Waganga wa Kienyeji na Matangazo yao

Waganga wa Kienyeji na Matangazo yao

Kaizer

Platinum Member
Joined
Sep 16, 2008
Posts
25,338
Reaction score
17,875
Wana MMU salaam!

leo limenijia wazo hebu tujadili, kuhusun waganga wa kienyeji
na mataangazo yao na sehemu hasa maarufu, wanakotokea

uzoefu unaonyesha kwamba matangazo mengi yanaonyesha waganga maarufu kutoka maeneo ya Sumbawanga, Tanga, Mwanza, Mombasa, Bagamoyo na maeneo mengine kama hayo (sina hakika na watani zangu wanyakyusa)

Halafu huwa wanaagua/tibu/wezesha mambo ya: Kumwita mpenzi aliye mbali, magonjwa sugu, UTAJIRI baada ya siku 3, nk......

sasa kwa nchi hii kuna sehemu kuna mafanikio/maendeleo lakini sijawahi kusikia waganga wa jadi kutoka huko....mfano sijawahi kusikia "mganga maarufu kutoka Moshi/kilimanjaro/arusha/Bukoba

sasa kwa nini huko wanakotoka kusiwe na maendeleo kama wanavyohubiri au ndio ile Nabii hakubaliki kwao? yaani sielewi elewi

Kwa nini hakuna uwiano wa kimaendeleo kati ya wanakotoka waganga wengi na maeneo mengine yasiyo maarufu kwa uganga?

Hebu namba Mtambuzi MziziMkavu The Boss Kaunga snowhite Mtoto halali na hela Asprin lara 1 miss strong Baba V watu8 mwallu Heaven on Earth amu mnidadavulie, kama mlishawahi kwenda kwao, waganga hao wanatokea wapi??
 
Last edited by a moderator:
Huku Mwanza mbona siwaoni wanaojiita wa kutoka Mwanza?

Huku nawaona wakutoka sumbawanga
Sikumbuki kama nimewaona wa kutoka Tanga
Wa Mombasa niliwahi kuwaona lakini ni mara chache sana
Nadhani wa Sumbawanga ni wengi sana!
 
hahaha....lakini mkuu Eiyer kwa nini Sumbawanga hakuna maendeleo ki ivyo?
 
Last edited by a moderator:
hahaha....lakini mkuu Eiyer kwa nini Sumbawanga hakuna maendeleo ki ivyo?

Tumelelewa kuuogopa sana uchawi
Na maeneo yanayosadikiwa kuwa na huo uchawi wanadai hawataki maendeleo
Kuna ushahidi wa watu kufa wanapojenga ka nyumba ka udongo kisha kukaezeka na bati
Hicho kinawafanya watu kuogopa kufanya maendeleo maeneo hayo

Lakini zaidi sana watu wakisikia mahali fulani kuna wachawi hupakimbia labda wale 'magwiji"

Sumbawanga napo pamekumbwa na hii kitu
Panasifika sana kwa uchawi
Japokuwa huwa nasikia jina lenyewe Sumbawanga lina maana hasi kuhusiana na uchawi
Wanadai Sumbawanga maana yake ni "tupa uchawi"

Pia inawezekana hao waganga wanaodai kutoka sumbawanga ni uongo tu
Watu wanawassifia waganga wa huko kuwa ni wazuri
Hivyo hata mganga feki nae atasema anatokea huko

Huenda sio kweli kuna waganga wengi wanaotokea sumbawanga!
 
sijawahi kwenda kwa mganga
lakini ninawasikia sana wakijinadi,na hua naona hakuna lolote zaidi ya kuwatia watu hofu na kuwafanya wawategemee wao
hata mafanikio wanayoyatangaza mbona wao hawana? au ndo mganga hajigangi?

ni upuuzi tu
 
010.JPG
 
Mkuu Eiyer hapo bold kuna kaukweli, majuzi nilikuwa Bariadi wenyewe wanapaita kwa Wanyantuzu....hao ni watu mahiri kwa biashara na utaftuaji kwa jamii ya wasukuma..ajabu ni kwamba pale kwao hawajawekeza sana ukilinganisha na walivyowekeza Kahama na Mwanza....sababu kuu ndio hiyo kwamba wanaogopa wakiwekeza kwao wataondolewa chap chap sana

Sasa basi na huko Sumbawanga tena.....hizi nguvu hizi nilidhani zingewasaidia hata kusoma (sipati picha unafahamu mtihani wote)....au kufanya mambo mengine ya kimaendeleo..kwa nini uchawi wa hao watu hauleti maendeleo ila vifo na visasi tu? fikiria idadi ya vikongwe wanaouwawa kwa sababu ya kuhisiwa wachawi!

wachagga wanasifikia kwa maendeleo...hali kadhalika maeneo ya Bukoba.....sijasikia 'mganga maarufu' kutoka huko....
 
Last edited by a moderator:
sijawahi kwenda kwa mganga
lakini ninawasikia sana wakijinadi,na hua naona hakuna lolote zaidi ya kuwatia watu hofu na kuwafanya wawategemee wao
hata mafanikio wanayoyatangaza mbona wao hawana? au ndo mganga hajigangi?

ni upuuzi tu

Sasa wewe hujawahi kwenda huko
Umejuaje kama ni upuuzi?
 
Mkuu Eiyer hapo bold kuna kaukweli, majuzi nilikuwa Bariadi wenyewe wanapaita kwa Wanyantuzu....hao ni watu mahiri kwa biashara na utaftuaji kwa jamii ya wasukuma..ajabu ni kwamba pale kwao hawajawekeza sana ukilinganisha na walivyowekeza Kahama na Mwanza....sababu kuu ndio hiyo kwamba wanaogopa wakiwekeza kwao wataondolewa chap chap sana
Mkuu hili ni tatizo kubwa sana na limewafanya watu wa maeneo hayo kuishia kuwa na maisha ya ajabu sana
Lakini siku wakiamua kuachana na hii kitu watafumbuka macho
Sasa basi na huko Sumbawanga tena.....hizi nguvu hizi nilidhani zingewasaidia hata kusoma (sipati picha unafahamu mtihani wote)....au kufanya mambo mengine ya kimaendeleo..kwa nini uchawi wa hao watu hauleti maendeleo ila vifo na visasi tu? fikiria idadi ya vikongwe wanaouwawa kwa sababu ya kuhisiwa wachawi!
Mkuu uchawi unakuwa na madhara kwakuwa mapokeo yake ni hasi mara nyingi
Lakini pia wale waliokuwa nao mwanzo ndio waliharibu dhimanzima ya hizo nguvu

Uchawi ni nguvu kama nguvu zingine
Lakini watu huzitumia kwenye mazingira hasi zaidi kuliko chanya
Mtu anazitumia hizo nguvu kumdhuru mtoto wa jirani aliye fauli mtihani vizuri kwasababu tu ya wivu

Mtu anaamua kumdhuru jirani yake kwasababu amejenga nyumba
Hii ni aina mbaya sana ya kufikiri
Hatukufundishwa kukubaliana na matokeo na hatimae kujikwamua kwa juhudi
Tunaona kuwamaliza wale wanaoonesha juhudi na kuwa na aina moja ya maendeleo ni sawa bila kuiona athari tunayoisababisha

Watu hawajajifunza kujikubali kabisa
wachagga wanasifikia kwa maendeleo...hali kadhalika maeneo ya Bukoba.....sijasikia 'mganga maarufu' kutoka huko....
Hii inatokana na mapokeo ya wazee wa mwanzo
Lakini nahofia siku hizi hata haya maeneo yatamezwa na hii kadhia!
 
Mkuu Eiyer hapo bold kuna kaukweli, majuzi nilikuwa Bariadi wenyewe wanapaita kwa Wanyantuzu....hao ni watu mahiri kwa biashara na utaftuaji kwa jamii ya wasukuma..ajabu ni kwamba pale kwao hawajawekeza sana ukilinganisha na walivyowekeza Kahama na Mwanza....sababu kuu ndio hiyo kwamba wanaogopa wakiwekeza kwao wataondolewa chap chap sana

Sasa basi na huko Sumbawanga tena.....hizi nguvu hizi nilidhani zingewasaidia hata kusoma (sipati picha unafahamu mtihani wote)....au kufanya mambo mengine ya kimaendeleo..kwa nini uchawi wa hao watu hauleti maendeleo ila vifo na visasi tu? fikiria idadi ya vikongwe wanaouwawa kwa sababu ya kuhisiwa wachawi!

wachagga wanasifikia kwa maendeleo...hali kadhalika maeneo ya Bukoba.....sijasikia 'mganga maarufu' kutoka huko....

Ulishawahi kujiuliza hao waganga wateja wao ni kina nani siku hizi?
Hata Wahindi na Waaarabu wanapenda sana mambo hayo lakini huwezi kumkuta mganga Upanga, Ilala au Kisutu!!

Homework.................!
 
Labda amejua kuwa ni upuuzi from the first place so hakuna sababu ya kwenda huko

Unajua kuna watu tunasema hivyo kwa sababu hatujui
Kuna jamaa wengi sana nawajua na wao wamenithibitishia kuwa mafanikio walionayo ni kutokana na waganga

Sasa ukikuta mtu anasema "mbona waganga hawana maendeleo"
Kisha anamalizia "upuuzi mtupu"
Napata wasiwasi kama anajua alichokiandika!
 
Kuna wengine siku hizi wanaweka mabango yenye tangazo "Pete ya utajiri, pesa za majini, ndoa haraka"...........Kubwa kuliko "Kujiunga na freemason" na hapo uikute hajakosea spelling.............Friimasoni!!
 
Back
Top Bottom