Wafanyakazi wa wahindi


Invisible,
Hili la kuhama kutoka kwa mhindi mmoja kwenda kwa mhindi mwingine linategemea na sababu zenyewe. Kama mtu ni "potential" kwa mhindi huwa wanawa-treat vizuri na wako tayari kukupa mshahara mzuri kabisa. Kuna rafiki yangu mmoja alikuwa anafanyakazi kwa Mansoor Daya Chemicals pale Nyerere road kama mkemia, alikuwa analipwa mshahara mara tano ya wenzie wenye elimu sawa. Kwa mhindi kila mtu ana kitabu chake cha kusaini mshahara hakuna kujua mshahara wa mwenzio. Kwahiyo mtu anaweza kuhama kutoka kwa mhindi mmoja kwa kwa mwingine baada ya kuahidiwa maslahi mazuri na mazingira mazuri ya kazi.

Tatizo kubwa liko kwa watu wenye elimu ndogo wanaofanya kazi ambazo si professional, hawa ndo wananyanyasika zaidi.
 
Wahindi nafikiri wana vijizadi vidogovidogo kama unga, mchele sukari n.k hivyo watu hao hupumbazika na vijizawadi kutokana na hali ngumu ya maisha "MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA" ni ndoto kwao
 

Hapana mkuu siyo mimi, mimi niliondoka DAIKIN mwaka 97 sasa sijui huyo ni nani na wala siko TAA nadhai huyo ni mhandisi mwingine.

Kwa hoja yako kwamba watu wanarudi kwa wahindi hilo ni sawa na sababu yake ni kwambawahindi ndiyo wana access ya mikopo na hivyo kuweza kuwa rahisi kwao kuanzishakampuni. Sasa kwa hali hiyo ndo waajiri wakubwa, ukiacha wabongo wachache wenye makampuni yao.

Kwa hiyo kinacho sumbua ni kwamba "vijana wetu watakimbilia wapi?"
 

Mkuu invisible wala hakuna wasi wasi namjibu tu kwa sababu ametaka kujua. Kuhusu kutoka kwa mhindi huyu na kuhamia kwa mwingine, hili naweza kulielezea kuwa wahindi no waajiri wakubwa wa pili baada ya serikali kwa hiyo vijana wetu hawana pa kukimbilia.
 
Na balaa kubwa ni hawa vijana na wazee wanokuwa wanafanya kazi kwa wahindi bila elimu na wanajua akija mwenye eliu wao huenda mkate ukakosekana, sasa kasheshe inaanza hapo mnaanza kupigana juju wenyewe kwa wenyewe....mifano ninayo lukuki.
 

Tumaini 'Shiwji" ni proudly tanzanian tena wa kilosa....labda hiyo pia imechangia kuwa vile alivyo.

nakubaliana nawe kuwa zambi ya ubaguzi wanayo tena sana kwa kweli kweli.... (christians and muslims much better i concur)
 
Kuhusu kutoka kwa mhindi huyu na kuhamia kwa mwingine, hili naweza kulielezea kuwa wahindi no waajiri wakubwa wa pili baada ya serikali kwa hiyo vijana wetu hawana pa kukimbilia.

huo ndo ukweli...
 
Mimi naona kwamba wafanyakazi hawa huhama kutoka kwa mhindi mmoja na kwenda kwingine kutokana na sababu mbalimbali.

Moja huenda kuna mikataba mifupimifupi "temporary employment" au short "term contracts" au "call on and off basis" kati ya wahindi hawa na wafanyakazi. Kutokana na mazingira haya huenda wafanyakazi hawa wanakuwa na waajiri zaidi ya mmoja iwe kwenye ajira kubwa ama nyumbani. Mathalani utaona wafanyakazi hawa wakiwapeleka watoto shule na kuwafuata mchana na kuwarudisha nyumbani.

Sababu ingine inawea kuwa ni kutokana na muda wa biashara tuchukulie mfano wa madukani, kwamba wahindi wenyewe wana kazi nyinginyingi kwa hio huitaji mtu wa kuwasaidia moaka saan nane au kumi tu basi, na baada ya hapo wewe huitajiki tena kwa hio unaweza kwenda kwa mhindi mwingine kuanzia saa kumi na mbili ili ukamwagilie bustani.

Tatu ni kwamba hali ya uchumi inapelekea wafanyakzi hawa wawe na uhakika "guarantee" ingawa ni fwedha ndogo sana kuhakikisha kwamba wanashikilia ajira hizo ambazo zinaweza kuwasaidia kujikimu wao na familia zao.

Mwisho ni kutokana na "opportunity to choose and to conceal" mambo kadha wa kadha ambayo wahindi wanayo kama vile fwedha, chakula, na mengine ambapo kutakuwa hakuna ushahidi kwamba kulikuwa na hujuma. Kwa mfano ukifanya kazi kwa mhindi utajua jinsi ya kucheza na "stock" iwe maboksi ya biscuits na itakuwa rahisi ku-smuggle nje kwa ajili ya kuuza tena ili nawe upate faida.

Hayo ni maoni yangu tu.
 
Kwanini wafanyakazi wa wahindi wanakaa muda mrefu kwenye kazi zao pamoja na manyanyaso na mishahara midogo wanayolipwa? na akiacha kazi kwa mhindi mmoja anahamia kwa mhindi mwingine mpaka anazeekea kwa wahindi, kuna nini tusichokijua?

Kwanza Jiulize swali almost 80% ya makampuni ni ya wahindi??? why???na hao wahindi ndio wanao waajiri waaafrika wengi na ndiko huko huko TRA wanapochukulia kodi na hatuoni manufaaa yake. Na hayo makampuni kila kukicha yanaingiza faida mbaya usipimie,

Ilani mbovu za CCM zinawafanya wahindi waendelee kuwakandamiza watanzania wanyonge na kuwatumikisha kazi kwa saaanaaaaa na kuwapa kipato kidogo miaka 4 still unapokea 150000/=Tsh kweli na ukija tizama hata huko NSSF wamekuandikia wanakulipa 70,000/=Tsh, Na kuna makampuni mengine huwalipa mishahara mikubwa 500000/=Tsh lakini nenda NSSF umeandikishwa unalipwa 150000/=Tsh jamani yani hata hiyo NSSF hawajui kazi yao PCCB mwende huko mkawachunguze kuna utumbo huko .
TRA,NSSF,PPF,TANESCO,IDARA ZA MAJI MIKOA YOTE,BIMA, ndio yako mstari wa mbele kumkandamiza mtanzania wa kipato cha chini
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…