Inasikitisha sana kwa kweli. Hata transaction ya mpesa ya kulipia kwa wale wenye UDART Card imekufa. Kila ukilipia inakuambia "Samahani Huduma hii haipatikani na hutaweza kufanya miamala kwa sasa. Tafadhali jaribu tena baadae". Tunaomba yeyote anayehusika hebu ingilia kati uokoe hii hali. Mwendokasi ni usafiri mzuri, umetusaidia wengi lakini uendeshaji wake si mzuri.