Wafanyakazi wa TRL wagoma!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wafanyakazi wa TRL wagoma!!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Akili Unazo!, Aug 4, 2009.

 1. Akili Unazo!

  Akili Unazo! JF-Expert Member

  #1
  Aug 4, 2009
  Joined: Feb 18, 2009
  Messages: 2,761
  Likes Received: 2,394
  Trophy Points: 280
  wakuu unajua kuna vitu hata mtu mdogo akiangalia anajua kama kuwa viongozi wetu wa nchi siyo wazalendo aliyekuwa mzalendo alikuwa Julius Kambarage Nyerere,Sokoine na wengine waliotanguli japo na wao walikuwa na mapungufu ila hawa wa sasa hivi wamezidi.

  Hivi kweli hakuna tamko la serikali juu ya huyu mhindi aliyekodishwa kuendesha TRL.?
  Kwa nini wanashindwa kuwachukulia hatua mpaka mkataba wa hiari umeshindwa kusainiwa?

  Yule kiongozi wao aliyesema kuwa mktaba utasainiwa India muafaka wake bado au walikuwa wameenda kujifanya wanafanya mkutano kumbe wanahamisha hela za Tanzania?
   
 2. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #2
  Aug 5, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,132
  Likes Received: 5,571
  Trophy Points: 280
  na Datus Bornface

  WAFANYAKAZI wa Kampuni ya Reli nchini (TRL) jana waligoma kuzungumza na baadhi ya viongozi wa shirika hilo kwa madai kuwa msemaji wao hakuwapo katika mkutano ulioitishwa kujadili mkataba wa hiari unaohusu mkono wa heri.

  Wakizungumza kwa hasira baada ya kumalizika kwa kikao cha viongozi wa wafanyakazi na menejimenti, walisema hawako tayari kusikiliza porojo zozote kutoka kwa viongozi wa kampuni hiyo bila kuwapo kiongozi wao waliyemtaja kwa jina la Silvester Rwegasira.

  Hali hiyo ilitokea baada ya menejimenti ya TRA kutaka kuzungumza na wafanyakazi hao muda mfupi baada ya kumaliza kikao chake na viongozi wa Chama cha Wafanyakazi wa kampuni hiyo (TRAWU).

  "Hatutaki kumuona, aondoke mbele yetu, tutampiga kwa mawe, ameona Katibu wetu Rwegasira hayupo, ndiyo anataka kuongea, hatutaki kumsiliza,'' walipaza sauti kwa hasira.

  Walidai kuwa TRAWU iliitisha mkutano Julai 29 mwaka huu, Ikulu, ambapo menejimenti ya TRL iligoma kuhudhuria.

  "Tuliitisha kikao cha pamoja, lakini aliingia mitini, sasa iweje leo aje, anataka kusema nini, hatutaki tumechoka na porojo zake,'' alisema mmoja wa wafanya kazi, aliyejitambulisha kwa jina la Masindiko Shao.
  Wafanyakazi hao walilieleza gazeti hili kuwa katibu wao ambaye ndiye msemaji wao yuko mkoani Morogoro kikazi na kwamba hana taarifa juu ya kikao hicho.

  Wakati wafanyakazi hao wakikataa kuondoka na menejimenti, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Miundombinu, John Ndunguru, ambaye alikuwa katika ofisi hizo alieleza kushangazwa kwake na hatua hiyo ya wafanyakazi.

  Alisema kuwa lengo la kufika ni kuwatuliza kwani suala lao linafanyiwa kazi, pia uongozi huo kuomba msamaha, lakini anashangaa kukataa kuongea na menejimenti. Wafanyakazi hao walianza mgomo wa kutofanya kazi juzi wakiushinikiza uongozi wa kampuni yao kusaini mkataba wa hiari unaohusu mkono wa heri. Hatua ya mgomo ilifikiwa baada ya viongozi wa TRAWU kuwaambia wafanyakazi hao kuwa TRL wamegoma kusaini mkataba huo unaojumuisha mkataba wa wafanyakazi.
   
Loading...