Kurzweil
JF-Expert Member
- May 25, 2011
- 6,622
- 8,410
Bunge nchini Ujerumani limepiga kura ya kuunga mkono wafanyikazi wa serikali kutovaa vazi la kiislamu linaloficha uso la Niqab wakati wanapokuwa kazini.
Mswada huo sasa utapelekwa katika bunge kuu ili kuidhinishwa. Waziri wa maswala ya ndani Thomas de Maiziere alisema kuwa hatua hiyo imeweka wazi viwango vya uvumilivu miongoni jamii nyengine nchini humo.
Mnamo mwezi Disemba ,chansela wa Ujerumani Angela Merkel alitoa wito wa kupigwa marufuku kwa vazi hilo linalofunika uso linalovaliwa na wanawake kadhaa wa Kiislamu.
Vyama vya mrengo wa kulia vimekuwa vikishinikiza kupigwa marufuku katika maeneo ya ummakama vile nchini Ufaransa.
Zaidi ya wahamiaji milioni moja ,wengi wao wakiwa waislamui kutoka mashariki ya kati wamewasili nchini Ujerumani katika kipindi cha miaka miwili iliopita.
Chanzo: BBC