Mtambuzi
Platinum Member
- Oct 29, 2008
- 8,809
- 15,419
View attachment 357161
Wafanyakazi wa Dar Serena Hoteli, NMB na Montage kwa pamoja walisherehekea siku ya mtoto wa Afrika leo tarehe 16/6/2016 kwa kutembelea kituo cha Dogodogo Centre Bunju ambacho hutoa elimu ya ufundi kwa watoto wanaoishi katika mazingira magumu au hatarishi.
Katika hafla hiyo walitoa misaada mbalimbali kwa watoto hao pamoja na kushiriki zoezi la kupaka rangi sehemu ya kulia chakula ya kituo hicho.
Wakizungumza karika Hafla hiyo wawakilishi wa kampuni hizo yaani Dar Serena Hotel ikiwakilishwa na Mkurugenzi wa Masoko ndugu Seraphin Lusala na Meneja wa mafunzo Bi Rhoda Kitila, NMB ikiwakilishwa na Madam Elizabeth na Elice Wangwe na Montage ikiwakilishwa na Madam Tedi Mapunda waliitaka jamii na taasisi mbalimbali kusaidia kituo hicho ambacho kinakabiliwa na ukata wa fedha za kuendeshea mafunzo ya ufundi kwa kutoa tenda za samani na ushonaji wa sare ili kukijengea uwezo kijiendeshe kibiashara kwani wana fani za ushonaji na ufundi seremala pamoja na fani nyingine mbalimbali.