Noti mpya tz
JF-Expert Member
- Mar 23, 2011
- 974
- 247
Imenitokea mwenyewe live leo kwenye ofisi za TRA makao makuu ya mkoa wa Arusha.
Ni hivi, mwaka juzi nilijiandikisha kama mlipa kodi mkoani mwanza na lengo langu kuu ilikuwa ni kupata TIN namba ili nikate leseni ya kuendesha magari, bahati mbaya nikapata safari nje ya nchi kabla sijapata tin namba ikabidi niahirishe zoezi la leseni niwahi mbele.
Niliporudi mwaka jana makao yangu kwa muda yakawa Singida na ikabidi nikatie huko leseni yangu. Walitafuta jina kwenye system yao wakalipata hivyo nikafanya process nikapata leseni.
Miezi miwili iliyopita nilianzisha kibiashara changu hapa Arusha, kimeendelea baadae nikajiambia mwenyewe kuwa ni vizuri kukata leseni ya biashara kwani sipendi vitu bubu, leo nimeamka nikaenda tra nikakutana na dada mmoja akanielekeza nipande ghorofani nikamuone mama mmoja anaitwa mama KESSY.
Ngodongodo huyo kwa mama kessy, nikajieleza kila kitu na nikauliza uwezekano wa kutumia TIN namba yangu niliyoikata mwanza ili nikate leseni ya biashara na mambo mengine.
La haula, Mama kessy akaniambia ni lazima niende mwanza kwanza kwenye ofisi za TRA halafu ndiyo nije kukata leseni. Nikauliza namba yangu si iko kwenye system kwanini nisifanyiwe process nikalipa hapa arusha? Mama akasema nisimfundishe kazi ni lazima niende mwanza.Nini kunanipeleka mwanza?
Ni kwamba, Nilipokata tin namba sikupewa certificate ya TIN namba so ni lazima niende mwanza wakaniprintie ile certificate ndipo nije arusha kulipa kodi.
Mimi si mtaalam wa tra, inawezekana taratibu ndivyo zilivyo. Shwaki langu ni hiki.Kwani hakujipa muda kunipa maelezo ya kutosha ni kwanini napaswa kwenda mwanza?
Je, ni kweli kwamba tin namba certificate haiwezi kuprintiwa sehemu nyingie? Na je, siwezi kulipa leseni kwa kutumia tin namba yangu inayoonekana kwenye system ya tra kama nilivyofanya singida wakati wa kukata leseni?
Swali la mwisho, Ni wananchi wangapi wenye moyo wa kulipa ushuru wamekatishwa tamaa na wafanyakazi wa TRA?
Nisaidieni