengo na kadhalika Nairobi. Hata jirani wangu hapa Kasarani, Mtanzania mwenye asilia ya Kichagga amejenga jengo nzuri la kupendeza lenye orofa kadhaa.
Kwetu sisi hatubagui na ndio maana uchumi wetu umeendelea hivi, Wasudan, Wasomali n.k. wanajenga sana.

Hii dunia ukibagua, hatimaye utachoka na kuzidi kuwa na nchi kubwa yenye raslimali lakini umaskini unakumaliza. Akija mgeni kwa uwoga uwoga anakwapua na kugeuza maana haumpi nafasi ya kuwekeza.
 
NHC was suppose to build low cost houses for majority of tanzanians that was the mission for its establishemnt ila kwa sababu ya ufisadi wana jenga nyumba kifisadi mwisho wa cku ili ziuzike kwa faida zinakua bei kubwa na maana nzima ya kuwauzia watanzania wenye kipato cha chini inakua ngumu.

hii habari imechanganya mambo mawili ambayo hayapaswi kuchanganywa, kwanza suala la wagen kununua au kumiliki nyumba bongo ni separate na NHC kuuza nyumba ni separate, serikali inaweza ku review sheria kuwaruhusu wagen kumiliki nyumba no problem ila si sawa kwa serikali kuibadili NHC kua shirika la kuuza nyumba kwa yoyote.

maana nzima ya shirika la umma kuuza low cost housing kwa wananchi wake inapoteaje? kama serikali inataka NHC ibadili mission basi libinafsishwe lisiwe mali ya umma alafu liendelee na shughuli zake kama mashirika mengine ya binafsi.

ila as long as kama litabaki kua shirika la umma mission ya kujenga makaz ya bei ya chini kwa majority ya watanzania inatakiwa ibaki hivyo cha kushughulikiwa ni ufisadi ndani ya shirika hili ktk ujenz wa hizi nyumba alafu mwisho wa cku nyumba zinakua haziuziki haiwezekan nyumba ya mil 40 mtaan unaweza ijenga kwa mil 10 ndo maana watanzania wanazisusia kukwepa hizo fedheha ndo wanakuja na upuuz huuu!!!
 
NHC wameamua kuwa mabepari wanajenga nyumba ambazo wateja hawawezi zinunua,wasipokuwa makini zitawadodea
 
Hapa wadau naona kuna shida zinazoikumba NHC sio ya bongo tu bali za nchi mengine afrika mashariki. Nilipokuwa nasomea shahada yangu roomate wangu architect aliniambia kuwa hakuna demokrasia kwenye swala la nyumba miongoni mwa nchi mengi afrika. chukua mfano hapa kenya.

NHC ya hapa yamejenga mitaa kama Nyayo ambalo ni la kifahari kwa gharama kubwa mno yeneye inahitaji miaka zaidi ya 15-20 kuurudisha mtaji. lakini wamesahau kuwajengea pia wasio na uwezo mdogo ilhali utafiti umeonyesha una manufaa zaidi na hata kurudisha mtaji kwa muda mdogo zaidi - 7-10.

Iliyobaki kama changamoto sasa ni low cost(but decent) housing ambazo manufaa zake zime fanyiwa utafiti wa kutosha. Au kwa njia ingine kuna investment opportunity kwenye low cost housing kwa wanaopenda kuingia huu sekta.
 
Hivi karibuni Tanzania itaruhusu wageni kununua hizo nyumba, wageni wengi kutokea ncchi zingine za Afrika huwa tunajionea jinsi Wahindi wameruhusiwa kuzinunua kwa wingi wakati tunawekwa pembeni. Binafsi mkiruhusu hii lazima nitakua na nyumba huko, ni muhimu sana kuwa na nyumba kadhaa kwenye nchi tofauti tofauti.

Aliekuambia Hao wahindi sio citizen ni nani? Wahindi wengi wamezaliwa hapa wengi wao waliozaliwa Tabora .
 
Aliekuambia Hao wahindi sio citizen ni nani? Wahindi wengi wamezaliwa hapa wengi wao waliozaliwa Tabora .

Huwa nashangaa sana kuona Wahindi wanaodai wazawa, ila Kiswahili cha kuunganisha, ina maana huwa hawajimix na Waswahili ama vipi. Nimekutana pia na wanao ongea Kiswahili poa kabisa, lakini hao wa kuunga unga huwa siwaelewi kabisaaaa...
 
Hapa wadau naona kuna shida zinazoikumba NHC sio ya bongo tu bali za nchi mengine afrika mashariki. Nilipokuwa nasomea shahada yangu roomate wangu architect aliniambia kuwa hakuna demokrasia kwenye swala la nyumba miongoni mwa nchi mengi afrika. chukua mfano hapa kenya.

NHC ya hapa yamejenga mitaa kama Nyayo ambalo ni la kifahari kwa gharama kubwa mno yeneye inahitaji miaka zaidi ya 15-20 kuurudisha mtaji. lakini wamesahau kuwajengea pia wasio na uwezo mdogo ilhali utafiti umeonyesha una manufaa zaidi na hata kurudisha mtaji kwa muda mdogo zaidi - 7-10.

Iliyobaki kama changamoto sasa ni low cost(but decent) housing ambazo manufaa zake zime fanyiwa utafiti wa kutosha. Au kwa njia ingine kuna investment opportunity kwenye low cost housing kwa wanaopenda kuingia huu sekta.

Suluhisho ni vijana kununua nyumba zinazojengwa nje ya mji, NHC Bongo nimewapa hongera kwa kujenga nyumba nyingi mikoani. Hadi hata Kigoma, japo bei yake si ya Waswahili wa kawaida aisei.
 
MK254,

Hivi huwezi kuleta habari yoyote bila kuwa personal?

Mali za Watanzania hata kama wataamua kugeuza mabanda ya kuku..Wewe kinachokukera ni nini?

Hivi wewe una moral-position ipi ya kutuita sisi Wabaguzi?

Haki ya nani omba nisje ijua nyumba yako utakayonunua hapa.
 
Last edited by a moderator:

Mimi nitakuwahi nikijua yako.
 
NHC wameamua kuwa mabepari wanajenga nyumba ambazo wateja hawawezi zinunua,wasipokuwa makini zitawadodea
Ndio maana kila siku nasema Serikali yetu imewapa Wakurugenzi wa mashirika haya ya UMMA uhuru uliyo pitiliza mipaka,wanafanya wapendalo kwa kushirikiana na baadhi ya Board members/Chairmen kujingiza kwenye projects ambazo has nothing 2 do na uhanzisaji wa Mashirika hayo,NHC kwa mfano inajingiza kukopa ma trillion ya fedha kutoka Mabenki kwa ajili ya kujenga ma shopping malls wakati hawana uhakika kama wataweza kurudisha mkopo na interest juu ndani ya agreed timeframe tusije tukajikuta n ujanja wa Mabeki
 
NHC wameamua kuwa mabepari wanajenga nyumba ambazo wateja hawawezi zinunua,wasipokuwa makini zitawadodea

Ndio maana kila siku nasema Serikali yetu imewapa Wakurugenzi wa mashirika haya ya UMMA uhuru uliyo pitiliza mipaka,wanafanya wapendalo kwa kushirikiana na baadhi ya Board members/Chairmen kujingiza kwenye projects ambazo has nothing 2 do na uhanzisaji wa Mashirika hayo.

NHC kwa mfano inajingiza kukopa ma trillion ya fedha kutoka Mabenki kwa ajili ya kujenga ma shopping malls wakati hawana uhakika kama wataweza kurudisha mkopo na interest juu ndani ya agreed timeframe tusije tukajikuta ni long term strategy za Mabenki ya kuja kuli posses majengo na plots kama Shirika litashindwa kurudisha mkopo kwa bahati mbaya au by design.

Serikali inayokuja inapaswa kuangalia upya spending spree ya NHC hasa katika ujengaji wa maghorofa ya kifahari ambayo hayawezi kununuliwa na wananchi/raia wa kawaida - wakumbuke NHC ilihanzishwa kwa madhumuni ya kujenga nyumba zenye bei nafuu na kuwahuzia wananchi au kuwapangisha, again kwa kodi nafuu, siku hizi naona madhumuni hayo hayapewi kipa umbele hata kidogo wanajenga nyumba chache za kawaida kwenye baadhi ya mikoa tu na kuwahuzia wananchi kwa bei mbaya
 
NHC wameamua kuwa mabepari wanajenga nyumba ambazo wateja hawawezi zinunua,wasipokuwa makini zitawadodea

Ndio maana kila siku nasema Serikali yetu imewapa Wakurugenzi wa mashirika haya ya UMMA uhuru uliyo pitiliza mipaka,wanafanya wapendalo kwa kushirikiana na baadhi ya Board members/Chairmen kujingiza kwenye projects ambazo has nothing 2 do na uhanzisaji wa Mashirika hayo.

NHC kwa mfano inajingiza kukopa ma trillion ya fedha kutoka Mabenki kwa ajili ya kujenga ma shopping malls wakati hawana uhakika kama wataweza kurudisha mkopo na interest juu ndani ya agreed timeframe tusije tukajikuta ni long term strategy za Mabenki ya kuja kuli posses majengo na plots kama Shirika litashindwa kurudisha mkopo kwa bahati mbaya au by design.

Serikali inayokuja inapaswa kuangalia upya spending spree ya NHC hasa katika ujengaji wa maghorofa ya kifahari ambayo hayawezi kununuliwa na wananchi/raia wa kawaida - wakumbuke NHC ilihanzishwa kwa madhumuni ya kujenga nyumba zenye bei nafuu na kuwahuzia wananchi au kuwapangisha, again kwa kodi nafuu.

Siku hizi naona madhumuni hayo hayapewi kipa umbele hata kidogo wanajenga nyumba chache za kawaida kwenye baadhi ya mikoa na kuwahuzia wananchi/wafanyakazi kwa bei mbaya wanatumia mwanya huo 4 publicity stunts tu - Kazi ya kujenga majumba ya gharama kubwa wawahachie NSSF na mashirika mengine ya mifuko ya jamii.

Nimalizie kwa kusema kwamba JK amepewa ushauri mbaya kuhusu kuwahuzia wageni nyumba za NHC,binafsi naona wageni wawe wapangaji tu, ukisema wahuziwe nyumba unakuwa umewapa passport ya kumiliki plots(aridhi)sasa sheria yetu inasemaje kuhusu wageni kumiliki aridhi kupitia back door.

JK hawezi kuwa amezungumzia suala hili bila ya kuwa amedanganywa na wahusika - sijui kama alikumbuka kwamba ukimuhuzia mgeni nyumba automatically unakuwa unamuhuzia vile vile plot(aridhi) ilipojengwa nyumba!!
 
Hii business model ya NHC sielewi kabisa,kama walitaka kusaidia wananchi kupata nyumba za bei nafuu nafikiri wange operate kama financial institution yenye kutoa mikopo nafuu na udhamini kwa wananchi waweze kununua nyumba,sasa wao ndio builders,wauzaji,wakopaji etc wanachofanya is too much and will never work
 
MK254,

Hivi huwezi kuleta habari yoyote bila kuwa personal?

Mali za Watanzania hata kama wataamua kugeuza mabanda ya kuku..Wewe kinachokukera ni nini?

Hivi wewe una moral-position ipi ya kutuita sisi Wabaguzi?

Haki ya nani omba nisje ijua nyumba yako utakayonunua hapa.
Heshima yako mkuu Malcom,Tanzania imepakana na zaidi ya nchi nane hivi, je umewahi kuona raia wa Zambia,Msumbiji,Uganda,Burundi,DRC nk wakifatilia fatilia magazeti yetu, social networks zetu and what have you, kati ya majirani zetu tajwa hapo juu kuna nchi hata moja ambayo anajitia kimbele mbele kwa kujaribu kutupatia somo 'how to run our Country' jibu ni hapana. Sasa swali je, kwa nini baadhi ya Wakenya wanakosa usingizi masaa yote wanafikiria kitu kimoja tu, nacho ni: How 2 get even na TANZANIA!!
 
Last edited by a moderator:
Hii business model ya NHC sielewi kabisa,kama walitaka kusaidia wananchi kupata nyumba za bei nafuu nafikiri wange operate kama financial institution yenye kutoa mikopo nafuu na udhamini kwa wananchi waweze kununua nyumba,sasa wao ndio builders,wauzaji,wakopaji etc wanachofanya is too much and will never work
Well said mkuu KOBA,kuna kitu hakijakaa sawa hapa - Serikali inayokuja inapaswa kuchukua drastic measure the soonest kabla shirika halijangia kwenye matatizo, naya sema haza kwa nia njema tu
 
Hili swala tena sio la choice bali lishakuwa la lazima kutokana na majukumu yanayo waelemea na strategy ya awali walioichagua wenyewe mbovu na kukopa bila ya mpango.

Imagine hiyo project ya Morroco inagharama ya sh billioni 150 pamoja na hapo watakuwa wanakaribia deni la billioni miatatu wamejenga nini wakiulizwa chenye kuonekana.

Kwa mujibu wa watu wengi gharama ya kujenga a decent house ni 40 million shillings, ina maana sh billioni 150 ya Morroco project pekee ambayo aitoi hata nyumba mia ingeweza kuweka idadi ya nyumba si chini ya 3750 Dar-Es-Salaam pekee as detached houses or with a mixture of semi detached and high rising the number of units could easily top 4000 in additional to lowering their costs of buildings due to economies of scale.

How many local contractors would have benefited from such a strategy, how many jobs would have been created in such a dispersed investment in the region, how much would the local cement industry benefited the wider economic benefits are immense in addition quick sales which might give a chance to develop other properties quickly elsewhere.

Huyu jamaa sijui wamemuwokotea wapi yaani ovyo kweli kweli ndio maana wachina wameingia mitini washamuona bogus he is just not qualified for that public role, wao wamejenga mpaka kuna ghost cities for less huko kwao huyu anashindwa kujenga hata kwa demands tatizo la watanzania ni kujifanya watu wa viwango sijui matawi wakati wengi ovyo tu hizi fikra potovu inabidi zizibitiwe kwakweli.
 
Back
Top Bottom