Wafanyakazi wa wahindi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wafanyakazi wa wahindi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Annina, Nov 28, 2009.

 1. Annina

  Annina JF-Expert Member

  #1
  Nov 28, 2009
  Joined: Nov 15, 2009
  Messages: 437
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Kwanini wafanyakazi wa wahindi wanakaa muda mrefu kwenye kazi zao pamoja na manyanyaso na mishahara midogo wanayolipwa? na akiacha kazi kwa mhindi mmoja anahamia kwa mhindi mwingine mpaka anazeekea kwa wahindi, kuna nini tusichokijua?
   
 2. rmashauri

  rmashauri JF-Expert Member

  #2
  Nov 28, 2009
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 3,008
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Hii inategemea na mtu. Kuna watu ambao hawana jinsi zaidi ya kuvumilia tu hayo manyanyaso na malipo kidogo ili aweze kupata chochote cha kumwezesha kuishi mjini.

  Sababu nyingine ni kwamba hawa wafanyakazi wa wahindi huwa wanawaibia sana wahindi wakati mwingine wakishirikiana na wateja. Mfano waweza kwenda dukani mfanyakazi anaaza kukushawishi achukue mzigo akutolee nje halafu utalipa kidogo mfano bidhaa za sh. 150,000 anaweza kukuomba umpe 70,000 sasa inategemea msimamo wako wewe mteja.

  Nimewahi kushuhudia kwa macho yangu jamaa mmoja aliachiwa kaunta na mhindi kwenye studio moja maarufu sana ya kupiga picha jijini Dar ile kutoka tu huyo bosi wake wa kihindi jamaa akachomoa pesa kwenye ile mashine na kuweka mfukoni mwake haraka haraka.

  Hayo ndo maisha wanayoishi wafanyakazi wa wahindi walio wengi. Ni ya kiwiziwizi tu.
   
 3. A

  AmaniGK JF-Expert Member

  #3
  Nov 28, 2009
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,101
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Ndugu yangu Wahindi ni wajanja na wana akili sana katika kuhakikisha watumishi wao wanadumu katika himaya zao muda mrefu.Katika kuhakikisha mtumishi anakaa nao mpaka utimilifu wa dahari,wamegundua kwamba mishahara tu sio kigezo cha kumfanya mfanyakazi akaa muda mrefu.

  Kwa maana hiyo basi, asilimia kubwa ya hao unaowaona wanatumika kwa wahindi watoto wao wanalipiwa ada ya shule moja kwa moja kutoka kwa hao wahindi,kwa vile basi wafanyakazi wao wameshatengenezewa mazingira ya kuhakikishiwa vitu kama shule chakula na mavazi viipo basi wanakua na woga wa kuhama.Ni hayo tu kwa sasa
   
 4. s

  shabanimzungu Senior Member

  #4
  Nov 28, 2009
  Joined: Jul 7, 2009
  Messages: 182
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  tafadhali, issue hii ni racism..ata waswahili pia wana fanya hivi we read it in newspapaers...........do not accuse the minorities.
   
 5. Tumain

  Tumain JF-Expert Member

  #5
  Nov 28, 2009
  Joined: Jun 28, 2009
  Messages: 3,158
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  mishahara katikati ya mwezi ni sababu ya watu kubaki kila siku kwa wahindi, wahindi hawalipi full salary kwa hiyo kila siku mfanyakazi anajikuta ana hela kidogo au karibuni hatapata fedha..mpaka unazeeka!

  Option chukua risk acha nusu mshahara ili ujikomboe otherwise utabaki maskini...nawafahamu sana hao...wezi wakubwa.
   
 6. Annina

  Annina JF-Expert Member

  #6
  Nov 28, 2009
  Joined: Nov 15, 2009
  Messages: 437
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Pole kama nimekugusa pabaya...
   
 7. Mama Subi

  Mama Subi Member

  #7
  Nov 29, 2009
  Joined: Feb 9, 2008
  Messages: 88
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 15
  Hii ni kasumba ya sisi watu weusi. Walio wengi wetu wanaonaga ni bora kufanya kazi kwa mzungu ama muhindi kuliko kwa weusi wenzetu. Ni slave mentality tu. Very sad indeed!
   
 8. Serendipity

  Serendipity JF-Expert Member

  #8
  Nov 29, 2009
  Joined: Jan 24, 2009
  Messages: 475
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Waindi wengine wana juju kali sana, kushinda za kibongo! hivyo akigundua una faida kwake, anakuchapa juju na huwezi kuwaza kuacha kazi kwake!
   
 9. M

  Magezi JF-Expert Member

  #9
  Nov 29, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  watu ni wazembe tu na kuogopa ku-take risk mimi nimewahi kugombana na wahindi wa pale DAIKIN mwaka 1997 wakanitisha eti watanifukuza nikawaambia mbona wamechelewa sana kunifukuza mpaka nimekuwa na pesa za kuniwezesha kutafuta kazi nyingine?

  Basi siku iliyofuata nikaambiwa hakuna kwenda site, nami nakakaa pale, wakaona wala hata sibabaiki ndo wakanipa visenti vya kuniachisha nikasema asante mmenipa hela ya bia, basi ndo nikaachana nao na the next month nikajiunga UDSM for bachelor degree.

  Kwa hiyo tatizo la watanzania wengi wananoteseka kwa wahindi ni wasiokuwa na pa kwenda i.e. elimu yao duni, lakini pia wengine ni waoga kuchukua maamuzi hasa ambao tayari wana familia zinawategemea.

  Nashauri tu kwamba kwa wale wenye elimu nzuri wasiogope ku-take risk na kuacha kazi kwani mhindi anakubana kiasi kwamba huna muda wa kutafuta kazi mahali pengine.

  Halafu mimi nilikuwa na utaratibu kwamba lazima kila mwezi nikose kazini siku moja ili niweze kupata muda wa kutafuta kazi sehemu nyingine, make bila hivo utafia kwa mhindi huku wenzio wenye elimu kama wewe wanapeta na vigali mtaani.
   
 10. Annina

  Annina JF-Expert Member

  #10
  Nov 29, 2009
  Joined: Nov 15, 2009
  Messages: 437
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Hili limezungumzwa mara nyingi, lakini cha kushangaza hata wale wanaoacha kazi kwa mhindi next time utakuta yupo kwa mhindi mwingine. Mifano ni mingi... sasa sijui ni mazoea au?

  Nafaham jamaa mmoja wa DAIKIN aliacha kazi kwa makasheshe na kwenda mlimani for engineering sasa yupo TAA - ndio wewe?
   
 11. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #11
  Nov 29, 2009
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,091
  Likes Received: 238
  Trophy Points: 160
  Haha, sasa unaanza kuua bendi... Mkuu Magezi usijibu hilo hapa, malizaneni PM.

  Mi nadhani maoni ya wengi almost yanafanana, lakini bado la kuhama kutoka kwa mhindi mmoja kwenda kwa mwingine sijaona anayelijibu :).

  Very interesting kusoma maoni ya watu. Mkuu Wande, hivi wanaopiga juju ni wahindi au wafanyakazi wenyewe kwa wenyewe? LoL
   
 12. s

  shabanimzungu Senior Member

  #12
  Nov 29, 2009
  Joined: Jul 7, 2009
  Messages: 182
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Annina...this is an issue of everyday..why wahindis are being stereotyped? I notice in Tanzania wahindis are always looked on the side of "mirijas" but let me tell you frankly, this issue needs a careful study.We have seen child labour amongst our own african brothers and small girls exploited for sex by their employers! pid pittance salaries and so so..............so this is a social problem no need to accuse wahindis.We are living in different era ..let us build our nation and be proud of it..Exploitation of any kind is oppressive be it African..wahindi or a Mzungu who is on a misssion of peopdophile in Tanzania.
   
 13. s

  shabanimzungu Senior Member

  #13
  Nov 29, 2009
  Joined: Jul 7, 2009
  Messages: 182
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Unemployment conditions are worse for women than for men. From July 10 to 23, 1999, TAMWA conducted an outreach programme in Tanzania's six regions that were identified as catchment areas of domestic workers. The programme found that women workers faced harassment, sexual abuse and unwanted pregnancies, denial of wages, and battery. Girl children domestic workers were exposed to exploitation, discrimination, and dehumanisation through working long hours and earning low wages. Not only the head of the household, but also relatives and children bossed around these girl children domestic workers.

  TAMWA was involved in a programme to repatriate girl children labourers from Dar es Salaam City to their respective home villages. By June 2000, some 512 girl children labourers had been repatriated.

  The programme involved Kiponzelo, Tanangozi, Ilula, Izazi, and Migori villages in the southern district of Iringa. The main objectives of the outreach were to prevent recruitment of girl children domestic workers, raise awareness of the adverse effects of child labour among potential girl children domestic workers, and change policies and the law to protect and promote development opportunities for girl children.
   
 14. Annina

  Annina JF-Expert Member

  #14
  Nov 29, 2009
  Joined: Nov 15, 2009
  Messages: 437
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Shabanimzungu,
  nakubaliana na wewe kwamba kuna matatizo mengi yanayohusiana na ajira kuanzia kwenye public mpaka private sector ndio maana pamoja na tafiti mbalimbali pia kuna vyama vinavyojaribu kupigania haki za wafanyakazi.

  Interest yangu ilikuwa ni juu ya "utayari" wa baadhi yetu kufanyakazi kwa mhindi katika mazingira magumu pengine kuliko anayoweza kuyapata kwa mwajiri mwingine - na ikitokea ameacha kwa mhindi mmoja anahamia kwa mhindi mwingine... hapa ndipo lilipo swali langu -kunani?

  Hakuna hidden agenda ya racism, wala usifike mbali na kuamsha hisia za watu. Labda umewahi kujiuliza kwanini wahindi pamoja na kukaa karne kadhaa na kuwa watanzania lakini hawajichanganyi na jamii ya kitanzania? uhusiano wa mhindi na watanzania wengine upo kwenye ajira, au uwe mteja katika biashara zao... vinginevyo wana shule zao, hospitali zao, makazi yao, nyumba zao za ibada na mpaka makaburi yao! tofauti na wazungu kwa mfano ambao huo wanajichanganya na wakati mwingine kuoa/kuolewa na mweusi -sina mfano wa hili kwa wahindi! (sikutaka tujadili hili)

  Naomba nieleweke, sina chuki wala ubaguzi wa rangi...nimeuliza out of curiosity which I believe its not a crime!

  Mniwie radhi niliowakwaza
   
 15. Jayfour_King

  Jayfour_King JF-Expert Member

  #15
  Nov 29, 2009
  Joined: Nov 15, 2009
  Messages: 1,142
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Mimi nadhani hapa suala la msingi ni aina ya kazi unayofanya na sifa ulizonazo, na pia tatizo sio kufanya kazi kwa muhindi suala ni je taaluma unayoiuza hapo inakulipa?

  Huwezi kuwa mfanyakazi wa ndani (houseboy/house girl) ukategemea unaweza kumpiga mkwara bosi na hapa suala sio muhindi hata waswahili mbona tunafanyiana hivyo?

  Mifumo mizima ya ajira ndani ya nchi ina utata na ndio maana hata serikali yetu tukufu kila siku ina ligi na wafanyakazi wa kada mbali mbali, serikali yenyewe ina ubaguzi katika utoaji wa mishahara. Wafanyakazi wanaofanya kazi idara kama TRA, BOT, na taasisi nyingine zilizofumuka enzi ya Mr Clean kama SUMATRA na zingine zina taaluma gani ambazo ni maalum sana kiasi cha kutoangalia watumishi wengine wa serikali kwa usawa.

  Kwa mtazamo wangu wizi unaanzia serikalini huko huko ndiko mambo yalipoanza kushindikana. Na ndio maana walipotangaza kiwango cha mishahara mipya sekta ya mahoteli ilishindikana na hadi sasa wanalipwa kujadiliana kutokana na hali ya soko.
   
 16. macho_mdiliko

  macho_mdiliko JF-Expert Member

  #16
  Nov 29, 2009
  Joined: Mar 10, 2008
  Messages: 6,437
  Likes Received: 2,352
  Trophy Points: 280
  Wahindi wengi ni wabaguzi. Hilo halina ubishi. Haswa kwa Waafrika. Haitoshi tu kusema ni wabuguzi ila ni wabaguzi sana. Si watu wa kuonewa huruma hata kidogo. Mimi nina uzoefu nao. Waafrika hatuna sababu ya kujipenedekeza kwao. Tuwa-treat wanafyotu-treat. Ndio njia pekee ya kuwaonyesha ubaya wa ubaguzi.
   
 17. Tumain

  Tumain JF-Expert Member

  #17
  Nov 29, 2009
  Joined: Jun 28, 2009
  Messages: 3,158
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Call a spade a spade I like it..ni wabaguzi malizia hapo siyo wote...there are good very good indeed hawana ubaguzi hata kidogo mfano. Issa shivji ni mtu mwema na anaishi na waafrika vizuri na wengi wa marafiki zake ni black...

  Kuwa mwangalifu na ku-generalize...hii haiondoi zambi yao ya ubaguzi ni wabaguzi wakubwa sana..hasa wenye dini za kihindi ni balaa..afadhali wale wahindi waislamu na wahindi wakristo wanachanganyika..my observation..
   
 18. Ruge Opinion

  Ruge Opinion JF-Expert Member

  #18
  Nov 30, 2009
  Joined: Mar 22, 2006
  Messages: 1,696
  Likes Received: 306
  Trophy Points: 180
   
 19. LazyDog

  LazyDog JF-Expert Member

  #19
  Nov 30, 2009
  Joined: Apr 10, 2008
  Messages: 2,478
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Pengine ni urahisi wa kupata kazi. Mhindi akijua umewahi kufanya kwa mhindi mwenzie atakupa kazi bila kusita.
  Wahindi wanapenda type fulani ya wafanyakazi wa kupelekwa-pelekwa, wenye kuvumilia kukandamizwa, na vitu vya mfano huo.

  Usisahau kwamba, ujuzi wa wengi wa hawa watu ni "kumtumikia mhindi". Yeye amefuzu kwenye nyanja hii, kwanini aende kutafuta kazi kwa mtu asiye mhindi?
   
 20. Alnadaby

  Alnadaby JF-Expert Member

  #20
  Nov 30, 2009
  Joined: Sep 28, 2006
  Messages: 507
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Wahindi wenye asili ya baniani ndiyo hatari zaidi kwa ubaguzi.Hawabagui waafrika tu hata wahindi wenzao ambao kidogo ni tofauti na wao.Hii inatokana na dini yao na huwezi kuizuia.
  Wamejipangia tabaka zao na wanazifuata kwa umakini.Kwa ujumla ni wabaguzi wa kupindukia.
  Wahindi wasiokuwa Hindu kama huyo Issa Shivji au,kina Mohamed Enterprises ni wale aina ya Wahindi wa Kiislamu ambao mafundisho yanawazuia kubagua watu kwa makabila yao.Pia wale aina ya Goa ambao ni Wakristu nao kiasi wana imani na upendo.

  Na mimi binafsi nimefanya kazi kwa Wahindi wa aina ya Hindu sikukaa sana nao.Nikafanya na Waafrika kwa miaka mitano sikupata matatizo makubwa na nikafanya na Waarabu wenzangu ambao wao na wajomba(Wasukuma) ni karibu sare ila wana matatizo ya elimu ya uendeshaji wa biashara na inakuwa tatizo kwenda nao kwa biashara za kisasa.
   
Loading...