Wafugaji wa Samaki jijini Arusha kunufaika na mikopo ya riba nafuu

Waziri2025

Senior Member
Sep 2, 2019
148
379
Halmashauri ya jiji la Arusha imewataka wafugaji wa Samaki katika jiji hilo kujiunga Kwenye vikundi vidogo vya ujasiriamali ili kunufaika na mikopo ya riba nafuu inayotolewa na halmashauri hiyo waweze kuboresha shughuli zao na kufanya uzalishaji wenye tija.

Rai hiyo ilitolewa na mkuu wa idara ya mifugo na uvuvi wa jiji la Arusha Onesmo Mandike aliwataka Wafanyabiashara na wadau wa Samaki jijini Arusha ulioandaliwa na chama Cha Wafanyabiashara Tanzania(TCCIA) Kwa kushirikiana na shirika la Trias .

Mandike alisema sekta ya ufugaji wa Samaki ni sekta muhimu na ikisimamiwa vema inafaida kubwa Kwa kuongeza kipato na kuimarisha Afya za mlaji.


Mandike ambaye alimwakilisha Mkurugenzi wa jiji la Arusha katika mkutano huo,alisema kuwa jiji la bado kuna idadi ndogo ya wafugaji wa samaki licha ya kuwepo kwa mfugaji mkubwa qnayefuga kisasa na kuzalisha vifaranga vingi vya Samaki .


Naye afisa Samaki wa Jiji ,Maria Kalinga alisema kaika jiji la Arusha Kuna wafugaji wa Samaki wapatao 98 ikilinganisha na mwaka 2011 ambapo wafugaji walikuwa watatu.


Alisema ongezeko hilo limetokana na Serikali kuajiri maafisa Samaki katika halmashauri zake ambao wamekuwa wakitoa Elimu na kufanya utafiti wa Samaki na hivyo kupelekea ufugaji kuimarika.


Aidha alisema mkakati wa kuongeza wazalishaji wa Samaki ni pamoja na kutoa elimu Kwa wazalishaji na kupata vifaranga Bora na chakula ikiwemo mkakati wa Jiji hilo Kuanzisha kituo cha uzalishaji wa vifaranga.


Kwa upande wake mwendeshaji wa chama Cha Wafanyabiashara TCCIA Mkoa wa Arusha,Charles Makoi Kwa kushirikiana na shirika la Trias alisema wamelenga kukuza zao la Samaki katika jiji la Arusha na kwamba hadi Sasa wameweza kuwafikia wafugaji wa Samaki wapatao130 Kwa kuwapatia mafunzo.


Alisema tangu mwaka 2019 TCCIA na Trias imekuwa ikitoa mafunzo Kwa wafugaji wa Samaki ili kuwasaidia wafugaji jinsia ya kuinua zao la samaki katika jiji la Arusha.

Mwisho
 
Back
Top Bottom