Akihutubia mkutano wa kampeni, Rais Samia Suluhu Hassan alisisitiza umuhimu wa kuinua kilimo na ufugaji, akisema kuwa Serikali imepanga kupitia Ilani kuongeza maeneo ya ufugaji hadi hekta 6,000,000 pamoja na kuboresha huduma muhimu kama maji, majosho, malisho na ugani, hatua itakayosaidia kuongeza tija na kuhakikisha usalama wa chakula. Aliongeza kuwa mpango huu utatamaliza kabisa migogoro ya wakulima na wafugaji nchini, huku pia ukichangia kuimarisha kipato cha wakulima na wafugaji na kukuza uchumi wa vijijini.