Wafanyakazi wa Dar susieni mikutano ya Kikwete | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wafanyakazi wa Dar susieni mikutano ya Kikwete

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Magezi, May 24, 2010.

 1. M

  Magezi JF-Expert Member

  #1
  May 24, 2010
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Ni siku chache tu zimepita Rais kikwete amewabeza wafanyakazi na kutolea mifanoya mbayuwayu.

  Sasa anajifanya kutembelea Dar es Salaam, najua atajifanya kuongea na wafanyakazi ktk maeneo yenu sasa ndiyo wakati wa kumuonyesha kuwa hamkupendezwa na kauli zake za kejeli.

  Mwacheni aongee na atakaokuja nao kwenye msafara tuone kama yeye ataona raha.
   
 2. M

  Magezi JF-Expert Member

  #2
  May 24, 2010
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  We must shame him for his deeds
   
 3. K

  Kapwani JF-Expert Member

  #3
  May 24, 2010
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 668
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sioni sababu ya wafanyakazi kuwepo ama kutokuwepo katika ziara yake kwani wala hawataongeza wa kupunguza lolote. Wakihuduria kwa wa TZ ninavyowajua kumuona JK tu watatamani hata kumuomba msamaha kwa kupanga mgomo.....tunaogopa dola kweli!
  Pili sidhani kama rais ataongeza au kupunnguza lolote hata wakienda ama wasipoenda kwa sababu kwa tathmin yake ni kwamba miaka 8 ijayo serikali haiwezi kuwaweka wanapotaka...msimamo huu unaonekana hauwezi kubadilishika hata kama watahudhuria au hawata hudhuria
  Lakini zaidi ni kwamba wamachinga, wa mama wa nyumbani wauza vitumbua,wanafunzi hilo tukio kwa ni la muhimu sana watajazana sana wakiimba na kumshangilia kila atakapopita kwa iyo uwepo au kutokuwepo kwa wafanyakazi kwenye mikutano hakuna tija kivileeeeeeee

  Usidhani huu ujio kapanga jana jioni wenzaako washamwandalia vikundi vya mganda,zeze na wauliza maswali ka iyo kusema kuwa ataongea na watu wa msafara wake ili ajisike upweke hilo halipo........wanachama na wapenzi wake wapo tayari kumpokea
   
 4. M

  Malunde-Malundi JF-Expert Member

  #4
  May 24, 2010
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,287
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  yuko hoi chali JK
   
 5. Lyangalo

  Lyangalo JF-Expert Member

  #5
  May 24, 2010
  Joined: Sep 10, 2009
  Messages: 681
  Likes Received: 77
  Trophy Points: 45
  Sioni sababu wa wafanyakazi kwenda kwa kikwete kwani alishatukana hadharani kwa yoyote atakaekwenda kama si punguani basiatakuwa kwenye payroll ya mafisadi.
   
 6. Abunwasi

  Abunwasi JF-Expert Member

  #6
  May 25, 2010
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 3,166
  Likes Received: 1,061
  Trophy Points: 280
  Hivi wenzangu nyinyi hamson dots na dashes JK kuna watu wanampenda sana na wanaamini kuwa amefanya kazi nzuri katika kipindi cha urais ingawa amekutana na vizingiti vingi kama ukame/kashfa za richmond/EPA/ Dharuba ya kuyumba kwa uchumi duniani.
  Watu hawa ni wengi na vilevile kuna wengine hawampendi kuanzia haiba, chama chake hadi uongozi wake.
  Wote kwa vile ni watanzania mnahaki zenu za kuamua lakini hakuna mnoja wenu mwenye haki ya kumnyang'aya mwenzake haki yake .
  Mwanzoni mwa November sauti zetu zote zitakuwa zimekwisha ongea hivyo ni jukumu letu kubwa litakuwa kuheshimu tofauti zetu na kumuachia mshindi aendelee. Sisi kama wanajamii tutatakiwa kutoa ushirikiano wa kutoa alternative options badala ya kukaa na kulalamika na kuponda kila kitu.
   
Loading...