Kufuga mifugo mbalimbali ilianza toka zamani za kale. Binadamu alipewa uwezo wa kuwamiliki wanyama na kuwatumia anatakavyo kulingana na mahitaji yake. Mfano kulima, kupata nyama, maziwa, ngozi kwa matumizi mambalimbali, huongeza pato la taifa, ajira. Imezoeleka kwamba binadamu hasa wa kitanzania hufuga au humiliki wanyama kama mbuzi, ng'ombe, kondoo, punda na wengine wengi.
Tanzania inasifika dunia kwamba ni ya tatu afrika kwa kuwa na mifugo mengi. Tanzania kama nchi isingepata hii sifa kimataifa ingekua sio raia wake ndo wanaofuga. Serikali kama serikali isingeweza kufuga kiwango ambayo wafugaji binafi wanafanya. Vile sidhani hata kama serikali inayo mradi inayoiendesha kama serikali. Pamoja na hayo nchi yetu imekua ikifaidi yatokanayo kwa mifugo ndani na nje ya nchi kwa sababu raia wake wanafuga.
Pamoja na faida mfugaji anayoyapata kwa kufuga pia jamii nzima hufaidi kutoka kwa mifugo yake. Mfano katika jamii ya kitanzania hakuna mji unaweza ukaenda usikute bucher maana wanakula nyama kutoka kwa wafugaji wanaofuga kijijini, pia mijini kuna maziwa madukani iwe ya unga au ya packit au ya kupima inapatikana kutoka kwa mifugo husika, Vile vile watu wanafaa viatu na mavazi mengine yatokanayo na ngozi ya mifugo na faida nyingine ambayo jamii kwa ujumula inapata moja kwamoja kutoka kwa mifugo ambayo wao hawafugi.
Hata hivo serikali inafaidi mambo mengi kutoka kwa mifugo ikiwemo kupatikana kwa ajira kwa vijana aidha kwa kuwa wachungi wa mifugo au kufanya biashara ya mifugo au kwa kufanya biashara ya vitu yatokanayo kwa mifugo. Mfano biashara ya bucher, kuuza maziwa, ngozi n.k.
Pato la taifa huuongezeka kulingana na mapato yatokanayo na mifugo. Serikali inapata fedha za kigeni kutoka kwa mifgo mfano, kila siku mifugo aina ya mbuzi na kondoo wanapakiwa kwenye meli na kuwasafirisha nje ya nchi. Bila shaka serikali inafaidi mambo mengi kupitia kwa mifugo ikiwemo kukusanya kodi.
Lakini hawa wafugaji wanaotaabika kuifaidisha jamii ya kitanzania kwa kutoa huduma nzuri kwa watanzania kulingana na faida ya mifugo niliyotaja hapo juu hawajapewa kipau mbele ya maeneo ya kuwekeza. Wao wameoneka wanaharibu mazingira na kuoneka wanyang'anyi wa maeneo.
Hii imejidhihirisha wazi kwani kila siku kwenye vyombo vya habari ukisikia mapigano. Ni lazima iwe ni baina ya wafugaji na wakulima. Wafugaji mara nyingi ndo wanaonekana wakorofi, wameingilia maeneo ya wakulima, wameingilia sehemu ya mwekezaji, wameingiliea sehemu ya hifadhi.
Mfano mapigano iliyotokea huko INVOMERO, KITETO, LOLIONDO, NGORONGORO na sehumu zingine ilikua ni baina ya wafugaji wa jamii ya kimasai na wakulima au na mwekezaji. Watu wengi walipoteza maisha wakiwemo watoto na wakinamama, Watu walipoteza mali na hata makazi kwani kuna mengine yaliteketezwa kwa moto.
Hawa watu wameshindwa kupata sehemu za kudumu za kufuga. Hawa watu wamekua wakimbizi kila uchao katika nchi yao huru, kila siku kuna mapigano baina wafugaji na jamii inayo wazunguka. Wafugaji wanashindwa sasa kukaa na kufaidi mifugo yao na kuwasomesha watoto wao. Wafugaji wamekua ni kuhamahama kwani hawana sehemu maalum zilizotengwa kwa ajili ya ufugaji wao.
Uwekezaji wa wafugaji ni wa manufaa sana katika nchi yoyote ile. Wafugaji hunufaisha watu wengi hata wale ambao hawafugi pamoja na serikali yao.
Sasa kwa kizazi kinachokuja ya wafugaji vile wanaona kizazi iliyowatangulia wasulubiwa kila uchao wao watakua na hamu ya kufuga? Na kama hapana maanayake kama taifa tutakosa yatokanayo kwa mifugo. Badala ya kuimarisha uchumu wa taifa itakua inaporomoka kwani itatulazimu tuwe tunawaleta mifugo kutoka nje ya nchi kwa ajili ya matumizi ya kawaida mfano nyama na mengine mengi.
Serikali yetu haina budi kuangalia kwa upya namna ya kuboresha ufugaji. Hii itawezeka kwa kutengeneza sera nzuri na kutenga maeneo maalumu kwa ajili ya ufugaji. Serikali haina budi kuboresha miundo mindu ya wafugaji kama mabwawa, majosho n.k.
karibuni kwa mjadala!!!!