PureView zeiss
JF-Expert Member
- Sep 5, 2016
- 10,595
- 35,336
Tanzania imepewa heshima ya kuwa mwenyeji wa Mkutano wa Nishati wa Afrika unaotarajiwa kufanyika tarehe 27 na 28 Januari 2025 jijini Dar es Salaam. Mkutano huu mkubwa utawahusisha viongozi wa juu kutoka mataifa mbalimbali ya Afrika, wakiwemo Wakuu wa Nchi na Mawaziri wa Nishati na Fedha, ambapo masuala muhimu ya nishati yatajadiliwa kwa mustakabali wa bara hilo.
Kutokana na umuhimu wa mkutano huo, Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limetangaza hatua mbalimbali za kuhakikisha usalama na utaratibu wa trafiki wakati wa tukio hilo. Aidha, barabara kadhaa jijini zitafungwa kuanzia tarehe 25 hadi 30 Januari 2025 ili kupisha misafara ya viongozi. Jeshi la Polisi limewahimiza wananchi kutumia barabara mbadala zilizopendekezwa ili kuepusha msongamano na kurahisisha shughuli za usafiri.
Barabara ambazo zitafungwa ni pamoja na Barabara ya Nyerere kutokea Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere kwenda katikati ya Jiji, Barabara ya Sokoine, Kivukoni na Lithuli kuanzia taa za Gerezani kwenda Hoteli ya Johari Rotana, Hyatt Regency hadi Ikulu, Barabara ya Ohio kutokea Kivukoni kwenda Hoteli ya Serena na Barabara ya Ghana kutokea barabara ya Ohio kwenda Hoteli ya Onomo.
Barabara nyingine ni Barabara ya Bibi Titi kutokea makutano ya barabara za Ohio na Ally Hassan Mwinyi kwenda Hoteli ya Crowne, Barabara ya Azikiwe kwenda Hoteli ya Four Points, Hoteli ya Golden Tulip City Center na Hoteli ya Holiday Inn, Barabara ya Morogoro kutokea Sokoine kwenda Hoteli ya Tiffany No. 1, Barabara ya Makunganya kutokea Azikiwe kwenda Hoteli ya Tiffany No.2, naBarabara ya Garden kutokea barabara ya Lithuli kwenda Hoteli ya Southern Sun pamoja na Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa JNICC.
Magari madogo kama bodaboda na bajaji pia hayataruhusiwa kuingia katikati ya jiji wakati wa kipindi hicho, lengo likiwa ni kuboresha usalama na kuzuia vurugu zisizotarajiwa. Jeshi la Polisi limeahidi kuweka usimamizi thabiti wa njia mbadala na kutoa maelekezo kwa wakati ili kuhakikisha huduma za usafiri zinaendelea kwa kiwango kinachokubalika.
Kutokana na hatua hizo, Jeshi la Polisi limetoa wito kwa wananchi kushirikiana kikamilifu na vyombo vya usalama kwa kufuata maelekezo na sheria zilizowekwa.
Mkutano huu unatarajiwa kuvuta hisia za kimataifa na kutoa nafasi kwa Tanzania kuonesha juhudi zake katika kushiriki na kuchangia maendeleo ya sekta ya nishati barani Afrika.View attachment 3213850