Wafuasi wa CCM na CHADEMA wapi wanaojitambua sawasawa?

Wafuasi wa CCM na CHADEMA wapi wanaojitambua sawasawa?

Jemmie

JF-Expert Member
Joined
Mar 6, 2018
Posts
216
Reaction score
285
#Ukitazama kwa undani na umakini kati ya makundi haya mawili, yaani wafuasi wa CCM na CHADEMA, utabaini kwa urahisi tu kwamba, wafuasi wa CCM wako vizuri zaidi ya wale wa Chadema.

#Kuna mifano michache inayoweza kudhihirisha hili:

***Wafuasi wa Chadema hawaelewi kwa undani mfumo na falsafa ya chama chao, yaani CHADEMA. Wengi wa wafuasi na wanachama wa Chadema hufuata mkumbo tu kwa kuangalia matakwa ya kiongozi hasa mwenyekiti, bila kuwa na ufahamu wa ndani wa chama. CCM ina mfumo, misingi na miiko inayoeleweka vizuri kwa wanachama, viongozi na wafuasi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM). Viongozi wa Chadema wanaweza kubadilisha gia wakati wowote kwa maslahi yao binafsi, na wafuasi au wanachama wake wasiweze kuhoji chochote. Mfano ni mwaka 2015 ambapo mwenyekiti alibadili mgombea urais dakika za mwisho bila kufuata utaratibu, au mwenyekiti anapoamua kuhamisha matumizi ya ruzuku za chama kwenda kwenye AKAUNTI binafsi ya familia, nk. Yote haya yanafanyika wafuasi na wanachama wa Chadema wakiwepo lakini hawawezi kumuuliza mwenyekiti wao. Ni sawa na kutotambua nafasi yao ndani ya Chadema. Wapowapo tu na hawajielewi.
***Wafuasi wa Chadema wao ni wafia viongozi, wakati wale wa CCM ni wafia chama. Hii ina maana kuwa wanachama wengi wa Chadema wapo kulinda maslahi binafsi ya viongozi wao, wakati CCM wao wanaangalia maslahi ya chama na taifa kwa ujumla. Wakati CCM wakibadilisha viongozi wa chama kila baada ya miaka 10 kwa njia ya kidemokrasia, Chadema wao wanang'angana na mwenyekiti mmoja tu miaka zaidi ya 25 kwa hofu kwamba mwenyekiti aliyepo akiachia madaraka eti Chadema itakufa. Hii inamaanisha kwamba, misingi ya CCM imejengwa kichama zaidi, wakati ile ya Chadema iko mikononi mwa mtu mmoja. Mwenyekiti wa CHADEMA akiamua kujiuzulu Leo, chama kitakufa kwa sababu kinamtegemea mtu mmoja na kwamba hakina mfumo endelevu wa kichama.
***Wakati viongozi, wanachama na wafuasi wa CCM wana malengo ya kuleta maendeleo ya nchi na wananchi wake, viongozi na wafuasi wa Chadema wao ni kupinga tu kila kitu hata kama ni cha maendeleo. Kuanzia kwa kiongozi hadi wafuasi wa Chadema, wao ni kupinga tu kila kitu. Na hii inaonyesha kuwa wafuasi wa Chadema hawajitambui (wengine huwaita misukule au nyumbu), kwa sababu wao hufuata na kusikiliza lolote wanaloambiwa na viongozi wao hata kama halina maslahi kwao na kwa taifa kwa ujumla. Mfano: waliambiwa Lowassa na Nyalandu ni mafisadi wakashangilia sana, siku chache baadae wakaambiwa tena hao sio mafisadi, ni madume ya mbegu, wanaChadema wakapiga makofi na kushangilia. Wangekuwa wanajitambua wangewahoji viongozi wao inakuwaje watuhumiwa wa ufisadi Leo hii wamekuwa vidume vyao vya mbegu?
 
Kuanzia leo, naona usifananishe CCM na Saccos ya Mbowe.. Plz plz..!!
 
Wafuasi wa CCM hawajawahi kumdekia Barabara Hata Baba wa Taifa
 
Mkuu unalinganisha mlima kilimanjaro (CCM) na Kichuguu CHADEMA? 🙄
 
Ccm (Jiwe, Dab na yule wa bungeni) najua utakuwa umepata jibu


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Ilani ilitaka ya chama ilipendekeza raisi akiingia madarakani wasichana wanaopata mimba wakishajifungua waendelee na masomo.

Lakini imekuwa vice versa. Na mengi kati ya hayo ila tunaambiana tu Chukua Chako Mapema kinaendeshwa na mfumo ..

Mfumo PERIOD!!

Vyama vyote vya siasa hapa Tanzania havina mifumo imara ya kujieimamia vyenyewe kwa sababu haviwezi kumuwajibisha mwenyekiti wao si CCM wala CDM wala ACT-WAZALENDO.

Wanachama wote ni wafia tumbo tu hakuna mtu anayepambana kwa ajili ya masilahi ya chama au taifa lake.

Sitokaa nipige kura mpaka nakufa kwa vyama vilivyopo hapa Tanzania.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom