Wafugaji wananyanyasika sana katika nchi hii!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wafugaji wananyanyasika sana katika nchi hii!!!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Nali, Feb 14, 2012.

 1. N

  Nali JF-Expert Member

  #1
  Feb 14, 2012
  Joined: Mar 31, 2010
  Messages: 826
  Likes Received: 248
  Trophy Points: 60
  Wana JF,

  Imekua desturi sana serikali hii ya Magamba kuwahamisha wafugaji katika maeneo yao na kuwapatia wawekezaji. Kibaya zaidi wana waambia wafugaji hao waende walikotoka, Je Mwekezaji ndio mzalendo au Mtanzania kuliko mfugaji aliekuwa toka enzi za mababu zetu? Na je huyu mwekezaji yeye katoka wapi? Obvious katoka nje ya nchi!!

  Hii serikali legelege sana, sasa hivi kila kona na vilio na laana kwa serikali hii. Wakati akihutubia Bunge kwa mara ya kwanza 2005 huyu Kikwete alisema; "Wafugaji wabadilike maana ng'ombe anakonda na mfugaji anakonda pia".

  My take: Kwani wafugaji wameanza kufuga leo? Huo ni mfumo wao wa maisha toka zamani, hawakuanza leo.Na huyu kikwete akiwa Bagamoyo na akiwa mdogo naye alichunga tena ng'ombe wa kimasai na alikuwa akinywa na kula mazao yatokanayo mifugo na huo ufugaji anaouita leo "holela". Yaani watu wanasahau walikotoka!!! Unatupa mbachao kwa msala upitao???!!!

  Anyway; inauma sana maana hawa wafugaji ni raia halisi wa nchi hii, kikubwa wawekewe tu utaratibu mzuri wa kufuga ikiwa ni pamoja na miundo mbinu katika ufugaji wao.
   
 2. Job K

  Job K JF-Expert Member

  #2
  Feb 14, 2012
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 6,865
  Likes Received: 2,807
  Trophy Points: 280
  Serikali hii tumba..f sana! Ukimsikiliza Punda akiongea ufugaji haki ya nani unapata hasira sana! Wanajidai na wingi wa mifugo huku hawatusaidii bwana, eti nchi yetu ni ya tatu kwa wingi wa mifugo Afrika. Unafukuza wafugaji unataka waende wapi? Ila na sisi wafugaji tumezidi kuwakumbatia hawa maggambas. Tukisikia ugeni wa kiongozi eti tunajitolea mboga! She.nzi zetu acha tuwe wakimbizi kwenye nchi yetu!
   
 3. M

  MIGNON JF-Expert Member

  #3
  Feb 14, 2012
  Joined: Nov 23, 2009
  Messages: 2,587
  Likes Received: 1,563
  Trophy Points: 280
  Nisingependa nionekane kama ni mfuasi wa ubaguzi wa aina yoyote ile ila nashauri uchukue machache nitakayoeleza na uyafanyie kazi,naamini mtizamo wako utabadilika.
  Ufugaji usiozingatia eneo na idadi ya mifugo una madhara makubwa kwa mazingira na nenda katika wilaya ya kilosa na utayaona haya.Ardhi iliyokuwa nzuri ya tambarare inayopata mvua sasa hata nyasi hazioti.
  Jamii ya wafugaji ina ukwasi mkubwa ukilinganisha na wakulima wadogo wadogo na ili kuthibitisha hili katika wilaya ya kilosa pamoja na kuwa sio wilaya ya wafugaji kwa upande wa kusini lakini kwa kutumia pesa tayari wafugaji wamepewa vijiji vilivyopimwa zaidi ya vitatu.Wakulima wanazidi kubanwa.Niliwahi kuandika hapa kuwa kesi ya mfugaji na mkulima ni mtaji kwa polisi na mahakama.
  Wafugaji wanatakiwa waishukuru sana serikali hii kwani kwa kuwa inalea rushwa wafugaji wataendelea kunyanyasa wakulima,watasambaa kila mahali na pia wataangamiza maeneo mazuri ya kilimo.
   
 4. j

  jigoku JF-Expert Member

  #4
  Feb 14, 2012
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 2,347
  Likes Received: 80
  Trophy Points: 145
  Hili jambo ni nyeti sana na ni jambo linagusa maisha ya watu au jamii kubwa isipokuwa kwa kuwa watu wengi hata wasomi jambo hili limekuwa nje ya uwezo wao bila kujali viwango vya elimu zao basi ndio maaana hadi leo jamii za wafungaji wamekuwa ni wakimbizi ndani ya nchi yao,wamekuwa ni wahamiaji haramu ndani ya nchi yao,yaani hakuna tofauti na wasomali au wahabeshi wanao kamatwa wakisafirishwa kwenda Afrika kusini,wafugaji hawa wamekuwa eti ni wavamizi ndani ya nchi yao.
  Hivi inkweli?au umagharibi nao umetutawala kiasi kwamba tumekuwa watumwa wa kifikra?hata kwa wasomi tena wengine wamesoma kilimo na mifugo lakini bado wameshindwa kumaliza tatitzo la wafugaji wa nchi hii?mwisho wa siku na vishule shule vyao wanavitumia kusema wafugaji wanaharibu mazingira,je ni kweli hayo?okay na je msaada au suluhu kwa hilo ni kuwafukuza na kukosa haki ndani ya nchi yao?hivi je kule kwenye mbuga za wanyama kama Serengeti,Ngorongoro na kwingineko hao wanyama hawaharibu mazingira?mbona nao wako kwa makundi mengi tu na pengine zaidi ya ng'ombe wafugwao na wasukuma,wamasai na wamang'ati?,hivi kweli inakuingia akili mtu ana ng'ombe elfu 2 hadi 6 unampa eneo la kufugia la kilometa kumi za mraba?na wakati mwingine wanapewa jirani na vijiji?hivi kunatafiti gani ilishawahi kufanyika iliyolenga kumaliza tatizo la wafugaji?na je leo tunapowaambia wafuge kibiashara wanaelewa nini maana yake?unapowambia wavune mazao yanayotokana na mifugo yao wanaelewa maana yake ni nini?je tunajua viwango vyao vya uelewa?je elimu zao tunazijua kiwango chake?lakini je maeneo ya ardhi ndani ya TZ ambayo yako wazi tu huko maporini ambayo pia yanafaa kwa ufugaji yanatumika sawasawa?
  Iweje leo tunakuwa malimbukeni wa kudai eti wanaharibu mazingira wakati hao ni wafugaji wenye makundi makubwa ya ng'ombe halafu unawapa eneo dogo la kuchungia?unategemea mazingira yatasalimika?je nani alishafanya kazi ya kuwatambua wafugaji hawa kwa kuzingatia idadi ya mifugo wanayofuga na wakatafutiwa maeneo ya kuchunga kwa kuzingatia wingi wa mifugo kwa kila mfuganji?
  Je ni kwa nini mtoto wa mkulima aligawa eneo la karibu hakari laki na ushee hiv ama zaidi kwa huyu muwekezaji kule Mpanda mzungu kutoka Amerika,kitu ambacho Mbunge Arfi kupitia CDM amepeleka hoja binafsi na imezimwa na Spika?ni vipi angeligawa kwa wafugaji?maana wafugaji hawa ili wasiharibu mazingira anahitaji eneo kubwa kulingana na idadi ya mifugo yake.
  Au mnataka tu-import nyama?leo tunafug wenyewe lakini kilo ni 6000 vipi tukianza ku-import?na je viwanda vya kusindika hata mazao viko wapi?
  Achani bana,huo ni ubaguzi wa wazi dhidi ya wafugaji,najua jinsi Mtoto wa mkulima alivyokuwa akifanya kampeni ya kichochezi dhidi ya wasukuma tangu zamani walipoanza kuhamia mikoa ya kwao,na wapo wanaweza kuthibitisha juu ya hilo.
   
 5. N

  Nyumisi JF-Expert Member

  #5
  Feb 15, 2012
  Joined: Nov 10, 2010
  Messages: 451
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 60
  Nakubaliana kabisa na bwana jigoku hapo juu. Kuna watu wengine serikalini, NGOs na hata wananchi wamekuwa wakilaumu wafugaji kuwa ni waharibifu wa mazingira. Lakini wameshindwa kuelewa mchango wa kutoka enzi na enzi wa wafugaji hawa wa asili katika kuwalisha watanzania nyama na maziwa ambavyo ni chanzo cha protini muhimu mwilini mwa binadamu. Hivi mlishawahi kujiuliza kama hawa wafugaji wa asili wasingekuwepo nyama kwenye mabucha ingekuwa shilingi ngapi? kwa sasa inafika 9000/= kwa kilo Dar.
  Kwa kutambua mchango wao mkubwa, badala ya kuwanyanyasa wafugaji wa asili ni vema serikali iwamilikishe maeneo makubwa ya ufugaji ambayo yatazingatia idadi ya mifugo yao. Pia wajengewe miundombinu kama malambo ya kunyweshea mifugo yao, majosho, madawa, n.k. Tukiendelea kuwaona wafugaji wa asili kama waharibifu na kama lengo ni kutaka watoweke kabisa, vitu kama nyama na maziwa watakuwa wanatumia vigogo tu ambao wanauwezo wa kununua supermarket nyama na maziwa yaliyoagizwa toka nje. Makabwela tutapigwa na utapiamlo hadi tutajuta. Sasa nyie endeleeni kugawa ardhi kwa wakoloni mamboleo mnaowaita wawekezaji na kuwanyanyasa wazalendo, hata kama hamtakuwepo watoto na wajukuu zenu watapata shida kubwa huko mbeleni.
   
 6. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #6
  Feb 15, 2012
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,785
  Likes Received: 2,397
  Trophy Points: 280
  wanawapiga vita wafugaji ili mhindi wa export trading aendelee kuuza mbolea ya chumvi chumvi samadi isiwepo!
   
Loading...