Wafanyakazi wa benki

Wafanyakazi wa benki

MPENZI JINI

Member
Joined
Sep 11, 2013
Posts
12
Reaction score
3
Habari zenu ndugu wanajamvi, mada yangu hii ya leo inatokana na matembezi yangu siku ya jana katika kutafuta mkate wa kila siku. Nikaingia benk ya nmb pale kariakoo kupeleka kacheck kangu, sasa baada yakufanya taratibu zote za kudeposit yule kijana alinihudumia akaniandikia nambayake ya simu ili nimpigie aweze kunijulisha itakapokuwa tayari na nimjulishe siku nitakayoenda kuchukua. Sasa kilichinishtua nikwann anipemba yake? Na je maadili ya kazi yao yanaruhusu hayo? Kwa kitendo hicho cha huyo mfanyakazi si kuna uwezekano kukutengenezea hata mazingira ya kufanyiwa ujambazi? Naomba mnisaidie kwa hili wanajanvi.
 
Ndo maaan yake ...usipokuwa makini utapigwa kitakomwa tena kweupeee.
 
Hapo kuna mawili...kama ni jinsia tofauti kuna mahusiano anataka kuyaanzisha pia pamoja na kufaidi tips kila ukitia mguu bank, pili inaweza kuwa mtego kama unavyosema. Huna haja ya kumripoti kwani utamripoti kwa lipi baya? Maana maadili hayazuii kuchukua namba ya mteja. Zaidi we mpotezee as long as hajachukua namba yako, au kama kachukua namba yako pia mpige chenga hasa siku utakayoenda kufanya withdraw.
 
kafanya hivyo kukusaidia coz maa nyingi namba za ofisi ni vigumu kupokelewa, sioni kama kuna tatizo kwa kuwa ni yeye aliekupa namba yake na hajaomba ya kwako, watu wanakwenda extra mile katika kukuhudumia pia hiyo pesa iko benk umedeposit sasa utaibiwaje mzee. Msipende kulaumu bila sababu.
 
Habari zenu ndugu wanajamvi, mada yangu hii ya leo inatokana na matembezi yangu siku ya jana katika kutafuta mkate wa kila siku. Nikaingia benk ya nmb pale kariakoo kupeleka kacheck kangu, sasa baada yakufanya taratibu zote za kudeposit yule kijana alinihudumia akaniandikia nambayake ya simu ili nimpigie aweze kunijulisha itakapokuwa tayari na nimjulishe siku nitakayoenda kuchukua. Sasa kilichinishtua nikwann anipemba yake? Na je maadili ya kazi yao yanaruhusu hayo? Kwa kitendo hicho cha huyo mfanyakazi si kuna uwezekano kukutengenezea hata mazingira ya kufanyiwa ujambazi? Naomba mnisaidie kwa hili wanajanvi.

huyo anataka tip ...watu wanaboa...mtu ameajiriwa kwa kufanya hyo shughuli lakini...akishaakuhudumia anataka umpe kitu kidogo wabongo nomaaa..
 
Hataki kukuibia wala kukutafutia majambazi, kwa uzoefu wangu huyo mfanyakazi wa NMB anataka tu umfahamu ili unapokuwa na maswala ya kufanya Benki akupe msaada wa hapa na pale. Ni kawaida tu hasa kwa sisi tunaokwenda ku-deposit cheque kuwa na mahusiano ya kusaidipiana na hawa jamaa. Wakati mwingine hatuna muda wa kusubiri ule muda wa cheque ku-mature so kama unafahamiana naye anakufanyia mipango unapata mzigo wako within seconds. Ila pia usisahau kumpa tip maana ndio sababu ya hao Bank tellers kutafuta kufahamiana na wateja. However hauna haja ya kumwambia siku utakapokuwa unaenda fanya Withdraw maana hiyo ni issue binafsi na haimuhusu.
 
Huyo mfanyakazi anatumia vizur taaluma ya Customer Relationship Management anapenda awe karibu na mteja ili amhudumie vizur.
 
wabongo bwana ukikuta huduma mbovu unalalamika ukipata huduma nzuri unawaza kuibiwa yaan hyo jamaa kukufanyia favour ushaanza kumuwazia mabaya

hakika mkuu,hatuna jema watanzania yaan tumeumbwa kufikiri hasi kwa kila jambo.
 
kafanya hivyo kukusaidia coz maa nyingi namba za ofisi ni vigumu kupokelewa, sioni kama kuna tatizo kwa kuwa ni yeye aliekupa namba yake na hajaomba ya kwako, watu wanakwenda extra mile katika kukuhudumia pia hiyo pesa iko benk umedeposit sasa utaibiwaje mzee. Msipende kulaumu bila sababu.
Tushazoe huduma mbovu tukihudumiwa vema tunawaza kuibiwa, shame! Siku hizi hata baadhi ya madaktari wanakupa namba zao za simu ili utoe feedback ya afya yako esp dawa zinavyo react kwenye mwili wako ama +vely or -vely. Na mfano mimi ni female, nshapewa namba na dr mwanamke na mwanaume, yote ni kutaka kujua naendeleaje baada ya matibabu. Na they never ask for my number, wao ndo wanakupatia namba and I find it very ok and feel cared

The truth shall set u free.
 
kama wewe ni ke basi kuna mawili aidha kakupenda na kapenda kupata mawasiliano yako au, anataka ukifika benki kupata huduma usisumbuke hasa ukiwa na pesa nyingi za ku deposit au kutoa. mi naona huna haja ya kifikiria vibaya.
 
Kupewa namba ya mtu kazini ni jambo zuri tena katika kurahisisha kazi. Once you have his number you can contact him directly kitu ambacho kitakurahisishia kupata huduma. Ni mara ngapi tunapiga namba 100 huduma kwa wateja hazipokelewi au haturidhiki na majibu yao? But kama una mtu kwenye huo mtandao ni rahisi kuwasiliana na kumueleza shida yako akakusaidia. Kama eti ni hizo hela zako 10mil anataka kukuibia sidhani hata kama angehitaji namba yako na kama ni mapenzi huna haja ya kulalamika,atakutongoza utakataa akikusumbua unachukua hatua stahiki sasa kimbelembele kwenye mitandao cha nini? Tubadilike watanzania.
 
Kama 15 hivi, naona ndo maana huyo jamaa kapagawa

Nijuavyo mimi, cheki za benki tofauti siku hizi zimewekewa kiwango cha mwisho 10 M, na hilo ni agizo la BoT. Kama cheki yako ni ya NMB haitakiwi ichukue muda mrefu kuwa tayari ku withdraw.

Kuwa na namba ya huyo kijana aliyekuhudumia sioni kama ni tatizo, nnachopinga ni yeye kujua siku unayoenda kuchukua pesa zako. Sio kazi yake wala hapaswi kujua jinsi unavyoiendesha account yako.
 
Tushazoe huduma mbovu tukihudumiwa vema tunawaza kuibiwa, shame! Siku hizi hata baadhi ya madaktari wanakupa namba zao za simu ili utoe feedback ya afya yako esp dawa zinavyo react kwenye mwili wako ama +vely or -vely. Na mfano mimi ni female, nshapewa namba na dr mwanamke na mwanaume, yote ni kutaka kujua naendeleaje baada ya matibabu. Na they never ask for my number, wao ndo wanakupatia namba and I find it very ok and feel cared

The truth shall set u free.

Kuna watu wanakera mkuu unatamani hata uwapige risasi. Jana nimekaa kwenye foleni bank halafu nafika pale naambiwa ninachohitaji ni hadi siku ya jumanne tu. Nilitamani hata nimtukane yule mtu pale kwanini ananiona kwenye foleni na haniambii( sasa sijui angejuaje!!!!) halafu mtu hapa anapewa namba ya simu analalamika anaona ametamaniwa au hicho kihela kinamchanganya.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom