Wafanyakazi Tanesco wataja mafisadi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wafanyakazi Tanesco wataja mafisadi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by dosama, May 20, 2012.

 1. dosama

  dosama JF-Expert Member

  #1
  May 20, 2012
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 786
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  WAFANYAKAZI wa Shirika la Ugavi wa Umeme nchini (TANESCO) wameibua hujuma zinazofanywa na baadhi ya wafanyakazi wa shirika hilo wasio waaminifu na kukabidhi majina hayo kwa Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo.

  Wafanyakazi hao walifikia hatua hiyo jana katika mkutano wao na waziri huyo alipotembelea shirika hilo kwa mara ya kwanza tangu alipoteuliwa kushika wadhifa huo.

  Baada ya kuibua madai hayo na kupitishwa na makaratasi, wafanyakazi hao waliandika majina ya mafisadi hao na kumkabidhi waziri ambaye aliondoka nayo na kuahidi kuyafanyia kazi.

  Katika mkutano huo, baada ya wafanyakazi hao kuibua madai hayo na kudai kuwa wanawafahamu watu hao kwa majina, Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Eliakimu Maswi, aliwataka wawataje kwa majina watu hao, ili waweze kushughulikiwa.

  Maswi alisema haiwezekani miaka 50 ya Uhuru bado nchi inakabiliwa na tatizo la umeme na wananchi wanaendelea kulalamika, hivyo ni wakati wa kuwashughulikia wale wote ambao ni wazembe na wala rushwa ambao wanarudisha nyuma maendeleo ya shirika hilo.

  “Mkiona ni vigumu kusema hadharani andikeni muweke kwenye boksi ili waziri aondoke nayo. Wajibu wangu ni kutekeleza majukumu yangu, sitamwonea mtu yeyote aibu,” alisema katibu mkuu huyo.

  Aliwatahadharisha watumishi hao kuwa na uhakika na ushahidi kwa majina watakayoandika, ili hatua ziweze kuchukuliwa kwa walengwa.

  Katibu mkuu huyo alisema hataki kuona mgawo wa umeme ukiendelea nchini na kuongeza kuwa baadhi wa watumishi hawana nidhamu wala heshima kwa kuwa miongoni mwao kuna vishoka.

  “Wezi wa mafuta ya transfoma mnao humu na mnawajua. Uhujumu hauwezi kuwa wizarani tu, hata hapa upo,” alisema.

  Katibu mkuu huyo alitoa agizo hilo, baada ya Mwenyekiti wa Kamati ya Majadiliano wa TANESCO, Abdul Mkama, kueleza kuna watu wachache wanaoharibu taswira ya shirika hilo ambao wanawajua kwa majina na wapo tayari kuwataja.

  Mkama alikiri mbele ya watendaji wakuu wizarani kuwa, kwa makusudi wanaamini viongozi wa shirika hilo, wana nia ya kuliua ili wawaweke wawekezaji wa kufua umeme.

  “Uwezo tunao lakini biashara na siasa haviendi pamoja ni sawasawa na kupenga kamasi huku unataka kupiga mluzi,” alisema Mkama.

  Naye mfanyakazi Kamuri Malangwa wa Kituo cha Ufuaji Umeme megawati 100, alisema wawekezaji wanathaminiwa zaidi na serikali kuliko TANESCO kwa kuwa katika kutumia gesi, TANESCO inakuwa ya mwisho kuipata hadi Kampuni ya Symbion ipate ya kutosha na wengine.

  “Mara nyingi tunaambiwa tuzime mitambo gesi haitoshi, ili wenye gesi wauze kwa makampuni mengine, matokeo yake kituo hiki kila siku kinatengeneza chini ya kiwango cha ufuaji wa umeme. Inafikia mahala sisi wenyewe tunavutana mashati, ili wengine watengeneze pesa,” alisema.

  Alisema hivi sasa shirika hilo limekuwa machinga wa umeme, pamoja na kuwakaribisha wawekezaji, linanunua umeme senti 27 na kuuza kwa senti 11, lakini wengine wananufaika kwa kuwa wao ndio wanajua kutengeneza fedha.

  Alisema kutokana na hali hiyo kituo hicho kitafungwa muda si mrefu kwa kuwa hakuna fedha za kukarabati injini.

  Naye Raison Mwambage, alisema IPTL imelalamikiwa kwa mikataba mibovu, mawaziri mbalimbali wameshapita katika wizara husika bila kurekebisha tatizo hilo.

  Akizungumza katika mkutano huo, Waziri Muhongo alisema hivi sasa ni wakati wa vitendo, si wakati wa kusikiliza hotuba, risala wala sera kwa kuwa vimekuwa vikitolewa siku zote, lakini hakuna mabadiliko.

  Waziri huyo alikiri wananchi kukabiliwa na maisha magumu baada ya kuletwa mitambo ya kuzalisha umeme, kwani dunia ni ya ushindani na hivyo anafahamu kuna watu wanaotengeneza fedha ambao wanakwamisha masuala ya umeme yasisonge mbele.

  Waziri huyo alikiri kuwa mikataba mibovu huiyumbisha nchi na kwamba kinachofanyika sasa ni kuipitia na kuhakikisha mikataba mingine haitakuwa na tatizo.

  Alisema mikataba yote itakayosainiwa sasa itakuwa ni ya wazi, na kusema kuwa hatasaini mikataba mibovu.

  Alisema tatizo la umeme nchini linatokana na kutegemea chanzo kimoja cha maji na kusema kuwa ili TANESCO iendelee alishauri vyanzo vitakuwa makaa ya mawe, gesi asilia, umeme wa maji, jua, upepo na ule unaotoka ardhini.

  Kwa upande wake, Naibu Waziri anayeshughulikia Nishati, George Simbachawene alisema atatumia akili, uwezo na ujuzi alionao, ili nchi itoke kwenye tatizo hilo.

  Naye Naibu Waziri anayeshughulikia Madini, Stephen Masele, alisema hawatasita kuwaondoa wote watakaokwamisha safari hiyo kwa kuwachukulia hatua.
   
 2. Osaka

  Osaka JF-Expert Member

  #2
  May 20, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 1,766
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Pamoja na hayo, jitihada za makusudi zifanyike kubaini vishoka wa nje na kuwaadabisha.
   
 3. Arvin sloane

  Arvin sloane JF-Expert Member

  #3
  May 20, 2012
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 963
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  Tz kuna vioja sasa hao mafisadi wa tanesco kama wanafahamika tena kwa majina kuwa wanalihujumu shirika kwa nini wasichukuliwe hatua?? mpaka kina ngeleja weang'oke haya sasa huyo Muhongo kapewa majina atakaa kimya mpaka siku akitaka kong'olewa ndio utasikia anajitetea.
   
 4. Rweye

  Rweye JF-Expert Member

  #4
  May 20, 2012
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 15,058
  Likes Received: 3,085
  Trophy Points: 280
  Matendo hukidhi haja maridhawa kuliko maneno.. Let,s wait&see
   
 5. Z

  Zimamoto JF-Expert Member

  #5
  May 20, 2012
  Joined: Mar 28, 2012
  Messages: 464
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  Mafisadi wako sehemu na wanafahamika. Tatizo ni kuogopana, kuleana na dhana nzima ya kusubiri 'kujiridhisha'. Tutafika?
   
 6. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #6
  May 20, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,874
  Likes Received: 6,228
  Trophy Points: 280
  wameamua kudili na dagaa? Lini watadili na papa?
   
 7. N

  NasDaz JF-Expert Member

  #7
  May 20, 2012
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 11,308
  Likes Received: 1,655
  Trophy Points: 280
  Nchi hii palishawahi kutolewa orodha ya wauza unga ambayo ilipelekwa kwa Mzee Makamba (wakati akiwa RC wa DSM)!! Hadi leo hii hakuna kilichofanyika! Hivi majuzi tu ikatolewa orodha ya viongozi wa dini wauza mihadarati....hata JK alizungumzia suala hili....hawa wakaambiwa wajirekebishe!!! Hivyo, hiyo orodha iliyopewa waziri ni upuuzi mwingine ambao umeshazoeleka na katu hauwezi kuwa na positive impact kwa taifa. Ni kheri orodha hiyo ingewekwa hapa JF kuliko kumpa waziri!
   
 8. W

  WEMBE WENGE Senior Member

  #8
  May 20, 2012
  Joined: Mar 6, 2011
  Messages: 127
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  poleni sana Mh waziri na team yako kama yaliyokupeleka wizarani ni kufanya kazi ya Polisi basi Watanzania hatutashuhudia mabadiliko yoyote wizara ya nishati na madini
  Pole sana unataka kushindwa kabla hujaanza.
  Waziri ni mtu wa Policy na Strategy sisi watanzania wenzako wachovu kabisa tunanufaikaje na hatua zako za kuwashughulikia hao mafisadi. Wewe hukuwa waziri na wala hayakuhusu
  mimi naamini na watanzania wenzangu tulitarajia tusikiwe una mikakati gani ya kileo ya kutupatia umeme ukiachana na ahadi za megawati lukuki toka kwa mtangulizi wako
  Maswala ya kimenejimenti ya TANESCO na wizarani kwako sisi hayatuhusu kabisa endelea kivyako.
  Tunachohitaji ni umeme na kujua utawadhiti vipi akina ABG wanao yuna magold yetu kwa kutupatia shanga za kiunoni
  thanks few more comments letter

  Wafanyakazi hao walifikia hatua hiyo jana katika mkutano wao na waziri huyo alipotembelea shirika hilo kwa mara ya kwanza tangu alipoteuliwa kushika wadhifa huo.

  Baada ya kuibua madai hayo na kupitishwa na makaratasi, wafanyakazi hao waliandika majina ya mafisadi hao na kumkabidhi waziri ambaye aliondoka nayo na kuahidi kuyafanyia kazi.

  Katika mkutano huo, baada ya wafanyakazi hao kuibua madai hayo na kudai kuwa wanawafahamu watu hao kwa majina, Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Eliakimu Maswi, aliwataka wawataje kwa majina watu hao, ili waweze kushughulikiwa.

  Maswi alisema haiwezekani miaka 50 ya Uhuru bado nchi inakabiliwa na tatizo la umeme na wananchi wanaendelea kulalamika, hivyo ni wakati wa kuwashughulikia wale wote ambao ni wazembe na wala rushwa ambao wanarudisha nyuma maendeleo ya shirika hilo.

  “Mkiona ni vigumu kusema hadharani andikeni muweke kwenye boksi ili waziri aondoke nayo. Wajibu wangu ni kutekeleza majukumu yangu, sitamwonea mtu yeyote aibu,” alisema katibu mkuu huyo.

  Aliwatahadharisha watumishi hao kuwa na uhakika na ushahidi kwa majina watakayoandika, ili hatua ziweze kuchukuliwa kwa walengwa.

  Katibu mkuu huyo alisema hataki kuona mgawo wa umeme ukiendelea nchini na kuongeza kuwa baadhi wa watumishi hawana nidhamu wala heshima kwa kuwa miongoni mwao kuna vishoka.

  “Wezi wa mafuta ya transfoma mnao humu na mnawajua. Uhujumu hauwezi kuwa wizarani tu, hata hapa upo,” alisema.

  Katibu mkuu huyo alitoa agizo hilo, baada ya Mwenyekiti wa Kamati ya Majadiliano wa TANESCO, Abdul Mkama, kueleza kuna watu wachache wanaoharibu taswira ya shirika hilo ambao wanawajua kwa majina na wapo tayari kuwataja.

  Mkama alikiri mbele ya watendaji wakuu wizarani kuwa, kwa makusudi wanaamini viongozi wa shirika hilo, wana nia ya kuliua ili wawaweke wawekezaji wa kufua umeme.

  “Uwezo tunao lakini biashara na siasa haviendi pamoja ni sawasawa na kupenga kamasi huku unataka kupiga mluzi,” alisema Mkama.

  Naye mfanyakazi Kamuri Malangwa wa Kituo cha Ufuaji Umeme megawati 100, alisema wawekezaji wanathaminiwa zaidi na serikali kuliko TANESCO kwa kuwa katika kutumia gesi, TANESCO inakuwa ya mwisho kuipata hadi Kampuni ya Symbion ipate ya kutosha na wengine.

  “Mara nyingi tunaambiwa tuzime mitambo gesi haitoshi, ili wenye gesi wauze kwa makampuni mengine, matokeo yake kituo hiki kila siku kinatengeneza chini ya kiwango cha ufuaji wa umeme. Inafikia mahala sisi wenyewe tunavutana mashati, ili wengine watengeneze pesa,” alisema.

  Alisema hivi sasa shirika hilo limekuwa machinga wa umeme, pamoja na kuwakaribisha wawekezaji, linanunua umeme senti 27 na kuuza kwa senti 11, lakini wengine wananufaika kwa kuwa wao ndio wanajua kutengeneza fedha.

  Alisema kutokana na hali hiyo kituo hicho kitafungwa muda si mrefu kwa kuwa hakuna fedha za kukarabati injini.

  Naye Raison Mwambage, alisema IPTL imelalamikiwa kwa mikataba mibovu, mawaziri mbalimbali wameshapita katika wizara husika bila kurekebisha tatizo hilo.

  Akizungumza katika mkutano huo, Waziri Muhongo alisema hivi sasa ni wakati wa vitendo, si wakati wa kusikiliza hotuba, risala wala sera kwa kuwa vimekuwa vikitolewa siku zote, lakini hakuna mabadiliko.

  Waziri huyo alikiri wananchi kukabiliwa na maisha magumu baada ya kuletwa mitambo ya kuzalisha umeme, kwani dunia ni ya ushindani na hivyo anafahamu kuna watu wanaotengeneza fedha ambao wanakwamisha masuala ya umeme yasisonge mbele.

  Waziri huyo alikiri kuwa mikataba mibovu huiyumbisha nchi na kwamba kinachofanyika sasa ni kuipitia na kuhakikisha mikataba mingine haitakuwa na tatizo.

  Alisema mikataba yote itakayosainiwa sasa itakuwa ni ya wazi, na kusema kuwa hatasaini mikataba mibovu.

  Alisema tatizo la umeme nchini linatokana na kutegemea chanzo kimoja cha maji na kusema kuwa ili TANESCO iendelee alishauri vyanzo vitakuwa makaa ya mawe, gesi asilia, umeme wa maji, jua, upepo na ule unaotoka ardhini.

  Kwa upande wake, Naibu Waziri anayeshughulikia Nishati, George Simbachawene alisema atatumia akili, uwezo na ujuzi alionao, ili nchi itoke kwenye tatizo hilo.

  Naye Naibu Waziri anayeshughulikia Madini, Stephen Masele, alisema hawatasita kuwaondoa wote watakaokwamisha safari hiyo kwa kuwachukulia hatua.[/QUOTE]
   
 9. WAHEED SUDAY

  WAHEED SUDAY JF-Expert Member

  #9
  May 20, 2012
  Joined: Jun 24, 2011
  Messages: 7,157
  Likes Received: 1,249
  Trophy Points: 280
  Sitashangaa tanesco kesho kuja na taarifa ya kukanusha haya yaliyosemwa maana imekuwa ni kawaida kulindana baada ya kuona mambo yanakwenda kombo
   
 10. Twilumba

  Twilumba JF-Expert Member

  #10
  May 20, 2012
  Joined: Dec 5, 2010
  Messages: 6,148
  Likes Received: 878
  Trophy Points: 280
  Ha haa haaa hizo ni mbwembwe tu, Hao wazungu wa Songas, Symbion, IPTL, Aggreko, Scada na kampuni nyingine zinazofanya biashara ya kuwauzia Tanesco umeme zimejiwekea mizizi huko mawizarani na ukweli ni kwamba hata ile top up ya mauzo halisi ya umeme ni cha juu cha hao wakubwa wa wizarani na hata kule mjengo mweupe!

  Mh. Waziri wa nishati kwa kweli kwa sasa hakuna ajualo kuhusu hiyo wizara ni lay man kabisa kwenye hayo madudu ya wizara, na wanachofanya sasa hivi wanamsoma ili wamfanyie suprise ya kumpa jumba moja tu pale mikocheni na from there hizo juhudi alizoanza nazo zitakuwa zimefikia kikomo!
   
 11. Ukwaju

  Ukwaju JF Bronze Member

  #11
  May 20, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 8,287
  Likes Received: 810
  Trophy Points: 280
  Kweli tumeliwa hao wafanyakazi wa Tanesco waongo kwa nini hayo majina wasitupatie humu JF
  Siku za nyuma walionekana humu wakjb tuhuma za mgawo baada ya kubandikwa humu ubadhiluufu wao
  Atokee tu mjanja aruhusu makampuni binafsi km ya simu hao wafanyakz wataheshimu km wa TTCL
   
 12. N

  Njoka Ereguu JF-Expert Member

  #12
  May 20, 2012
  Joined: Apr 7, 2012
  Messages: 822
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 35
  Porojo akipewa hicho kifungu ndiyo kwisha, hiyo mikataba ni nani anaipitia? siyo walewale waliokuwepo tangu zamnai ambao watacheza na maneno?
   
 13. N

  Nteko Vano JF-Expert Member

  #13
  May 20, 2012
  Joined: Feb 28, 2012
  Messages: 436
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0

  Kwahiyo unasema maneno ya Maige kweli kuwa ukipambana na hao watu unang'oka wewe?

  Kwahiyo inabidi tujadili wafanywe nini hao wazungu? maana ndio wanaturydisha nyuma.
   
 14. H

  Hacha Member

  #14
  May 20, 2012
  Joined: May 20, 2012
  Messages: 11
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Hapo sasa patamu!!

  Waziri Murraa, Katibu mkuu Murraa!!!!!

  Yetu macho na masikio!
   
 15. andishile

  andishile JF-Expert Member

  #15
  May 22, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 1,430
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 145
  hapooo chacha!
   
Loading...