Wafanyakazi wa UDART hawajalipwa mpaka sasa na kutaka kumuona Waziri mkuu

Shark

JF-Expert Member
Jan 25, 2010
29,459
29,153
Jana katika pita pita yangu na kupanda magari ya mwendokasi nlikutana na mfanyakazi mmoja akiwa amesimama na hataki kuhudumia wananchi, Raia wakawa wanataka kumpiga lakn baadhi ya wasamaria wema wakaona kabla ya kumpiga wamuhoji ndo akaongea mpaka watu wote wakatoka na machozi.

Kwanza alisema wao wanalipwa mishahara kidogo sana mpaka hakuna uhusiano kati ya mishahara ya wakubwa na wao mpaka wale wa chini makao makuu.

Pia akasema hua wanapewa mishahara kwa kujuana kwanza wanaanza wao wakubwa kisha madereva ili wasije wakagoma.

Na pia alisema kuna kabila ndo limekua kama miungu watu kwe kampuni hyo. Ilibidi tumsamehe na kumuonea huruma yule mfanyakazi.

WITO kwa wahusika wa Wizara ya Kazi wajaribu kutembelea wafanyakazi ili kujua matatizo yao na sio kukaa ofisini tu.
 
Sasa Waziri Mkuu wamuone kwa lipi..? Kwani kabla ya yeye hakuna wenye kuondoa hiyo kero.!
 
we upo kazini wengine wanajiandaa kufundisha shule za msingi kwa ushauri jiwekee 50,000 kila siku ya mauzo ya tiketi utojutia hiyo kazi...
 
Hakuna kinachonikera kama jibu la"Cards hatuna". Af kama kila sikuwatu wanakosa usafiri,abiria hatulipi? Kwa nini wao wasilipwe? Nimeona wakati mwingine hawana moods za kutoa huduma kumbe ndo hivo!
 
Hii nchi imefikia hatua ndani ya ofisi moja mkolomije analipwa mshahara kwa wakati alafu mzaramo anazungushwa na jasho lake.
 
Hakuna kinachonikera kama jibu la"Cards hatuna". Af kama kila sikuwatu wanakosa usafiri,abiria hatulipi? Kwa nini wao wasilipwe? Nimeona wakati mwingine hawana moods za kutoa huduma kumbe ndo hivo!
Wanachokifanya hua wanawalipa madereva wao ili wasije wakagoma lkn vitengo vingine hakuna kabisa. Imagine ijumaa sikukuu lkn mpk leo bila bila
 
Duuh huu mradi unaendeshwa kiunjaunja inaelekea

yaani jinsi tunavyopata shida asubuhi na jioni alafu bado watu wanasema hawajalipwa mpaka Leo?
 
Kwanini hawalipwi, kwa wanajiendesha kwa hasara?,hilo kabila ni lipi?,Kisena kabila gani?..
 
Si ungetaja hayo yalitokea kituo au eneo gani na kuda pia, ili wakisoma wanaohusika waliangalie hilo. Bila hivyo ni kama umeamua tu kutaka kuchafua serikali, na jinsi unavyoipinga haswaaaaa kwa kuwa upinzani.
 
We sema unataka ujue hayo ili umfukuzishe Kazi kijana wa watu. Wamekua wanaajiri kwa kujuana ili iwe tatizo kwa vijana wa watu kudai maslahi yao. Pia inasemwa wadada wengine wa vituoni wameamua kujirahisisha kwa mabosi ili waweze kuishi kimalkia. Na wakiendelea ntafanya research binafsi na kuwataja wote. Kwa nliyoyaona kwa yule kijana ni kitendo cha kinyama sana.
 
Nna video hapa ya dereva kalewa mwendo kasi kalewa ila naiapload inakataa
 
Nna video hapa ya dereva kalewa mwendo kasi kalewa ila naiapload inakataa
Washachukua hela hao hawaguswi kabisa maana wakigoma tu mkulu atastukia uozo wa ndani na jinsi wanavyotupiga hela zetu
 
Wanachokifanya hua wanawalipa madereva wao ili wasije wakagoma lkn vitengo vingine hakuna kabisa. Imagine ijumaa sikukuu lkn mpk leo bila bila

Siku zote najiulizaga vitu kama hivi.Ni unyanyasaji.Kila siku unaingiza pesa,lakini watu wanaokusaidia huwajali.Af wanahimiza watu wafanye kazi.Toka lini kazi za kujitolea zikanufaisha familia za wafanyakazi?
 
Back
Top Bottom